Social Icons

Home

HABARI MPYA KATIKA BLOG

Friday, November 27, 2015

MSIKILIZE HAPA KAMISHNA WA BAJETI AKIKANUSHA JUU YA RAISI KIKWETE KUKOMBA PESA ZOTE HAZINA
Serikali imekanusha taarifa zinazosambazwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa amekomba fedha hazina na kuiacha Serikali bila fungu lolote.
Hayo yamesemwa jijini dare es salaam na Kamishina wa Bajeti kutoka Wizara ya Fedha Bwa. John Cheyo huku akiwataka wananchi kupuuza habari hiyo kwani hazina ukweli wowote.
“Hazina inazo pesa za kutosha  na tunajivunia kufanya uchaguzi wa mwaka huu,  kununua mashine za BVR  kwa kutumia pesa za watanzania bila kutegemea msaada wowote kutoka nje ya nchi  na kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu mwaka huu” alisema Bwa. Cheyo.
Pia aliongeza kuwa serikali imeendelea kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa bomba la gesi ambalo limekamilika hivi karibuni, vinu vya kuchakata gesi na ujenzi wa barabara nchini.
Aliendelea kusema kwamba mfumo wa serikali wa bajeti unaiwezesha serikali kupanga vipaumbele vya matumizi kulingana na bajeti ilivyopangwa ambapo fedha zinazokusanywa kupitia mfuko mkuu wa serikali ndizo hutumika.
Bajeti iliyoidhinishwa na Bunge kwa kipindi cha 2015-2016 ni shilingi Trilioni 22.5 na bajeti hiyo inatengenezewa mpango wa makusanyo na matumizi kwa kulipia mishahara ya wafanyakazi na miradi mbalimbali iliyoidhinishwa.
Pia katika matumizi mengine bajeti hiyo inalipia chakula cha wanafunzi, mikopo ya wanafunzi elimu ya juu, ununuzi wa dawa na vifaa tiba na chakula cha hifadhi ya taifa

MSIKILIZE HAPA KAMISHNA WA BAJETI AKITOA UFAFANUZI
Read more ...

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI WAZIRI MKUU AWASIMAMISHA KAZI MAAFISA 
    
                                                       
​WATANO TRA
*Ni kwa upotevu wa makontena 349, yana thamani ya sh. bilioni 80/-

WAZIRI MKUU Majaliwa Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi maafisa watano na watumishi watatu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutokana na upotevu wa makontena 349 yenye thamani ya zaidi ya sh. bilioni 80/-.

Akizungumza na viongozi wa Mamlaka ya Bandari pamoja na viongozi wa TRA katika ziara ya kushtukiza leo mchana (Ijumaa, Novemba 27, 2015), Waziri Mkuu amewataka Kamishna Mkuu wa TRA, Bw. Rished Bade na Naibu Kamishna Mkuu wa TRA, Bw. Lusekelo Mwaseba wahahakikishe wanashirikiana na polisi kufuatilia upotevu huo na kwamba fedha hizo zinapatikana na zinarudi Serikalini.

Akitangaza uamuzi huo baada ya kufanya kikao na baadhi ya viongozi wa Serikali bandarini hapo, Waziri Mkuu aliwataja maafisa waliosimamishwa kazi kuwa ni Kamishna wa Forodha, Bw. Tiagi Masamaki na Mkuu wa Kituo cha Huduma kwa Wateja, Bw. Habibu Mponezya.

“Hawa wanasimamishwa kazi. IGP ninaagiza hawa watu wakamatwe na kuisaidia polisi. Hati zao za kusafiria zikamatwe na mali zao zikaguliwe kama zinaendana na utumishi wa umma,” alisema Waziri Mkuu.

Maafisa wengine waliosimamishwa kazi ni Mkuu wa kitengo cha TEHAMA, Bw. Haruni Mpande, Bw. Hamisi Ali Omari (hakutaja ni wa idara gani), na Mkuu wa Kitengo cha Bandari Kavu (ICD In-Charge), Bw. Eliachi Mrema. “Hawa wanasimamishwa kazi hadi uchunguzi utakapokamilika na pia wawe mikononi mwa polisi,” alisema.

Pia aliagiza watumishi watatu wa mamlaka hiyo wahamishwe kutoka Dar es Salaam na kupelekwa mikoani. Watumishi hao ni Bw. Anangisye Mtafya, Bw. Nsajigwa Mwandengele na Bw. Robert Nyoni.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemwagiza Katibu Mkuu wa Hazina, Dk. Servacius Likwelile ambaye alikuwepo kwenye kikao hicho, kuhakikisha kuwa anapeleka wataalamu kutoka Wakala wa Serikali Mtandao (e-Govt) haraka iwezekanavyo ili wakakague mifumo ya taarifa na kubaini jinsi ambavyo wizi huo unafanyika.

“Ninataka uchunguzi uanze kufanyika mara moja, tafuteni njia ambazo zinatumika kama mianya ya wizi kutokea hapa bandarini hadi kwenye ICDs. Nataka hayo makontena yatafutwe hadi yajulikane yako wapi, na fedha hiyo ihakikishwe inarudi serikalini,” alisema.

Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Bw. Ernest Mangu, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Florens Turuka, Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya DSM, Suleiman Kova, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari (TPA), Bw. Awadh Massawe na viongozi mbalimbali kutoka TRA na TPA.

Mapema akijibu maswali ya Waziri Mkuu, Kamishna Mkuu wa TRA, Bw. Bade alikiri kwamba kuna upotevu wa makontena ambao huwa unafanyika kati ya bandarini na ICDs na hasa ICD ya Ubungo. Akitoa ufafanuzi, alisema kwamba walifanya ukaguzi kwenye ICD moja na kukuta makontena 54 yamepotea kwa njia za wizi. “Hata hivyo, tulipoendelea na ukaguzi, namba iliongezeka na kufikia 327. Tunaendelea kufuatilia kwa kushirikiana na TAKUKURU. Mmiliki wa ICD ametakiwa kulipa faini sh. bilioni 12.6/- na ameshalipa sh. bilioni 2.4/-,” alifafanua.

Alipoulizwa na Waziri Mkuu kama ana majina ya watumishi wanaohusika na wizi huo, Bw. Bade akakiri kwamba anayo lakini siyo kwa wakati huo labda ayapate kutoka kwa wasaidizi wake. Ndipo Waziri Mkuu akamuonyesha orodha ya makontena 349 yenye taarifa zote hadi namba za magari yaliyobeba mizigo hiyo na Bw. Bade akakiri kwamba orodha hiyo ni ya kweli.

“Kwa utaratibu huo hatuwezi kufika, labda baadhi ya watu waondolewe kazini”. Ndipo akaanza kutaja majina ya maafisa hao waliosimamishwa kazi.

(mwisho) 

Waziri Mkuu 

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S.  L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM

IJUMAA, NOVEMBA 27, 2015
Read more ...

Wednesday, July 15, 2015

HATIMAYE CHAMA CHA WANANCHI CUF KIMETOA MSIMAMO WAO JUU YA MGOMBEA WA UKAWA

Chama cha wananchi CUF leo asubuhi kupitia viongozi wake  kimetoa ufafanuzi wakati kikiongea na waandishi wa habari juu ya taarifa zinazoendelea kutapakaa nakutoa  ufafanuzi  wa  mambo yafuatayo
1.CUF wamedhibitisha kuwa hawajajitoa UKAWA.
2.Kuhusu kutohudhuria kikao cha UKAWA jana wamedhibistisha kuwa hawakuhudhuria  kwasababu hawakupewa taarifa za kikao mapema hivyo wakashindwa kuhudhulia.
3.Kuhusu UKAWA kuchagua mgombea wa urais wamesema hawamtambui aliyechaguliwa na watakaa wote tarehe 25 mwezi huu kuamua nani atakuwa mgombea wa urais kupitia UKAWA.

Read more ...

Sunday, July 12, 2015

Hii ndiyo Historia ya Samia Suluhu Hassan wa CCM

Historia ya Samia Suluhu Hassan wa CCM
Chama tawala nchini Tanzania CCM ambayo imekuwa katika kongamano la kitaifa mjini Dodoma ilimchagua bibi huyo mwenye umri wa miaka 54 mchache wa maneno na mwenye asili ya Zanzibar kushirikiana na dakta Magufuli.
Lakini bi Samia Suluhu Hassanni Nani ?
Bi Samia Suluhu Hassan ni mtanzania mwenye asili ya Zanzibar
Kiongozi huyu pia amewahi kushikilia nyadhifa za uwaziri katika Serikali ya Muungano na ya Zanzibar akihudumu kama waziri katika afisi ya makamu wa rais
Ni mwanamke wa Kwanza Mgombea Mwenza
Tangazo hilo limewashangaza wengi kwani Bi Samia Suluhu hakuwa miongoni mwa wagombea wa kiti cha urais.
Tamko la kuwa Bi Samia ni mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi imeweka historia kwa kuwa mgombea mwenza wa kwanza nchini humo ambaye ni mwanamke.
Bi Samia alikamilisha masomo ya shule ya upili mwaka wa 1976 na akaajiriwa kama mchapishaji katika wizara ya mipango na maendeleo ya nchi kazi ambayo aliifanya huku akiendelea na masomo yake hadi alipohitimu katika chuo kikuu cha Manchester.
Read more ...

HATIMAYE EDWARD LOWASA AANDIKA SENTESI NZITO YENYE UTATA MUDA HUU MTANDAONI KWAKE

Nawe una lipi la kumuambia Lowassa?! Toa maoni yako hapo chini!
Read more ...

TAZAMA VIDEO YA HAYATI MWALIMU J.K NYERERE AKIZUNGUMZIA KUKATWA KWA EDWARD LOWASA KATIKA UCHAGUZI WA MWAKA 1995

Read more ...

Saturday, July 11, 2015

BREAKING NEWZZZ....HUYU JAMAA AKAMATWA NA MABILIONI YA PESA KWENYE BEGI MJINI DODOMA MDA HUU ...NI HATARIII

HUYU JAMAA MWENYE ASILI YA KIHINDI ANASWA NA HIZI PESA HAIJAFAHAMIKA BADO NI KWA AJILI YA KUFANYIA NINI...ENDELEA KUFWATILIA HAPA UPATE HABARI ZOTE

Read more ...