Skip to main content

Posts

WANANCHI WA JIMBO LA ARUSHA MJINI[CHADEMA] WAMPINGA HADHARANI KWA MABANGO MBUNGE WAO, GODBLESS LEMA

Soma Bango hilo, wafuasi wa CHADEMA jijini Arusha ,walioambatana na Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Monduli Bw. Amani Salenga wakionyesha bango hilo kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) ,wakidai kuwa Mbunge Lema ndie chanzo cha vurugu kwenye Chama kwa kuanzisha kikundi cha vijana ambacho kimekuwa tishio kwa wale wanaojaribu kupingana na sera za Mbunge huyo. pia wamedai kuwa Arusha kwa sasa CHADEMA imegawanyika katika makundi mawili, amabyo ni CHADEMA ASILI na CHADEMA FAMILY.

Kampuni 100 bora zatajwa

Dar es Salaam. Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda amesema kuwa, Serikali itaendelea kutengeneza mazingira mazuri ya kufanya biashara ili wawekezaji wa nje na ndani waweze kutekeleza majukumu yao bila kikwazo. Dk Kigoda aliyasema hayo juzi usiku alipokuwa kwenye hafla ya kuzitambua Kampuni 100 Bora zinazokua kwa kasi nchini (Top 100 Mid–Sized Companies), ambapo Kampuni ya Kipipa Millers Limited ya jijini Mwanza ilishika nafasi ya kwanza. Kampuni hizo zilitambuliwa na kupewa tuzo kutokana na shindano linaloendeshwa na Kampuni ya Mwananchi Communications (MCL) na KPMG Tanzania na kudhaminiwa na Benki ya NBC pamoja na Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE). Dk Kigoda alisema shindano hilo linaimarika kila mwaka na lina nafasi kubwa ya kuimarisha uchumi kwa Kampuni za Afrika Mashariki. Alisema ili kampuni hizo ziweze kufikia mafanikio, Serikali itajitahidi kuweka mazingira yatakayoziwezesha kufanya shughuli zake vizuri na kufanya uzalishaji kwa gharama n...

SAMATTA AFUNGA, LAKINI SFAXIEN YAIUA MAZEMBE DAKIKA YA 88 LUBUMBASHI, WAMKOSA MWALI WA CAF HIVI HIVI!

WASHAMBULIAJI Mbwana Ally Samatta na Thomas Emanuel Ulimwengu leo wameshindwa kutimiza ndoto zao za kuwa Watanzania wa kwanza kuvaa Medali za Dhahabu za michuano ya Afrika baada ya klabu yao, Tout Puissant Mazembe kushinda 2-1 dhidi ya CS Sfaxien ya Tunisia, katika fainali ya pili ya Kombe la Shirikisho Uwanja wa Mazembe mjini Lubumbashi, hivyo kuangushwa kwa matokeo ya jumla ya 3-2, baada ya awali kufungwa 2-0 Uwanja Olympique de Rades mjini Tunis katika Fainali ya kwanza. Mazembe ilitakiwa kushinda mabao 3-0 Jana nyumbani ili kutwaa taji hilo, na ilionekana kama ingeweza kufanya hivyo baada ya kuongoza kwa mabao 2-0 hadi dakika ya 88, yaliyofungwa na nyota wa Mali, Traore Cheibane dakika ya 10 na Samatta dakika ya 24. Lakini wakati Mazembe wakiwa bize na mashambulizi ya kusaka bao la tatu dakika za lala salama, Ben Youssef akaifungia bao muhimu Sfaxien dakika ya 88 na kuzima ndoto za akina Samatta kuvaa Medali za Dhahabu za Kombe la Shirikisho. Katika mchezo wa k...

Tazama Picha, Wasanii Kumi Wasio Vuta Wala Kutumia Kilevi Chochote.

Rapper na mfanya biashara mkubwa 50 Cent amefungua orodha ya wasanii wasio vuta wala kutumia kilevi chochote. Nakusanua kuwa anapenda kuonekana anafanya vitendo hivyo kwenye filamu na video zake ila kwenye maisha ya kweli hapendi kabisa pombe wala kuvuta sigara. Wasanni wengine wako hapa Hopsin Andre 3000 Tyler The Creator Lecrae K'Naan Rob Base Boots Riley Lauryn Hill Source-hiphopwired.com

HIZI NDIZO SABABU ZILIZOPELEA Msanii TID Kukamatwa Na Polisi Jana Usiku.

Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya, Khaleed Mohamed 'TID' yupo mahabusu katika Kituo cha Polisi Oysterbay tangu jana usiku baada ya kukamatwa na polisi kwa tuhuma za kumpiga na kumjeruhi msichana anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake,  Mariam Nnauye.  Huyu Ndio Mariam Nnauye. Taarifa zinasema kuwa ugomvi ulianza maisha club jana usiku baada ya TID kumkuta Mpenzi wake akiongea na mwanaume mwingine bila ruhusa ya Top In Dar na ndio Top akamvuta mpenzi wake na kumpiga makofi.Bila kijali mapenzi yao binti huyo alikwenda moja kwa moja kituo cha polici Osterbay na kutoa taarifa ya kupigwa naTid. Tid ametoka mida ya saa tano asubuhi kwa Dhamana na ataripoti tena polici jumatatu.

Huyu Ndio Mshindi Wa EBSS 2013

  Mshindi wa shindano la vipaji Epic Bongo Star Search Mwaka 2013 Ni Emmanuel Msuya. Amezawadiwa pesa za KiTanzania Milioni 50 Na Mkataba wa Kurekodi Chini Ya Studio Ya Mj Records.

Shabiki mkubwa wa soka, Rais Dkt. Jakaya Kikwete apokea kombe la Dunia!!

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akilifunua na kulinyanyua Kombe la Dunia katika uwanja wa michezo Kirumba mjini Mwanza leo jioni (picha na Freddy Maro) Rais Dkt. Jakaya Kikwete ni shabiki mkubwa mno wa michezo, na kila timu ya Taifa inapofanya kazi nzuri huwa anafarajika sana