Skip to main content

Posts

TUNAOMBA RADHI KWA HIZI PICHA: HAWA NDIO MAJAMBAZI WATATU WALIOUAWA NA KUCHOMWA HUKO MOROGORO

  WANANCHI wenye hasira wa Kijiji cha Kisiwa Kata ya Kiloka Wilaya ya Morogoro Vijini jana usiku wamewauwa kisha kuwachoma moto watu watu  wanaosadikiwa kuwa majambazi.   Akizungumza na Mtandao huu shuhuda wa tukio hilo Bw Shabani Mango alisema majambazi hao walivunja nyumba ya mkazi mmoja wa kijijini hicho na kuiba shilingi  490,000.   "Jamaa walifka hapa majira ya saa 8 usiku wakiwa na pikipiki Feko yenye namba za usajiri T310 BTC wakipakizana mshikaki,walivunga geni na kuingia ndani ambapo walipora kiasi hicho cha fedha "alisema Mango na kuongeza" Fedha hizo Mwalimu Said Swale Tajiri alizikopa jana mchana kwenye saccos ya Moboto kwa lengo la kumlipia ada mdogo wake anayesoma jijini Dar es salaam leo ijumaa alipanga kwenda Dar kulipa ada nahisi jamaa walipata taarifa kwamba Ticha ana mzigo ndani"alisema Bw Mango.   Akihojiwa na mtndao huu afisa mmoja wa jeshi la polisi alithibitissha kutokea kwa tukio hilo na kuwa...

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo amaliza ziara yake katika Mkoa wa Pwani.

Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Bi.Mwanamvua Mrindoko akimweleza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel(mwenyeshati Jeusi) Mpango wa kuendelea kuwawezesha vijana katika halmashauri yake kwa Kutekeleza mipango mbalimbali iliyowekwa ikiwamo kutoa mafunzo kwa vijana na kuongeza bajeti hadi kufikia shilingi milioni 40 kutoka milioni 10 iliyokuwa inatolewa hapo awali kwa mwaka wa fedha 2014-2015,wakati wa Ziara ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo kuangalia shuguhuli mbalimbali za vijana zinazoratibiwa na Wilaya hiyo. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel(mwenyeshati Jeusi) akiongea na vijana wa kikundi cha bodaboda wakati wakati wa Ziara ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo kuangalia shuguhli mbalimbali za vijana leo katika wilaya ya Kisarawe. Naibu Katibu Mkuu Wiz...

Huyu hapa MTOTO WA AJABU

Na Hamida Hassan na Imelda Mtema AMA kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya Farao, Andrea Marcus (13), mkazi wa Mbezi-Kibanda cha Mkaa, Dar anadaiwa kuwa wa ajabu kutokana na vitendo vyake. Mtoto huyu amedaiwa kuwa ni wa kichawi kutokana na maajabu yafuatayo: Mkazi wa Mbezi-Kibanda, Andrea Marcus. Ana uwezo wa kula ubwabwa sufuria moja la familia, anamudu kunywa maji ndoo moja, ana uwezo wa kuingiza tumboni mikate mikubwa saba kwa mlo mmoja,  amewahi kula mchele (si ubwabwa) ndoo nzima. Mbaya zaidi baada ya kula milo hiyo huwa haoneshi ameshiba. Maajabu mengine ambayo yanawashangaza watu wanaoishi naye ni jinsi anavyokula chakula kwa kumwaga chini kisha kukomba mpaka udongo. “Sina amani ya moyo, naomba Watanzania wanisaidie, mwanangu ananiuma sana, hata kujisaidia ni hapohapo, chakula anakula kupita kiasi, kama nilivyosema hashibi na bado hali kama mwanadamu wa kawaida,” alisema mama wa mtoto huyo. Akizungumzia madai ya uchawi, mama huyo, Angelina Marcus alis...

Hawa hapa wapiganaji 30 wa Al Shabaab waliouawa

Wanamgambo wa Al Shabaab Msemaji wa jeshi hilo Meja Emmanuel Chirchir ameelezea kuwa jeshi la Kenya lilishambulia kwa mabomu mojawapo ya kambi za kundi hilo katika eneo la Gedo , Alhamisi Jioni. Aliongeza kwamba miongoni mwa waliofariki ni makamanda kadhaa wa kundi hilo. Al Shabaab hata hivyo hawajatoa tamko lolote kuhusu shambulizi hilo. Kadhalika Al Shabaab walikiri kufanya shambulizi la kigaidi mjini Nairobi mwaka jana dhidi ya jengo la kifahari la Westgate na kuwaua watu 70. Kenya imekuwa ikipambana na wapiganaji wa kundi hilo tangu mwaka 2011 Oktoba wanajeshi wake walipojiunga rasmi na vikosi vya muungano wa Afrika ambavyo tayari vilikuwa nchini Somalia kwa kazi hiyo. Rais Uhuru Kenyatta ameahidi kuwa majeshi ya Kenya yataendelea va vita dhidi ya wanamgambao hao tangu waliposhambulia Kenya mwaka jana.

HIZI NDIZO SABABU ZILIZOMFANYA JOYCE KIRIA AIKACHIFU ELIMU YA PHD!

  Nikienda shule ntachizika!!!! Acha nibaki na hizi zinazonisaidia kukataa Usaliti ambao ni Ukatili mkubwa sana wa kijinsia... na wanaume ndiyo wanaoongoza kusaliti Ndoa zao tena Wasomi wa taifa hili (japo siyo wanaume wote.) Kama elimu hii ya std7 inanisaidia kuupiga vita Usalitikwa nguvu na akili zangu zote..huku wasomi wenye nondo zao wakipinga vikali na kutaka kunitoa roho kwa sababu tu ya kuvunja kwangu ukimya, Ni bora std7 yangu walahi.... Phd ya kukumbatia Maovu SIITAJ I. Phd ya kutetea Uzinzi/Umalaya/Wizi! SIITAKI Phd ya kutomsifia Mume wangu baba watoto wangu bila Eti kwa sababu anaweza kuja kugeuka! SIITAKI... 2014 siitaji umaarufu Mavi, wa kufa na tai shingoni. Najua ni ngumu sana msimamo wangu kuwaingia watu, lakini ntakomaa mpaka mwisho. Wanawake wengi sana tunaumia kwa sababu za Usaliti unaoitwa ni "Utamaduni wa Kiafrika Wanaume kusaliti Ndoa zao!!" Itatuitaji wanawake kubadili hii mitazamo kandamizi kwa kuchukua hatua ya kuach...

MATOKEO YA SENSA YA IDADI YA TEMBO KATIKA MFUMO WA IKOLOJIA WA SELOUS-MIKUMI NA RUAHA-RUNGWA

Wizara ya Maliasili na Utalii inapenda kuujulisha umma matokeo ya sensa ya tembo iliyofanyika mwezi Oktoba na Novemba mwaka huu ili kuiwezesha Serikali kutambua hali ya rasilimali ya wanyamapori ndani na nje ya maeneo yaliyohifadhiwa. Wizara kwa kushirikiana na wataalamu wa ndani na nje ya nchi imefanya sensa katika Maeneo ya Mfumo ikolojia wa Selous – Mikumi na Ruaha – Rungwa pekee kwa kuwa ni maeneo yenye tembo wengi nchini.  Matokeo ya sensa hii yanaonyesha kwamba Mfumo wa ikolojia wa Selous-Mikumi kwa sasa una tembo wapatao 13,084 na Ruaha–Rungwa una tembo wapatao 20,090. Takwimu hizi zinaonesha kupungua kwa idadi ya tembo na hasa katika mfumo ikolojia wa Selous-Mikumi ikilinganishwa na Sensa za awali. Takwimu za muda mrefu zinaonesha kwamba mwaka 1976 katika mfumo ikolojia wa Selous–Mikumi kulikuwa na tembo 109,419. Idadi hii ilipungua kufikia 22,208 mwaka 1991 kutokana na wimbi la ujangili uliokuwepo katika kipindi cha mwaka 1984 -1989. Hata hivyo, idadi ...

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA SHULE YA SEKONDARI YA KIEMBE SAMAKI ZANZIBAR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza jambo na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kiembe Samaki, Amina Salum Khalfan, wakati alipokuwa akitembelea chumba cha Maabara baada ya kuzindua rasmi Shule hiyo wakati wa hafla fupi iliyofanyika shuleni hapo mjini Zanzibar leo Jan 10, 2014. Picha na OMR Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na mmoja wa wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Kiembe Samaki, baada ya uzinduzi rasmi wa shule hiyo uliofanyika leo Jan 10, 2014, mjini Zanzibar. Picha na OMR Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kiembe Samaki, Amina Salum Khalfan, wakati alipotembelea katika chumba cha Mawasiliano na mafunzo ya Kompyuta cha shule hiyo, baada ya uzinduzi rasmi wa shule hiyo uliofanyika leo Jan 10, 2014, mjini Zanzibar. Picha na OMR Makam...