Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye Kituo chake cha kupigia Kura, kwa ajili ya kushiriki kupiga kura ya kumchagua Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki katika uchaguzi mdogo, uliofanyika leo mjini Zanzibar leo asubuhi. Kushoto ni Mgombea wa Jimbo hilo, Mahmoud Thabit Kombo. Uchaguzi huo umefanyika baada ya aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo hilo, Mansour Yusuph Himid, kuvuliwa uanachama mwishoni mwa mwaka uliopita . Picha na OMR Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimchagua kwa siri mgombea wa Jimbo la Kiembesamaki, katika uchaguzi mdogo wa Mwakilishi wa Jimbo hilo, uliofanyika leo mjini Zanzibar. Uchaguzi huo umefanyika baada ya aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo hilo, Mansour Yusuph Himid, kuvuliwa uanachama mwishoni mwa mwaka uliopita. Picha na OMR Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitumbukiza kura yake ya kumchagua Mwakilishi wa Jimbo la ...