Skip to main content

MAJIBU YA RIPOTI YA KIFO CHA NGWEA BADO NI KITENDAWILI

TAKRIBANI miezi miwili tangu alipofariki dunia mfalme wa freestyle wa Hiphop Bongo, Albert Kenneth Mangweha ‘Ngwea’ bado familia inalalama kuwa haijapokea ripoti ya kifo cha kijana wao.
Mama mzazi wa Ngwea, Denisia Mangweha (kulia) akiwa na aliyekuwa mchumba wa mwanaye aitwaye Misheily.
Habari za kiuchunguzi kutoka ndani ya familia zimeeleza kuwa ukiachilia mbali cheti cha kifo cha Ngwea walichopewa siku kadhaa baada ya mazishi ya mtoto wao, hawajawahi kuelezwa kwa kina juu ya kile kilichomsababishia mauti au hata mwenendo wa kesi au uchunguzi wa tukio hilo.
Ilidaiwa kuwa mara kadhaa familia hiyo ilikutana katika vikao vya ndani na kukubaliana kulifuatilia suala hilo katika Ubalozi wa Afrika Kusini jijini Dar. Huko walikumbana na vizingiti kwa maelezo imekataliwa kutolewa nchini humo.
Ilisemekana kuwa ndugu hao walipokwenda mara ya mwisho ubalozini hapo waliambiwa waandike barua ya kuomba kujua kinachoendelea ikiwa ni pamoja na ishu ya kama kuna kesi katika tukio hilo.
Albert Kenneth Mangweha ‘Ngwea’.
Habari nyingine zilidai kuwa huenda ripoti hiyo ilikwama sehemu au uchunguzi haujakamilika.
Baada ya kujishibisha na data hizo, gazeti hili lilisaga lami hadi Mazimbu Road, Kihonda mjini hapa nyumbani kwa mama Ngwea, Denisia Mangweha ili kupata undani wa habari hiyo.
Juu ya suala hilo mama Ngwea alisema: “Ukweli kama familia hatujakabidhiwa ripoti wala hatujui kinachoendelea.
“Mwezi uliopita tulikaa kikao kwa baba mdogo wa Albert (Ngwea), David Mangweha nyumbani kwake Mbezi jijini Dar ambapo tuliamua kufuatilia mambo hayo.
“Pia ni kweli tulimtuma kaka yake lakini walituambia kama familia tuandike barua ya kuomba ripoti na masuala mengine na tutume mtu kutoka ndani ya familia aende Afrika Kusini kwani hata wao hawajaipata, jambo ambalo ndiyo tunaendela nalo.
Wakati hayo yakiendelea, wiki iliyopita mchumba wa Ngwea alifika nyumbani hapo akitokea Dar ambapo alisababisha vilio upya huku akieleza jinsi ambavyo amekuwa akilia kila kukicha na kushindwa kuishi bila Ngwea.
Hadi gazeti hili linaanua virago nyumbani hapo mchumba huyo wa Ngwea alikuwa akiendelea kumfariji mama mkwe wake kwa maelezo kuwa anahisi kuendelea kuishi Dar bila msanii huyo kutamshinda.
Ngwea alifariki dunia ghafla Juni 28, mwaka huu huko Afrika Kusini ambapo hali leo wengi wamekuwa wakitaka kujua ukweli juu ya chanzo cha kifo chake.

Comments

Popular posts from this blog

Tazama picha za utupu ya Mwimbaji wa nyimbo za injili

Hili nalo ni tukio la kushitua baada ya msanii wa nyimbo za injiri kuamua kuanika picha zake za utupu kunako mitandao ya kijamii tukio hili limetokea hivi karibuni Nchini Nigeria Baada ya mwimbaji wa nyimbo za injiri kuweka piha na video kwenye mtandao anajulikana kwa jina la Maheeda  I doubt if this Naija female singer called Maheeda could still be described as a gospel singer giving her acts in recent times, especially in the social media. Her latest show of shame is posting videos of herself in the n*de while taking her bath. Check out more of her craze below:

HAYA NDIYO MAPENZI MAPYAAAAAAA..YA .!! RAY C KAFA KAOZA

Ray C  Msanii "kiuno bila mfupa" Rehema Chalamila. 'Ray C' anadaiwa kuwa bize na harakati za kumnasa sukari ya warembo Naseeb Abdul 'Diamond' katika anga za maoenzi huku duru za habari zikidai kuwa muda si mrefu kuanzia saaa yataandikwa mengi juu ya wawili hao Mwandishi wetu alizungumza na rafiki wa karibu na Ray C hivi karibuni na kuambiwa kuwa muda mwingi jina la Diamond halikatiki mdomoni mwa mrembo huyo   Diamond Platnumz Chanzo chetu cha habari kilizidi kudai kuwa kwa sasa Ray C hana furaha hadi atakapotimiza nia na lengo la kumnasa Diamond hapo ndipo furaha yake itakapotimu Aidha habari zinazidi kudai kuwa mara kadhaa Ray C amekuwa akipanga Miadi ya kukutana na Diamond licha yakushindikana kwa apointiment hizo kila mara "kwasasa Ray C haambiwi kitu kwa Diamond, ana haha kila wakati kumweka mikononi mwake, hana furaha kabisa hadi lengo lake litakapotimia, na muda si mrefu mtaandika juu ya hao" alisema rafiki ea K...

VIDEO YA NGONO YA WANAOSADIKIKA KUWA NI WANAFUNZI WA IFM YAVUJA

Watu wawili wanaosadikika ni wanachuo wa IFM wajirecord video wakifanya ngono ndani ya........... chumba ambacho kinaonesha kama ni cha hosteli, fungua na uone upuuzi uliofanyika humu ndani…. KUANGALIA VIDEO HII LAZIMA UWE NA UMRI WA ZAIDI YA MIAKA 18+ KUANGALI BOFYA HAPA