Skip to main content
TIZAMA PICHA NA MATUKIO MBALIMBALI YA WAZIRI MKUU MHE. MIZENGO PINDA AKIWA ZIARANI KARATU
Mke
wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akizungumza katika Mkutano uliohutubiwa
na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika uzinduzi wa Maktaba ya Shule ya
Sekondari ya Banjika wilayani Karatu Septemba 20, 2013. Katikati ni
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Mendeleo ya makzi, Profesa Anna Tibaijuka.
(Picha naOfisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo yaMkazi,
Profesa Anna Tibaijuka wakitembelea maktaba yaShule ya Sekondari ya
Banjika ya wilayani Karatu ambayo ilizinduliwa na Waziri Mkuu, Mizengo
Pinda, Septemba 20, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akiweka jiwe la Msingi la Tangi la Maji katika
Kijiji cha Gykrum Arusha wilayni Karatu Septemba 20, 2013. Wapili
kushoto ni mkewe Tunu na kushoto ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda na Mkewe Tunu (kushoto) wakipata maelezo Kutoka
kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka wa Arusha, Bibi
Ruth kuhusu ujunzi wa tangi la Maji katika kijiji cha Gykrum Arusha
wilayani Karatu baada ya kuweka jiwe la Msingi la mradi huo Septemba20,
2013. Kushoto kwa Waziri Mkuu, ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi, Profesa, Anna Tibaijuka. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akitazama uchimbaji wa kisima kirefu cha maji
unaofanywa na wakala serikali wa Uchimbaji visima katika eneo la
Bwawani wilayani Karatu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akiwasalimia wananchi wa Mbulumbulu baada ya
kuzindua Kituo cha Afya cha Kambi ya Simba wilayani Karatu Septemba 20,
2013. Kulia ni mkewe Tunu na kulia kwake ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka(Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Comments
Post a Comment