0712461976 au 0764302956
LIGI
kuu soka Tanzania bara imeendelea leo kwa mitanange miwili ya vuta
nikuvute iliyopigwa katika miji miwili tofauti hapa nchini.
Mabingwa
watetezi wa ligi hiyo, Young African walialikwa na maafande wa JWTZ,
Rhino Rangers kwenye uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Mbeya
City walikuwa wageni wa JKT Ruvu wanaonolewa na kocha Fredy Ferlix
Minziro, katika uwanja wa Azam Complex, uliopo Chamazi, nje kidogo ya
jiji la Dar es salaam.
Yanga waliuanza mchezo wa leo kwa lengo moja la kuibuka na ushindi ili kuwasogelea Azam fc kileleni.
Haikuwa
rahisi kwao kuwafunga Rhino kwa dakika 28 za kwanza, lakini dakika ya
29, mshambuliaji aliyekalia benchi kwa muda mrefu, Jeryson Tegete
aliandika bao la kuongoza.
Baada
ya bao hilo, Yanga waliendelea kulisakama lango la Rhino ambapo mara
kadhaa Tegete alijaribu kuzitafuta nyavu za wapinzani wao, lakini mabeki
wa Rhino walikuwa makini.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, Yanga walitoka kifua mbele kwa bao 1-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kuendelea kulishambulia lango la Rhino.
Dakika
ya 68, Yanga walipata bao la pili baada ya mlinzi wa Rhino kujifunga
wakati akijaribu kuokoa mpira wa winga machachari, Saimon Msuva.
Dakika ya 75, kocha Pluijm alimtoa Tegete na kumuingiza mshambuliaji Hussein Javu.
Comments
Post a Comment