Skip to main content

RUVU SHOOTING YAWAJIA JUU WACHEZAJI WANAOIPONDA, WASEMA DHAMIRA NI UBINGWA

RUVU Shooting StarsNa Baraka Mpenja wa fullshangwe, Dar es salaam
MAAFANDE  wa Ruvu Shooting wamedhamiria kufanya maajabu katika msimu wa 2014/2015 wa ligi kuu soka Tanzania bara unaotarajia kuanza kutimua vumbi mwezi agosti mwaka huu.
Masau Bwire, afisa habari wa klabu hiyo ameuambia mtandao huu kuwa wanaendelea vizuri na mazoezi waliyoanza jana chini ya kocha mkenya, Tom Alex Olaba katika uwanja wao wa Mabatini, Mlandizi, mkoani Pwani.
Masau amesema nia yao ni kujiimarisha mapema ili kuleta changamoto mpya na ili kufanikisha ndoto hiyo, ndio maana Shooting imekuwa timu ya kwanza kuingia kambini.
“Lengo letu ni kuchukua ubingwa au nafasi ya pili. Tukishindwa sana, sana tunahitaji nafasi ya tatu. Hatuongei kwa kujifurahisha, tunajipanga vilivyo”. Amesema Masau.

Comments