Skip to main content

CCM Yajipanga Kurudia Uchaguzi Zanzibar.......Yawataka Wanachama Wake Kujitokeza Kwa Wingi


KAMATI Maalumu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar chini ya Mwenyekiti wake Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein imewataka wananchi na wanachama kujiweka tayari na hatimaye.................
kujitokeza katika uchaguzi mkuu wa marudio.

Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu wa Itikadi na Uenezi Zanzibar, Waride Bakari Jabu, wananchi wametakiwa kujiandaa kwa uchaguzi wa marudio na kuachana na propaganda zinazotolewa na watu wachache kwa lengo la kupotosha ukweli.

“Kikao cha Kamati Maalumu ya CCM Zanzibar kilichokutana hapa chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar, Dk Shein kimewataka wananchi, wanachama na wafuasi wa CCM kujitayarisha kwa uchaguzi mkuu wa marudio ambao tarehe ya kufanyika kwake itatangazwa na taasisi husika,” imesema taarifa hiyo ya Waride.

Matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa Oktoba 25 ulifutwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salum Jecha kwa kile alichoeleza ni kuwepo kwa ukiukwaji wa kanuni na sheria za uchaguzi huru wa kidemokrasia.

Katika kikao cha jana kilichohudhuria pia na viongozi kadhaa wa kitaifa akiwemo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kilijadili ajenda mbili ikiwemo hali ya kisiasa mara baada ya uchaguzi mkuu kwa upande wa CCM.

Katika taarifa hiyo, chama hicho kimesema kimeridhishwa na mwenendo wa hali ya kisiasa na kimewapongeza wanachama waliojitokeza kwa wingi kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25.

Aidha chama kimepongeza na kutoa baraka kwa mazungumzo yanayoendelea ya viongozi wakuu wa kisiasa yakiwa na lengo la kuleta amani ya kudumu. Kamati ya mazungumzo ya hali ya kisiasa Zanzibar yenye lengo la kusaka amani ya kudumu iliyovurugika kutokana na kufutwa kwa uchaguzi mkuu inaundwa na viongozi wastaafu wakiwemo marais, Dk Salmin Amour, Amani Abeid Karume, Balozi Seif Ali Iddi ambaye ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Seif Sharif Hamad na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein.

Akizungumza juzi Ikulu, jijini Dar es Salaam, Rais wa Zanzibar, Dk Shein alisema mazungumzo hayo yanaendelea vizuri na taarifa kamili yatakapofikia tamati. Alipoulizwa kuhusu hatma ya CCM kama uchaguzi mkuu utarudiwa, Waride alisema chama bado kiko imara na hakijatetereka.

“Wapo wanaosema CCM imeyumba, si kweli wala CCM haijapoteza majimbo kwa sababu kura hazikumalizwa kuhesabiwa,” alisema.

Comments

Popular posts from this blog

VIDEO YA NGONO YA WANAOSADIKIKA KUWA NI WANAFUNZI WA IFM YAVUJA

Watu wawili wanaosadikika ni wanachuo wa IFM wajirecord video wakifanya ngono ndani ya........... chumba ambacho kinaonesha kama ni cha hosteli, fungua na uone upuuzi uliofanyika humu ndani…. KUANGALIA VIDEO HII LAZIMA UWE NA UMRI WA ZAIDI YA MIAKA 18+ KUANGALI BOFYA HAPA

Tazama picha za utupu ya Mwimbaji wa nyimbo za injili

Hili nalo ni tukio la kushitua baada ya msanii wa nyimbo za injiri kuamua kuanika picha zake za utupu kunako mitandao ya kijamii tukio hili limetokea hivi karibuni Nchini Nigeria Baada ya mwimbaji wa nyimbo za injiri kuweka piha na video kwenye mtandao anajulikana kwa jina la Maheeda  I doubt if this Naija female singer called Maheeda could still be described as a gospel singer giving her acts in recent times, especially in the social media. Her latest show of shame is posting videos of herself in the n*de while taking her bath. Check out more of her craze below:

Tazama Pichaz 14 za Kilimanjaro Stars ilivyowasili uwanja wa ndege wa JKIA Dar baada ya kutolewa Challenge

Timu ya taifa ya  Tanzania  bara  Kilimanjaro Stars  imewasili  Dar Es Salaam  December 2 ikiwa ni siku mbili zimepita toka itolewe na timu ya taifa ya  Ethiopia  katika michuano ya mataifa ya  Afrika Mashariki  na kati maarufu kama  CECAFA Senior Challenge Cup 2015 .  Kilimanjaro Stars  itolewa na  Ethiopia  katika hatua ya robo fainali kwa mikwaju ya penati 4-3 baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya goli 1-1. Naomba nikusogeze pichaz 15 za timu ya taifa ya  Tanzania  Bara  Kilimanjaro Stars  ikiwasili uwanja wa ndege Dar Es Salaam. Himid Mao baada ya kuwasili Nahodha wa Kilimanjaro Stars John Bocco baada ya kutua Dar akielekea katika basi. John Bocco na kocha mkuu na msaidizi wake wakizungumza jambo Shomari Kapombe ndani ya basi la timu ya Taifa Hassan Kessy akipanda basi la Stars Mshauri wa Kilimanjaro Stars na kocha wa Taifa Stars Charles Boniface Mkwasa aki...