Skip to main content

Marekani Yamuweka Rais Magufuli Njiapanda......MCC inakutana Kesho Huku Suala La Zanzibar Likiwa Bado Ni Kitendawili


Marekani imeiweka njiapanda Serikali ya Rais Dk. John Magufuli, baada ya Bodi ya shirika lake la Changamoto za Milenia (MCC) kuamua kukutana kesho kujadili masuala kadhaa ya utoaji wa misaada kwa nchi zinazoendelea huku angalizo lake kwa serikali ya Tanzania kuhusiana na uchaguzi wa Zanzibar likiwa bado halijapatiwa ufumbuzi.

Kwa mujibu wa ratiba ya MCC, kikao chao cha Bodi kitakutana kesho (Jumatano) na kupitia mapendekezo ya kupeleka misaada kwa nchi mbalimbali zinazoendelea.
 
Inaelezwa kuwa kikao hicho kitafanyika kwenye ukumbi wa Holbrooke, saa 4:00 asubuhi kwa saa za Marekani.

Inatarajiwa kuwa kupitia kikao hicho, nchi zitakazokidhi vigezo zitakuwa na fursa ya kuidhinishiwa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo iliyojipangia yenyewe kabla ya kupata fedha hizo. 
 
Tanzania inasubiri kuidhinishiwa fedha za awamu ya pili za MCC Dola za Marekani milioni 472 (takribani trilioni moja). 

Hata hivyo, kutokana na ratiba hiyo, Serikali ya Rais Magufuli inatarajiwa kuwa njiapanda kwani suala la Zanzibar lililokumbushiwa na MCC kupitia maelekezo yake yaliyoripotiwa mwezi uliopita, bado linaonekana kuwa kuendelea kuwa tete. 
 
Hadi sasa, licha ya vikao mbalimbali vinavyoendelea kufanyika na kuwakutanisha wagombea waliokuwa wakichuana kwa karibu kabla ya uchaguzi huo kufutwa, Dk. Ali Mohamed Shein wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Maalim Seif Shariff Hamad wa Chama cha Wananchi (CUF), bado ufumbuzi haujapatikana. 

CCM wanaamini kuwa uchaguzi huo ni lazima urudiwe baada ya kufutwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha, huku CUF wakisisitiza kuwa uchaguzi huo haukuwa na kasoro kubwa kiasi cha kufutwa wote na hivyo kutaka matokeo yatolewe na mshindi atangazwe kuwa Rais wa visiwa hivyo.

Awali, katika angalizo lake kwa serikali ya Magufuli iliyoingia madarakani Novemba 5, 2015, MCC ilitaka kupatiwa ufumbuzi kwa suala la Zanzibar na pia kuwapo kwa ufafanuzi juu ya watuhumiwa waliokamatwa kwa makosa ya mtandao wakati wa Uchaguzi Mkuu, Oktoba 25.

Ilifahamika kuwa maelekezo ya MCC kwenda kwa mamlaka mbalimbali za serikali ya Tanzania, yalionyesha kuwa lipo tishio la kufutwa kwa msaada huo (trilioni moja) iwapo mgogoro wa kisiasa wa Zanzibar hautapatiwa ufumbuzi na pia kutolewa ufafanuzi wa sheria ya makosa ya mtandaoni kabla ya kikao cha bodi ya MCC mwezi huu (Desemba, 2015).

 “MCC inafuatilia kwa karibu hatua zitakazochukuliwa na serikali ya Magufuli katika suala la utawala bora, katika kipindi hiki tunapokaribia kufanya kikao cha bodi ya MCC Desemba. Utatuzi wa mgogoro wa Zanzibar kwa kuridhisha pande zote zinazohusika,” ilielezwa katika kile kilichodaiwa kuwa ni sehemu ya angalizo la MCC kwa serikali ya Tanzania na kuripotiwa Novemba, 2015.

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, aliwahi kulitolea ufafanuzi suala hilo  Novemba 29, 2015, akisema kuwa Serikali haina wasiwasi kuhusu mashariti ya MCC juu ya Zanzibar kwani yatafanyiwa kazi kabla ya bodi ya MCC kukutana tena (Desemba).

Hata hivyo, hadi sasa hakuna muafaka uliotangazwa rasmi kuwa umefikiwa kuhusiana na uchaguzi wa Zanzibar huku pande zote zikiendelea kutoa msimamo tofauti; hali hiyo ikielezwa kuwa inaiweka njia panda serikali ya Magufuli kwani fedha za MCC ni muhimu katika utekelezaji wa ahadi zake mbalimbali, hasa juu ya dhamira ya kusambaza umeme na kuwaunganisha wananchi wengi katika gridi ya taifa.

Kadhalika, fedha za awamu ya pili za MCC ni muhimu pia katika uimarishaji wa taasisi zinazohusika na sekta ya nishati.

Akizungumzia hatari iliyopo sasa ya kukosa fedha za MCC baada ya suala la uchaguzi wa Zanzibar kutopatiwa ufumbuzi, Balozi Sefue alisema hakuna hofu yoyote (ya kukosa fedha) kwa sababu tayari kuna hatua kadhaa zimechukuliwa na Serikali ya Tanzania kushughulikia mambo yaliyohojiwa na MCC.

Akieleza zaidi, Balozi Sefue alisema taarifa ya MCC haikusema masuala hayo mawili yaishe vipi, bali walieleza yashughulikiwe; na kwamba hivi sasa yanaendelea kushughulikiwa na yanaendelea vizuri.

Alisisitiza kuwa Tanzania imefuata mashariti yote ya kupata fedha hizo kutoka MCC.

“MCC walituambia sisi kama serikali kuwa yaangalieni masuala haya, na siyo kwamba walituambia tuyashughulikie hadi tuyamalize ndipo watatupatia fedha … hilo siyo kweli,” alisema Balozi Sefue.

Aliongeza kuwa hadi sasa, hatua zilizofikiwa katika kutatua mgogoro wa Zanzibar na pia suala la wahalifu wa makosa ya mtandao, yote hayawezi kuikosesha sifa Tanzania kupata fedha hizo.

Comments

Popular posts from this blog

Tazama picha za utupu ya Mwimbaji wa nyimbo za injili

Hili nalo ni tukio la kushitua baada ya msanii wa nyimbo za injiri kuamua kuanika picha zake za utupu kunako mitandao ya kijamii tukio hili limetokea hivi karibuni Nchini Nigeria Baada ya mwimbaji wa nyimbo za injiri kuweka piha na video kwenye mtandao anajulikana kwa jina la Maheeda  I doubt if this Naija female singer called Maheeda could still be described as a gospel singer giving her acts in recent times, especially in the social media. Her latest show of shame is posting videos of herself in the n*de while taking her bath. Check out more of her craze below:

VIDEO YA NGONO YA WANAOSADIKIKA KUWA NI WANAFUNZI WA IFM YAVUJA

Watu wawili wanaosadikika ni wanachuo wa IFM wajirecord video wakifanya ngono ndani ya........... chumba ambacho kinaonesha kama ni cha hosteli, fungua na uone upuuzi uliofanyika humu ndani…. KUANGALIA VIDEO HII LAZIMA UWE NA UMRI WA ZAIDI YA MIAKA 18+ KUANGALI BOFYA HAPA

Tazama Pichaz 14 za Kilimanjaro Stars ilivyowasili uwanja wa ndege wa JKIA Dar baada ya kutolewa Challenge

Timu ya taifa ya  Tanzania  bara  Kilimanjaro Stars  imewasili  Dar Es Salaam  December 2 ikiwa ni siku mbili zimepita toka itolewe na timu ya taifa ya  Ethiopia  katika michuano ya mataifa ya  Afrika Mashariki  na kati maarufu kama  CECAFA Senior Challenge Cup 2015 .  Kilimanjaro Stars  itolewa na  Ethiopia  katika hatua ya robo fainali kwa mikwaju ya penati 4-3 baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya goli 1-1. Naomba nikusogeze pichaz 15 za timu ya taifa ya  Tanzania  Bara  Kilimanjaro Stars  ikiwasili uwanja wa ndege Dar Es Salaam. Himid Mao baada ya kuwasili Nahodha wa Kilimanjaro Stars John Bocco baada ya kutua Dar akielekea katika basi. John Bocco na kocha mkuu na msaidizi wake wakizungumza jambo Shomari Kapombe ndani ya basi la timu ya Taifa Hassan Kessy akipanda basi la Stars Mshauri wa Kilimanjaro Stars na kocha wa Taifa Stars Charles Boniface Mkwasa aki...