Jamii Media Limited inasikitika kutangaza kuondokewa na mmoja wa wafanyakazi wake, Mwandishi Mkuu wa FikraPevu.com, Dotto J. Mnzava aliyefariki leo, Disemba 14, 2015 kufuatia ajali iliyohusisha pikipiki na gari iliyotokea maeneo ya Victoria, Mwananyamala jijini Dar es Salaam.
Mnzava alikuwa mwandishi wa Habari akiiandikia mitandao ya JamiiForums.com na FikraPevu.com na alijiunga na Jamii Media mapema mwaka jana, 2014.
Mipango ya mazishi na kusafirisha mwili wa marehemu kuelekea kwao Same kwa ajili ya maziko inaendelea kufanyika na kwa sasa mwili umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala. Kuaga mwili kwa wakazi wa Dar kutafanyika Disemba 17, 2015 katika Kanisa la Waadventista Wasabato, Manzese (ulipo uwanja wa Tippi).
Tunatoa pole za dhati kwa ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Dotto J. Mnzava.
Mungu amjalie pumziko la amani!
Amina

Comments
Post a Comment