Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Montage Tanzania, Teddy Mapunda wa tatu kutoka (kulia) akimkabidhi mpira Mwanafunzi wa kidato cha kwanza wa Shule ya Sekondari ya wasichana ya WAMA - Nakayama iliyopo Rufiji, mkoani Pwani Rehema Mshama(kulia) ikiwa ni mchango wake katika kuwasaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi ili waweze kujiendeleza katika sekta ya michezo. Makabidhiano hayo yalifanyika leo kwenye ofisi ya Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), jijini Dares Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Montage Tanzania, Teddy Mapunda wa nne kutoka (kushoto ) akimkabidhi mpira Mwalimu wa Michezo wa Shule ya Sekondari ya WAMA- Nakayama iliyopo Rufiji, Mbwana R. Mbwana wa tatu kutoka (kulia) ikiwa ni mchango wake katika kuwasaidia watoto yatima na...