Skip to main content

Posts

BAADA YA MSHINDI WA BIG BROTHER KUTANGAZA KUWA HAMJUI BABA YAKE, MKENYA AJITOKEZA NA KUDAI NI BABA YAKE

Wiki iliyopita wakati mshindi wa $ 300,000 za Big Brother The Chase Dillish Mathews kutoka Namibia akifanyiwa mahojiano na mwandishi wa Namibia, alisema anahamu ya kukutana na baba yake mzazi ambaye hawajawahi kuonana. Dillish Mathews & Abdi Guyo Baada ya siku chache kupita hatimaye jana (September 2) mwanaume aitwaye Abdi Galgayo Guyo alijitokeza katika ofisi za Standard media Kenya na kudai kuwa yeye ndiye baba mzazi wa Dillish ambaye binti yake anahamu ya kumuona.   Guyo alirekodiwa na kituo hicho na kutoa maelezo ya jinsi alivyokutana na mama yake Dillish aitwaye Selma Pashukeni mpaka walivyompata Dillish na baadaye kupotezana.   Bwana Guyo ambaye ni askari mstaafu wa Kenya aliiambia Standard Media kuwa alikuwa ni miongoni mwa maaskari wa Kenya wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa mataifa ‘United Nations Transition Assistance Group ‘, kilichopelekwa nchini ...

SIRI YAFICHUKA: KISA CHA AUNT EZEKIEL KUPIGWA CHUPA NI PENZI LA JEFF LINALOGOMBANIWA NA WAREMBO

Siri  ya  Aunt Ezekiel  kupigwa  chupa  club  na  kujeruhiwa  mkono wake imefichuka.Habari  za  uhakika  zinadai  kwamba  Aunt  alipigwa  chumba  na  mrembo  wa  kike  katika  harakati  za  kugombea  penzi  la  mwanaume...  Mwanaume  aliyekuwa  akigombaniwa  ni  Jeff  ambaye  anadaiwa  kuwa  ni boyfriend  wa  Yvonne ( aliyempiga  aunt  chupa ).. Kutokana  na  aibu  hiyo, mastaa  kadhaa  wameongea  na  mpekuzi  kwa  nyakati  tofauti  na  kueleza  masikitiko  yao  dhidi  ya  aunt  Ezekiel  ambaye  ni  mke  wa  mtu...  Katika  maongezi  hayo, mastaa  hao  walidai  kwamba  mambo  anayofanya  aunt  hayaendani  na...

ZISOME SMS ZA MAPANZI AMBAZO ZITAMFURAHISHA MPENZI WAKO UKIMTUMIA

  1. Weupe wa penzi lako ni kama mwezi angani.Ucheshi na mahaba yako nifananishe na nini? Kupata mfano wako hatotokea amini. Elewa mimi  ni wako sikuachi asilani. 2 . Najiuliza kila leo hivi ni mimi tu kimeo katika dunia hii ya leo maana kila leo nayempata huishia kunipa ahadi kila leo, mpenzi kila siku waniaidi mara nitakupa leo mara kabla ya machweo, hivi ni lini utanipa jibu la uhakika nakunipa mapenzi ya uhakika nipate farijika? Nakupenda mpenzi.  3. Hakika mtoto umeumbika mithili ya malaika japo mbinguni sijafika lakini nauhakika kwa kila mwanaume aliyeumbika na kukamilika akikuona lazima udenda utamtoka, naomba japo yako dakika nipate kukueleza moyoni yaliyonifika kwani siwezi tena kuficha jinsi navyokupenda, nakupenda amini kwako nimefika! 

MAJIBU YA RIPOTI YA KIFO CHA NGWEA BADO NI KITENDAWILI

TAKRIBANI miezi miwili tangu alipofariki dunia mfalme wa freestyle wa Hiphop Bongo, Albert Kenneth Mangweha ‘Ngwea’ bado familia inalalama kuwa haijapokea ripoti ya kifo cha kijana wao. Mama mzazi wa Ngwea, Denisia Mangweha (kulia) akiwa na aliyekuwa mchumba wa mwanaye aitwaye Misheily. Habari za kiuchunguzi kutoka ndani ya familia zimeeleza kuwa ukiachilia mbali cheti cha kifo cha Ngwea walichopewa siku kadhaa baada ya mazishi ya mtoto wao, hawajawahi kuelezwa kwa kina juu ya kile kilichomsababishia mauti au hata mwenendo wa kesi au uchunguzi wa tukio hilo. Ilidaiwa kuwa mara kadhaa familia hiyo ilikutana katika vikao vya ndani na kukubaliana kulifuatilia suala hilo katika Ubalozi wa Afrika Kusini jijini Dar. Huko walikumbana na vizingiti kwa maelezo imekataliwa kutolewa nchini humo. Ilisemekana kuwa ndugu hao walipokwenda mara ya mwisho ubalozini hapo waliambiwa waandike barua ya kuomba kujua kinachoendelea ikiwa ni pamoja na ishu ya kama kuna kesi katika tukio hil...

VIDONGE VINAVYOSABABISHA WATOTO KUZALIWA WAMEUNGANA VYA JULIKANA

IDADI ya wajawazito nchini wanaojifungua mapacha walioungana au wenye ulemavu inazidi kupanda ambapo mwishoni mwa wiki iliyopita, Pili Hija (24), mkazi wa Jang’ombe, Zanzibar alijifungua watoto walioungana, kinachosikitisha zaidi mmoja alikuwa ni kiwiliwili. Pili alijifungua mapacha hao saa 1:00 asubuhi ya Agosti 18, 2013, nyumbani kwake na baadaye kupelekwa kwenye Hospitali ya Mnazi Mmoja, Zanzibar baada ya watoto kuonekana si wa kawaida. Kufuatia matukio kama hayo, Ijumaa Wikienda lilichimba kwa undani ili kubaini nini husababisha wanawake kubeba ujauzito wenye matokeo ya mapacha walioungana au mtoto mmoja kulemaa kiungo chochote cha mwili. Mtaalam mmoja aliyesomea mambo ya afya ya uzazi ambaye aliomba hifadhi ya jina, ndiye aliyefunua siri hii nzito ambayo wanawake wengi nchini hawaijui isipokuwa kwa kusoma habari hii leo. Mtaalam huyo alivitaja vidonge maarufu kwa matibabu ya tumbo la kuendesha viitwavyo Flagyl au Metronidazole kuwa ndivyo vinavyosababisha matat...

OPERESHENI YA KUWAVUA NGUO WANAWAKE WANAOVAA NUSU UCHI YAANZA RASMI

Mrembo aliyevuliwa nguo na vijana baada ya  kuvaa 'kichupi'. Habari hii inathibitishwa na tukio la mrembo ‘miss’ (jina lake halikupatikana) ambaye amejikuta katika wakati mgumu baada ya kukumbana na kasheshe zito kutoka kwa wanaume kufuatia kinguo kifupi alichokuwa amevaa, kilichoacha nje sehemu kubwa ya mapaja. Vijana wa mjini wakimvua kitenge alichojistiria mrembo huyo. JIJINI ARUSHA Tukio hilo lililovuta umati mkubwa ambalo lilishuhudiwa na shushushu wetu, lilijiri maeneo ya stendi ya mabasi madogo jijini Arusha, wiki iliyopita wakati mrembo huyo akiwa na marafiki zake watatu wakirandaranda kufanya ‘window shopping’. Mara baada ya kufika eneo hilo, miss huyo alijikuta akizungukwa na wapiga debe wa daladala na kuanza kumshushia maneno makali wakimwambia kuwa wamechoshwa kuona nyeti zao. Trafiki wakiwa na mrembo huyo baada ya kumwokoa kutoka mikononi mwa vijana. AVULIWA Huku sistaduu huyo akidhani ni kelele za kawaida, wapiga debe hao walimzingira na kua...

FAHAMU SIKU NZURI YA KUMWINGILIA MKEO KIMAPENZI

Hakuna siku maalumu iliyowekwa kwa mume na mke kufanya tendo la ndoa. Jambo la kueleweka ni kuwa ni lazima kwa wanandoa hao wajitayarishe kisaikolojia, kimwili kwa kujipamba, kuwa wasafi na mengineyo ambayo yatalifanya tendo hilo kufanikishwa na kuwaleta watu hao wawili karibu zaidi na kuongeza mapenzi kati yao . Haifai kabisa kwa mume kumtaka mkewe kwa tendo la ndoa kisha mke akatae. Mtume s.a.w.w. ametufundisha kuwa haifai kwa mke kufunga hata funga ya Sunnah ikiwa mume yupo mjini bila ya kupata idhini kutoka kwake. Na pia akasema ikiwa mume amemtaka mkewe basi na amtimizie hata ikiwa ameweka chungu motoni. Na ndio tendo hilo likawa ni ‘Ibadah na mume na mke hupata thawabu kwayo. Mtume s.a.w.w. amesema: “Na kujamiiana kwenu pia ni sadaka”. Wakasema: “Ewe Mtume wa Allah! mmoja wetu huyajia matamanio yake na akawa atapata thawabu?” Akasema: “Mwaonaje lau aliiweka (tupu yake) katika haramu, angekuwa na dhambi” (Muslim kutoka kwa Abu Dharr [r.a]).  ...