Skip to main content

Posts

TASWIRA ZA RAIS KIKWETE BAADA YA KUHUTUBIA BUNGE MAALUM LA KATIBA MJINI DODOM MACHI 21, 2014

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongozwa na Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mhe Samuel Sitta mara baada ya kulihutibia Bunge hilo Ijumaa  mjini Dodoma Machi 21, 2104 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa na Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mhe Samuel Sitta mara baada ya kulihutibia Bunge hilo Ijumaa  mjini Dodoma Machi 21, 2104 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipewa pongezi kwa hotuba nzuti na Makamu  Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Samia  Suluhu Hassan mara baada ya kulihutibia Bunge hilo Ijumaa  mjini Dodoma Machi 21, 2104  Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Zanzibar Dkt Mohamed Ali Shein,  Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mhe Samuel Sitta na Makamu  Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Suluhu Samia Hassan wakifurahia jambo mara baada ya Rais  kulihutibia Bunge hilo Ijumaa  mjini Dodoma Machi 21, 2104 Rais Kikwete katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba PICHA NA IKULU...

YANGA YAITUNGUA RHINO 3-0 TABORA, MBEYA CITY YAWAANGAMIZA JKT RUVU 2-0 CHAMAZI!!

Na Baraka Mpenjwa wa fullshangwe, Dar es salaam 0712461976 au 0764302956 LIGI kuu soka Tanzania bara imeendelea leo  kwa mitanange miwili ya vuta nikuvute iliyopigwa katika miji miwili tofauti hapa nchini. Mabingwa watetezi wa ligi hiyo, Young African walialikwa na maafande wa JWTZ, Rhino Rangers kwenye uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mjini Tabora. Mbeya City walikuwa wageni wa JKT Ruvu wanaonolewa na kocha Fredy Ferlix Minziro, katika uwanja wa Azam Complex, uliopo Chamazi, nje kidogo ya jiji la  Dar es salaam. Yanga waliuanza mchezo wa leo kwa lengo moja la kuibuka na ushindi ili kuwasogelea Azam fc kileleni. Haikuwa rahisi kwao kuwafunga Rhino kwa dakika 28 za kwanza, lakini dakika ya 29, mshambuliaji aliyekalia benchi kwa muda mrefu, Jeryson Tegete aliandika bao la kuongoza. Baada ya bao hilo, Yanga waliendelea kulisakama lango la Rhino ambapo mara kadhaa Tegete alijaribu kuz...

RIDHIWANI KIKWETE APIGA KAMPENI KATIKA KATA YA FUKAYOSE JIMBONI CHALINZE

Mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze Bw. Ridhiwani Kikwete akisalimiana na wananchi baada ya kuwasili katika ya Fukayose jimbo la Chalinze  wakati alipoendelea na mikutano ya kampeni kunania kiti cha ubunge jimbo laKani  hilo, Rid hiwani Kikwete amewaomba wananchi wa kata ya Fukayose kumuamini na kumpa kura za ndiyo siku ya jumapili Aprili 6 na yeye atawalipa maendeleo na watapata nafasi ya kupanga mipango ya maendelea kwa ajili ya mafanikio ya jimbo la Chalinze.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA F ULLSHANGWE-CHALINZE) Mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze Bw. Ridhiwani Kikwete akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Mkenge kata ya Fukayose jimbo la Chalinze leo   Mwenyekiti wa kata ya Fukayose Orinjulie Machanga akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Mkenge wakati wa mkutano wa kampeni za mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze Bw. Ridhiwani Kikwete Baadhi ya wanachama wa chama cha Mapinduzi wakiwa wameshikilia picha za mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM...

wajumbe wanawake wa Bunge Maalum waaswa kufanya kazi kwa ushirikiano

Na Tiganya Vincent-Dodoma Mwenyekiti wa Wabunge  Wanawake wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anna Abdallah  ametoa wito kwa  wajumbe wanawake wa Bunge Maalum la Katiba kufanya kazi kwa ushirikiano katika kuhakikisha kuwa wanaweka maslahi ya mwanamke mbele katika uandishi wa Katiba mpya na sio vinginevyo.   Mwenyekiti huyo ametoa kauli hiyo leo mjini Dodoma wakati anafungua semina ya siku moja  ya wajumbe wanawake wa Bunge Maalum la Katiba iliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake nchini (TAMWA)  kwa lengo la kuwaelimisha juu ya kuwepo  na haja ya kuwepo na vipengele vinavyotetea haki za wanawake na watoto katika masuala mbalimbali.   Alisema kuwa wajumbe hao wanawanawake wanapaswa kuweka kando tofauti zao za kivyama, kiitikadi na kiimani na kuhakikisha kuwa haki za msingi zinaweka katika Katiba mpya itakayotunga ili kujenga usawa wa kijinisia katika masuala mbalimbali hap...

BAADHI YA Wizara, Idara na Taasisi za Serikali ZAPEWA vifaa vya Teknolojia, Habari na Mawasiliano (TEHAMA)

Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akitoa maelezo mafupi juu ya Mpango wa Kuboresha na Kuimarisha Takwimu nchini wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya Teknolojia, Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa baadhi ya Wizara, Idara na Taasisi za Serikali iliyofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Fedha. Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum akimkabidhi laptop Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya Teknolojia, Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa baadhi ya Wizara, Idara na Taasisi za Serikali iliyofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Fedha. Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum akihutubia wageni waalikwa (hawapo pichani)  wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya Teknolojia, Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa baadhi ya Wizara, Idara na Taasisi za Serikali iliyofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Fedha. Mwakilishi wa Wadau wa Maendeleo...

WAZIRI MKUU MHE. PINDA AFUNGA WIKI YA MAJI MJINI DODOMA

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua mradi wa maji wa Mkonze katika Maanispaa  ya Dodoma katika kilele cha wiki ya maji Machi 22, 2014. Kushoto kwake ni Waziri wa Maji, Profesa  Jumanne Maghembe.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua mradi wa maji wa Mkonze katika Maanispaa  ya Dodoma katika kilele cha wiki ya maji Machi 22, 2014. Kulia ni Waziri wa Maji, Profesa  Jumanne Maghembe.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimtwika maji, Bibi Edna petro baada ya kuzindua mradiwa maji wa Mkonze katika Manispaa ya Dodoma ikiwa ni moa ya shughuli za kilele cha wiki ya maji  Machi 22, 2014.(picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) m Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akisalimiana na Wanachuo wa Chuo Kikuu cha Dodoma baada ya kuweka jiwe la msingi la  mradi wa tangi la maji  ikiwa ni moja ya Shughuli za kilele cha wiki  ya maji  Machi 22, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

TAMWA WATOA ELIMU KWA WABUNGE WANAWAKE WA BMK KUZINGATIA MASUALA YA USAWA WA KIJINSIA WAKATI WA UTUNZI WA KATIBA MPYA

Mwenyekiti  wa Wabunge wanawake Anna Abdallah (kulia) akifungua semina ya Wabunge wanawake wa Bunge Maalum la Katiba  leo mjini Dodoma uliokuwa ukijadiliana juu ya umuhimu wa kuwekwa kwa umri wa mtoto katika Katiba mpya  na umri unatakiwa kuolewa na kuoa na masuala ya uzazi salama.  Kushoto ni Naibu Waziri  wa Katiba na Sheria Mhe Angelah  Kairuki. Mjumbe wa Bunge la Katiba ambaye pia Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Dkt Pindi Chana akitoa maoni yake leo mjini Dodoma wakati wa semina ya Wabunge wanawake wa Bunge Maalum la Katiba uliondaliwa na Chama cha Waandishi  wanawake Tanzania (TAMWA) juu ya kuwaelimisha masuala mbalimbali ya kuzingatia wakati wa utungaji wa Katiba mpya ikiwemo uzazi salama na kutoa ufafanuzijuu ya umri wa mtoto. Mjumbe wa Bunge la Katiba ambaye pia  N aibu Waziri  wa Ofisi ya Makamu wa Rais,  Ummy Mwalimu akitoa maoni yake leo mjini Dodoma wakati wa Mk...