Skip to main content

Posts

amko la CHADEMA Kulaani Mbunge wao Saed Kubenea Kukamatwa Kwa Amri Ya Mkuu wa Wilaya

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Kama ambavyo imeripotiwa kwenye vyombo vya habari na njia zingine za upashanaji habari tangu jana kuwa Mbunge wa Jimbo la Ubungo kwa tiketi ya CHADEMA, Ndugu Saed Kubenea aliwekwa chini ya ulinzi na kuamriwa kwenda kituo cha polisi kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ambaye inadaiwa hakutaka mbunge huyo azungumze na wananchi ambao ni Wafanyakazi wa Kiwanda cha Tanzania Took Garment, waliokuwa wamemuita mbunge huyo kwa ajili ya kumweleza matatizo wanayokumbana nayo kazini hapo, ikiwa ni pamoja na ujira kidogo na mazingira magumu ya kazi. Aidha akitambua kuwa alichofanya matumizi mabaya ya dhamana ya uongozi, hivyo akakusudia kuficha umma usijue uovu huo, katika tukio hilo Makonda aliwaagiza polisi wakamate kamera za waandishi wa habari waliokuwa katika eneo hilo wakitimiza wajibu wao wa kikazi na kitaaluma kwa jamii. Katika hatua ya sasa, tunaomba kusema ifuatavyo; 1. Tukitambua kuwa mamlaka ya DC kuamuru watu kukamatwa yam...

Marekani Yamuweka Rais Magufuli Njiapanda......MCC inakutana Kesho Huku Suala La Zanzibar Likiwa Bado Ni Kitendawili

Marekani imeiweka njiapanda Serikali ya Rais Dk. John Magufuli, baada ya Bodi ya shirika lake la Changamoto za Milenia (MCC) kuamua kukutana kesho kujadili masuala kadhaa ya utoaji wa misaada kwa nchi zinazoendelea huku angalizo lake kwa serikali ya Tanzania kuhusiana na uchaguzi wa Zanzibar likiwa bado halijapatiwa ufumbuzi. Kwa mujibu wa ratiba ya MCC, kikao chao cha Bodi kitakutana kesho (Jumatano) na kupitia mapendekezo ya kupeleka misaada kwa nchi mbalimbali zinazoendelea.   Inaelezwa kuwa kikao hicho kitafanyika kwenye ukumbi wa Holbrooke, saa 4:00 asubuhi kwa saa za Marekani. Inatarajiwa kuwa kupitia kikao hicho, nchi zitakazokidhi vigezo zitakuwa na fursa ya kuidhinishiwa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo iliyojipangia yenyewe kabla ya kupata fedha hizo.    Tanzania inasubiri kuidhinishiwa fedha za awamu ya pili za MCC Dola za Marekani milioni 472 (takribani trilioni moja).  Hata hivyo, kutokana na ratib...

Wanne Wakataa Uwaziri wa Magufuli Wakihofia Kushindwa Kuendana na Kasi Yake

WABUNGE wanne wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wametajwa kukataa uteuzi wa nafasi ya uwaziri ili kujaza nafasi za wizara nne zilizokuwa wazi. Hatua hiyo imetokana na kile kilichoelezwa kuwa ni hofu ya wabunge hao kushindwa kwenda na kasi ya Rais Dk. John Magufuli, ambaye aliwaapisha mawaziri wapya Desemba 12, mwaka huu. Kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania, wabunge wamedai kuwa kasi ya Rais Magufuli inawatia hofu. “Kasi ya Rais Dk. John Magufuli ni nzito na kwangu ni ngumu na nilifikiri niko mimi peke yangu kumbe baada ya taarifa hizi nasikia na wenzangu wawili nao walikataa uteuzi. “Niliarifiwa juu ya uteuzi lakini baada ya kupima nikaona hapana siwezi kazi ya uwaziri, bora ni baki na ubunge wangu,” alisema mbunge huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe. Wizara 4 zilizokosa Mawaziri Wakati akitangaza Baraza la Mawaziri, Desemba 10, mwaka huu, Rais Magufuli alisema kuna baadhi ya wizara hazina mawaziri kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo unyeti wa wizara hizo na kwam...

Saed Kubenea Apandishwa Mahakama Ya Kisutu na Kusomewa Shitaka La Kutoa Lugha Chafu Dhidi Ya Makonda

Mbunge wa jimbo Ubungo kupitia Chadema, Saed Kubenea amepandishwa kizimbani kortini Kisutu, jijini Dar es Salaam leo na kusomewa shtaka la kutoa lugha chafu dhidi ya Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda. Hata hivyo, Kubenea amekana kufanya kitendo hicho na kesi yake kuahirishwa hadi Desema 29, mwaka huu huku uchunguzi ukiendelea

Mgombea wa CCM apinga Matokeo ya Godbless Lema......Alitupia Lawama Jeshi la Polisi Kwa Kuwatisha Wapiga Kura kwa Silaha za Kivita

Aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Arusha Mjini kwa tiketi ya CCM, Philemon Mollel amepinga matokeo ya uchaguzi huo yaliyompa ushindi wa kishindo, Godbless Lema wa Chadema. Akiongea na waandishi wa habari baada ya msimamizi wa uchaguzi huo kutangaza matokeo, Mollel alidai kuwa kulikuwa na udanganyifu mkubwa ambao unafanya matokeo hayo kutokuwa halali. Alisema kuwa wakati zoezi la kupiga kura likiendelea kuna gari lililokamatwa likiwa na kura bandia za kumpa ushindi Lema ingawa alidai gari hilo liliachiwa baadae. “Kulikuwa na Noah ya diwani wa Chadema ambayo ilipita katika baadhi ya vituo vya kupigia kura na kudai kupeleka vyakula. Lakini gari hiyo tumeambiwa ilikuwa na kura za bandia zilizofanikiwa kuingizwa kwenye masanduku,”alisema Mollel. Kadhalika, alieleza kuwa kulikuwa na mapungufu makubwa kwenye fomu za matokeo kwa kuwa baadhi ya fomu hazikuonesha idadi ya kura zilizopigwa. Mollel alilirushia lawama jeshi la polisi kwa madai kuwa liliwatisha akina mam...

Ukweli kuhusu kifo cha Dotto Mnzava, mwandishi na muhariri wa Jamii forums huu hapaa......!!!!

Jamii Media Limited inasikitika kutangaza kuondokewa na mmoja wa wafanyakazi wake, Mwandishi Mkuu wa FikraPevu.com,  Dotto J. Mnzava   aliyefariki leo, Disemba 14, 2015 kufuatia ajali iliyohusisha pikipiki na gari iliyotokea maeneo ya Victoria, Mwananyamala jijini Dar es Salaam. Mnzava alikuwa mwandishi wa Habari akiiandikia mitandao ya JamiiForums.com na FikraPevu.com na alijiunga na Jamii Media mapema mwaka jana, 2014. Mipango ya mazishi na kusafirisha mwili wa marehemu kuelekea kwao Same kwa ajili ya maziko inaendelea kufanyika na kwa sasa mwili umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala. Kuaga mwili kwa wakazi wa Dar kutafanyika Disemba 17, 2015 katika Kanisa la Waadventista Wasabato, Manzese (ulipo uwanja wa Tippi). Tunatoa pole za dhati kwa ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Dotto J. Mnzava. Mungu amjalie pumziko la amani!  Amina

TAZAMA BONGE LA VIDEO KUTOKA KWA Diamond Platnumz - Utanipenda