Skip to main content

Posts

Showing posts from March 1, 2015

TAZAMA PICHA ZA MAAFA YA KAHAMA NA IDADI KAMILI YA WATU WALIOFARIKI NA KUJERUHIWAA

Mkazi wa Kijiji cha Mwakata akizungumza na simu alipokuwa akitoa taarifa kwa jamaa zake baada ya nyumba yake kubomoka kutokana na mvua ya mawe iliyonyesha kijijini hapo wilayani Kahama. Na Shija Felician, Mwananchi KWA UFUPI Mvua hiyo ya aina yake ilisababisha nyumba 160 kuanguka na nyingine kuezuliwa paa kutokana na upepo mkali na watu wengine 900 wameripotiwa kukosa makazi. Kahama. Mvua kubwa ya mawe iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha juzi usiku imesababisha maafa katika kijiji cha Mwakata wilayani Kahama mkoani Shinyanga ambako zaidi ya watu 42 wameuawa, wakiwamo saba wa familia moja na wengine 91 kujeruhiwa vibaya. Mvua hiyo ya aina yake ilisababisha nyumba 160 kuanguka na nyingine kuezuliwa paa kutokana na upepo mkali na watu wengine 900 wameripotiwa kukosa makazi. Watu wengi walifariki kutokana na kuangukiwa na kuta za udongo za nyumba za wanakijiji hao na wengine kuuawa kutokana na kuangukiwa na mawe makubwa ya barafu wakati walipokuwa wakijaribu kutafuta h