Skip to main content

Posts

Showing posts from August 10, 2014

Waziri mkuu mpya ateuliwa CAR

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Catherine Samba-Panza, amemteua Muislamu kuwa waziri mkuu mpya. Mahamat Kamoun, ambaye alikuwa mshauri maalumu wa Michel Djotodia, kiongozi wa kundi la wapiganaji wa Seleka, ataongoza serikali ya mpito. Waandishi wa habari wanasema hatua hiyo ni jaribio la kuunda serikali ya pamoja baada ya ghasia za kidini za zaidi ya mwaka mmoja. Tangazo hilo lilitolewa kwenye redio ya taifa na msemaji wa rais ambaye mwenyewe ni Mkristo. Ghasia zilizuka baina ya Wakristo na Waislamu baada ya wapiganaji wa Seleka, wengi wao waliokuwa Waislamu, walipomtoa madarakani Rais Francois Bozize mwaka jana.

Mapigano yasitishwa tena Ukanda wa Gaza

Israel na Palestina wamekubaliana kusitisha mapigano tena Gaza kwa saa 72 - makubaliano yaanza kutekelezwa Jumapili saa 6 za usiku kwa saa za Afrika Mashariki Wapatanishi wa Misri wamesaidia kuwezesha makubaliano hayo kufikiwa na mapigano yakisita kweli, Jumatatu Israel itatuma waakilishi mjini Cairo kwa mazungumzo ya kutafuta suluhu ya muda mrefu katika mzozo huo. Mwandishi wa BBC mjini Jerusalem anasema Israel itaendelea kudai kuwa Gaza liwe eneo lisilokuwa na silaha - na Hamas itataka Israel iache kuizingira Gaza na iondoe vizuizi vya kuingia na kutoka. Watu zaidi ya 20 wameuwawa tangu usitishwaji wa mapigano wa mwisho kumalizika Ijumaa.