Skip to main content

Posts

Showing posts from September 8, 2013

Jokate ataja sababu nne zinazowafanya wanaume WAMMEZEE MATE na kumtongoza kila siku

 MREMBO anayefanya vizuri katika mambo mengi nchini, Jokate Urban Mwegelo (pichani) ametaja sababu nne zinazowafanya wanaume kumzimikia, akiwemo nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.  Akiandika katika mtandao wake wa Kidoti Life Style, Jokate, mshindi wa pili wa Miss Tanzania 2006, alizitaja sababu hizo kuwa ni kujiamini, kujitegemea, kupendeza na tabasamu muda wote.   “Kujiamini ndiyo sababu kubwa ya kwanza inayonifanya nipendwe zaidi, hamna kitu kinachowavutia watu hasa wanaume kama kujiamini,” anaandika Jokate. “Kujitegemea ni sababu ya pili, binafsi naamini kwamba hakuna kitu kinachowaboa wanaume kama mwanamke ambaye anapenda vitu vya kupewa. Ukimuonesha mwanaume wewe unapenda kutafuta vyako, basi jua atakupenda zaidi.”   Jokate alisema sababu nyingine inayomfanya kuwa kivutio kwa wanaume ni kupendeza katika mavazi, hasa kwa kuvaa nguo zenye rangi ya kuonekana. Sababu nyingine aliyoitoa ni tabasamu, akiweka wazi kuwa tabasamu linamfanya aonekane m

Huyu Mzee Ndio Aliyetia Aibu Kwenye Bar Hii yenye Makahaba wanaocheza Nusu Uchi

 vijimambo kwenye bar zetu  

Kaniki,Matumla wanaswa na unga

  STRAIKA wa zamani wa Simba, Joseph Kaniki ‘Golota’ pamoja na bondia chipukizi, Mkwanda  Matumla wapo mikononi mwa polisi jijini Addis Ababa, Ethiopia kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya. Watuhumiwa hao wawili, raia wa Tanzania ambao wanajuta na kububujikwa na machozi kila kukicha walifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Jumatatu iliyopita kwenye eneo linaloitwa Arada. Siku yoyote kuanzia leo Jumanne watapanda kizimbani tena kwa mara nyingine. Mwanaspoti liliipata habari hii tangu Jumamosi jioni na kuanza kuifanyia kazi kabla ya Kaimu Balozi wa Tanzania Ethiopia, Samuel Shelukindo kuithibitishia Mwanaspoti jana  Jumatatu kwamba wanamichezo hao wameshikiliwa nchini humo na polisi wa Kitengo cha Uchunguzi wa Makosa ya Jinai. Wanamichezo hao walikamatwa na kilo saba za dawa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole jijini Addis Ababa, Mkwanda akikutwa na kilo nne wakati Kaniki alikuwa na kilo tatu. Walikuwa wanajiandaa kuunganisha ndege ya Shirika la Ndege

Yanga, Simba; Ama zao ama zetu

      Kikosi cha timu ya Mbeya City mara baada ya kupanda daraja, leo timu hiyo inapambana na Yanga jijini Mbey SAHAU Manchester United dhidi ya Crystal Palace au Arsenal vs Sunderland. Shughuli ipo Dar es Salaam na Mbeya leo Jumamosi, unaijua? Simba na Yanga zimetamba kila mmoja kwa kudai ama zao ama zetu, lakini mambo yote yatakuwa hadharani leo Jumamosi. Vinara wa Ligi Kuu Bara, Yanga kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa msimu mpya wa ligi inatoka nje ya Dar es Salaam na Simba kwa mara ya kwanza inarudi katika jiji lenye Bahari ya Hindi. Yanga, wanacheza na timu mpya yenye hamasa kubwa ya mashabiki mjini Mbeya ya Mbeya City kwenye uwanja chakavu wa Sokoine huku Simba ikiwa Dar es Salaam kucheza na timu king’ang’anizi ya Mtibwa Sugar katika uwanja wenye kapeti. Ingawa Yanga ilikuwa ikifanya mazoezi kwenye uwanja chakavu wa Shule ya Sekondari Loyola, Dar es Salaam, Kocha wake Ernest Brandts alisema: “Nimeuona Uwanja (Sokoine), si mzuri kabisa, sijui mechi yetu

Okwi ajiunga na URA ya Uganda

    Emmanuel Okwi akiwatoka wachezaji wa timu pinzani STRAIKA wa zamani wa Simba, Emmanuel Okwi amejiunga na URA ya Uganda ili kujiweka fiti akisubiri hatma yake kwenye klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia. Okwi amegoma kuichezea Etoile du Sahel mpaka itakapommalizia malipo yake ya kusaini mkataba pamoja na kumlipa malimbikizo ya mishahara ya miezi mitatu. “Nimetulia kwanza nione suala langu linaendaje na suluhisho ni nini. Ninataka sana kurudi uwanjani kucheza soka la ushindani,” alisema Okwi. “Ishu ni kwamba hawajanimalizia pesa ya kusaini mkataba pamoja na mishahara yangu ya miezi mitatu sasa,” alisema Okwi ambaye anaendelea kujinoa na URA ingawa haruhusiwi kucheza mechi ya mashindano kwa sababu ana mkataba wa miaka mitatu na Etoile du Sahel. Wakala wa mchezaji huyo amesema kwamba wanaendelea na mazungumzo na Etoile ili kutatua suala la Okwi ingawa habari za ndani zinasema kwamba anafanya mpango wa kumpeleka kwa mkopo kwenye klabu moja ya Daraja la Kwanz

Ray C na Zamaradi Mketema waingia katika bifu zito....Kisa ni PENZI la mwanaume

  So Rehema Chalamila aka Ray C na mtangazaji wa kipindi cha Take One cha Clouds TV, Zamaradi Mketema haziivi? Katika kile kilichoacha wazi midomo ya watu wengi, warembo hao leo wameingia kwenye vita vya maneno kwenye mtandao wa Instagram.   Alianza Zamaradi aliyepost picha yenye maneno ya mafumbo:    Picha hiyo aliiandikia maneno haya: Huwezi amini sikuchukii ila nimezidi kukudharau!!!! Katika watu wa mwisho kabisa ambao siwezi kupanic nao hata siku moja ni WEWE.. Dont waste your energy.. you have so much to accomplish ndugu.. mi hunipi tabu kabsa, kabsaa, kabisaaaaaaaaa yani sanasana unanichekesha tu na vituko visivyoisha.. lol!! Ila sikulaumu sana sio kosa lako maskini…    ungekuwa una akili usingefanya hayo ya kitoto tena hasa KWA KIPINDI HIKI.. na huenda hiyo sio akili yako mwaya.. NIMEKUSAMEHE BURE maana hapo ulipo hujielewi bado..  Dramas Dramas Dramas… sizipendagi ila huwa zinanifata zenyewe.. lol!!! Mbona naandamwaga hivi jamani kwani kosa langu

Shilole atachukuliwa hatua za kinidhamu baada ya kuianika CHUPI na SHANGA za kiunoni hadharani

WENYEKITI wa Kamati ya Umoja wa Mashirikisho ya Sanaa Tanzania, Kimela Billa, ameutaka uongozi wa Shirikisho la Muziki Tanzania, kumchukulia hatua ya kinidhamu, msanii wa muziki wa mduara Shilole ambaye pia ni muigizaji wa filamu kwa kosa la kukiuka maadili ya Tanzania katika tamasha la Serengeti Fiesta, mkoani Iringa.   Shilole alipanda jukwaani akiwa anacheza wimbo wake wa ‘Nakomaa na jiji’ huku akiwa amevaa nguo ambazo zilionesha maumbile yake yote ya mwili.   Akizungumza jijini Dar es Salaam, Billa alisema Shirikisho la muziki chini ya rais wake, Addo Novemba wanatakiwa kuchukua hatua zaidi juu ya shilole kwa kosa la kuwadhalilisha wanawake ikiwa ni pamoja na kukiuka maadili ya Tanzania.   “Hatukatai hayo mambo yapo lakini kwa staili ile sisi kama viongozi wa sanaa hatutaweza kuvumilia, shirikisho la muziki wakishindwa kutekeleza hili lazima kamati ilivalie njuga swala hilo, kiukweli wanalidhalilisha taifa hawa wasanii, mbona wanaume hafanyi

Irene Uwoya akamatwa na polisi kwa wizi wa simu aina ya iPhone 5

MSANII aliyewahi kutamba kisha kuporomoka kwa kasi katika tasnia ya filamu nchini Tanzania kwa sababu ya tabia zake chafu, Irene Uwoya, amefikishwa Kituo cha Polisi Msimbazi kwa wizi wa simu aina ya iPhone 5.   Kwa mujibu wa habari za kipolisi, mmiliki wa simu hiyo  ni mwanamme aliyejulikana kwa jina la Mohammed Marjey, mkazi wa Dar.   Uwoya ambaye siku hizi anajitutumua kwa kuanzisha kipindi kwenye runinga moja ya Bongo baada ya kushindwa kwenye filamu, alidakwa na askari wa Kituo cha Polisi Msimbazi, Dar baada ya kusakwa usiku na mchana kwa kutumia kumbukumbu ya jalada la kesi namba MS/RB/8522/13 WIZI KUTOKA MAUNGONI. Simu aina ya iPhone 5 kama inayodaiwa kuibiwa na Uwoya. Akizungumza na mwandishi wetu, Mohammed alisema simu hiyo aliinunua mwaka huu kwenye Duka la Grande Center jijini New York, Marekani alikokwenda kwa shughuli zake.Akasema Agosti 22, mwaka huu alirejea Bongo akiwa na simu hiyo ambayo ni toleo jipya la mwaka huu.   “Nilirejea hapa nchini nikiw

Rais Shein amtembelea padri aliyemwagiwa tindikali mjini UNGUJA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Padri Joseph Monesmo Magamba, wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui, alipofika katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kumpa pole,Mjini Unguja,baada ya kumwagiwa tindikali na watu wasiojulikana katika Mtaa wa Mlandege Mkoa wa Mjini Magharibi jana jioni, Padri alimwagiwa Tindikali alipokuwa akitoka kupata huduma ya Mtandao  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimsikiliza Padri Joseph Monesmo Magamba,wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui,akitoa maelezo jinsi alivyopata mkasa wa kutiwa  Tindikali jana na watu wasiojulikanwa,katika mtaa wa Mlandege Mjini Unguja, alipofika katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kumpa pole,ambapo amelazwa na kuapatiwa matibabu.  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiwafariji jamaa  na ndugu wa Padri Joseph Monesmo Magamba,wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia

"Namshukuru mungu maana sina UKIMWI...Mwenye wivu ajinyonge"..Recho

Msanii  wa  Bongo Movie, Rachel Haule ‘Recho’ amejikuta akivuja  jasho  la  furaha baada ya kupima Ukimwi na kujikuta yupo salama.   Tukio hilo lilitokea hivi karibuni maeneo ya Sinza Palestina ambapo Recho alienda kupima katika Hospitali ya Amen iliyopo Sinza ambapo kabla hajapata majibu hayo alikuwa akihaha huku na kule kutokana na wasiwasi.   Baada ya vipimo hivyo, Recho alipewa majibu yaliyoonesha kuwa yupo salama kitu ambacho kilimsababisha acheke na kuwataka  wenye  wivu  wajinyonge.   “Namshukuru Mungu  kwa sababu nimejikuta mzima baada  ya  kupima  UKIMWI, Mwenye wivu  na  maisha  yangu  ajinyonge  tu,” alisema Recho

HII NI LAANA....!!! PICHA ZA UCHI ZA MKE WA MTU NA KIGOGO WAKIFANYA "NGONO" ZANASWA...Zicheki hapa...!!

  Kigogo mmoja ambaye jina lake halikupatikana mara moja, anayefanya kazi  katika kampuni ya simu za mkononi  na mwanamke aliyetajwa kwa jina la Mwamvua anayedaiwa kuwa ni mke wa mtu wamerekodi video wakifanya uchafu na ‘clip’ hiyo imevuja. Habari za kuaminika kutoka kwa chanzo chetu makini zinasema kwamba mke wa kigogo huyo aitwaye Zainab ndiye anayesambaza video hiyo kwenye mitandao mbambali na mitaani. Inaelezwa kwamba, Zainab alianza kupatwa na wasiwasi na tabia ya mumewe muda mrefu, hivyo akaanza kumfuatilia kwa karibu, ambapo alifanikiwa kunasa meseji za mapenzi kati ya mumewe na Mwamvua.    Zainab alivumilia bila kumwambia mumewe, lakini aliendelea kumfuatilia ili apate uhakika. “Aliamua kuchukua namba za simu za yule mwanamke kisha akampigia na kumuonya amuachie mumewe, lakini akamjibu mbovu,”  alitutonya mnyetishaji wetu   Akaongeza:  “Lakini siku moja aliona picha ya huyo mwanamke

Hiki ni kilio cha Bondia Rashid Matumla baada ya mdogo wake kukamatwa na dawa za kulevya

Bondia Rashid ‘Snake man’ Matumla amedai endapo itathibitika mdogo wake Mkwanda anajihusisha kusafirisha dawa za kulevya atakuwa ameipa fedheha familia yao. “Mkwanda ameipa fedhea familia yetu, hii ni aibu kubwa ukizingatia vitendo hivyo vinakatazwa si Tanzania tu bali na kwenye nchi nyingine” Mkwanda ambaye kwa mujibu wa Rashid alipumzika kucheza ngumi miaka kadhaa iliyopita kutokana na kusumbuliwa na maradhi alikamatwa wiki iliyopita nchini Ethiopia akiwa na mchezaji wa zamani wa Simba, Joseph Kaniki na leo watapandishwa kizimbani nchini humo kwa tuhuma hiyo. “Mimi mwenyewe nashangaa ni lini amejiingiza kwenye kazi hiyo, hata wakati anaondoka hakuniaga, mimi kaka yao na familia hatuelewi chochote,” alisema Matumla. Alisema mdogo wake huyo alikuwa amebadilisha uraia na kuchukua uraia wa Sweden na kuoa hukohuko Sweden licha ya kwamba hapa Tanzania alikuwa amepanga Mbagala, Dar es Salaam na alikuwa anakuja na kukaa kwa muda na kisha kuondoka. “Ni mwezi sasa

"Kwa sasa Sina MPENZI ....mwenye nia ya dhati ANITAFUTE"...Baby Madah 9/11/2013 habari za kitaifa

  Leo katika interview na baby Madaha ambaye hivi karibuni amesaini mkataba mnono na kampuni ya Candy n’ Candy Records  ya jijini Nairobi nchini Kenya , Bongomovie.com wameweza kupata mambo matano ambayo mashabiki wa mwanadada huyu watakuwa hawajui kumhusu yeye.   Katika interview hiyo, baby Madaha  ametaja mambo matano ambayo anasema mashabiki wake wanahitaji kuyafahamu kumhusu yeye. Mambo hayo ni haya yafuatayo: 1. I’m single ( Sina  mpenzi) Mwanadada huyu amesema kuwa kwa sasa yupo single na  yuko  bize  na PESA. Ila  kama  kuna  mwanaume  mwenye  nia  ya  dhati  anaweza  kumtafuta. 2. Anasoma degree ya sanaa kwenye sayansi ya siasa na historia (B.A- Political science and History) - chuo kikuu huria jijini Dar es Salaam.. 3. Mama yake mzazi ndio rafiki yake mkubwa maishani 4. Ni mpenzi wa soka na ni mshabiki wa Chelsea na anavutiwa na  Kevin-Prince Boateng wa club Schalke 04 ambaye ndiye alisababisha akanyoa nywele staili aliyonayo baby madaha kwa

Diamond ajibu tuhuma za KUMTUNDIKA MIMBA mwanafunzi na zile za wimbo wa Dayna

  Hatimaye Diamond Platnumz leo amejibu tuhuma kadhaa zilizokuwa zikimkabali ikiwemo ile ya Dayna Nyange kudai kuwa alitumia beat ya wimbo wake kurekodi wimbo wake unaotamba sasa, Number 1 na pia kuhusu Baba Levo kudai Diamond alimuibia chorus ya wimbo wake.  Katika mahojiano na kipindi cha XXL cha Clouds FM, Diamond pia amejibu scandal kuhusu kumzalisha mwanafunzi iliyoandikwa na magazeti  ya  leo.

Soma hapa "shairi la penzi lake" instagram...Albam yake mpya iko jikoni inapikwa

Haya wale wenye kiu na ujio mpya wa Ray C mnaweza kuanza kuandaa makoo yenu sababu chakula kimeshawekwa jikoni na muda si mrefu mnaweza kukaribishwa mezani. Ray C ameshea picha kadhaa akiwa studio na wadau mbalimbali akiwemo Bab Tale na Said Fella, na kama haitoshi ameweka mashairi ya wimbo wake ambao unaonekana ndio aliokuwa akiurekodi wakati anapiga picha hiyo na kuandika “Mashairi ya my new song…,its a very beautiful song…am sooooooo happy..Thank you Lord”. Unaweza kuyapitia na kuanza kutengeneza taswira ya kile kinachokuja kutoka kwa Rehema Chalamila amabaye anasubiriwa kama nguo ya Christmas au Idd kwa watoto. Pia Ray C amesema album yake inakuja hivi karibuni

Tazama picha ya Wazazi wa Dogo Janja walivyotua Bongo na Kuongea na Ostaz Juma Baada ya Kusikia Fununu za Mtoto wao Kutaka Kurudi Tip Top

Wazazi wa Dogo Janja aka Janjaro, wamekuja Dar es salaam wiki hii kuangalia maendeleo ya mtoto wao baada ya kusikia tetesi kuwa anarudi Tip Tipo Connection na kuhisi Watanashati wameshindwa kumsimania. Ostaz Juma kushoto,wazazi wa Dogo Janja katikati na Dogo Janja wa mwisho Wakiongea na Bongo5 jana wakiwa katika Hotel ya Atrium, Sinza jijini Dar es salaam, Baba wa Dogo Janja, Mzee Chende alisema waliamua kusafiri kutoka Arusha mpaka Dar ili kukutana na mmiliki wa Watanashati Ostaz Juma, ili wajue kimetokea nini kwa mtoto wao. Wazazi wa Dogo Janja “Tuna week moja, mimi na mke wangu tumetoka Arusha kukutana Ostaz Juma ili tujue nini kilitokea baada ya kusikia Dogo Janja anataka kururi Tip Top, sasa tumekuna na Ostaz Juma tumeongea tumekuta mtoto wetu hana tatizo lolote na yupo salama kwa Watanashati na tumejua yalikuwa mambo ya kuzusha tu,” alisema baba yake na Janjaro. Kwa upande wake mmiliki wa kampuni ya Watanashati Entertainment, Ostaz Juma na Musoma alisema n

Obama kuendeleza shinikizo kwa Syria

Rais wa Marekani Barack Obama, amesema kuwa atafanya juhudi zaidi za kidiplomasia kuangamiza zana za kemikali za Syria , lakini pia ameambia jeshi lake kuwa tayari kuchukua hatua ikiwa juhudi zake zitafeli. Kwenye hotuba yake , Obama alisema kuwa amelitaka baraza la Congress kuakhirisha kura yake kuhusu kutumia nguvu za kijeshi dhidi ya Syria. Marekani imetishia kufanya mashambulizi ya angani baada ya shambulizi la kemikali kuwaua mamia ya watu mjini Damascus mwezi jana. Urusi imependekeza kuwa silaha hizi ziwekwe chini ya udhibiti wa jamii ya kimataifa. Ingawa maafisa wa Syria wamekubali kutii agizo la Marekani, nchi hiyo pamoja na washirika wake wana wasiwasi ikiwa Syria itafanya kama inavyosema. Athari za vita nchini Syria , watoto hawajasazwa Mpango wa Urusi ulisababisha siku moja ya mashauriano mazito ya kidiplomasia katika Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne. Akiongea katika Ikulu ya White House, Obama alisema kuwa serikali yake, ilikataa wito wa kuch

SADC yamuonya Kagame kuhusu mipango yake ya kuivamia Tanzania baada ya kuomba msaada wa kijeshi toka Kenya na Uganda

MZOZO wa kidiplomasia alioibua Rais wa Rwanda, Paul Kagame kwa Rais Jakaya Kikwete, sasa unaonekana kuchukua mwelekeo mpya, baada ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), kumuonya kiongozi huyo kuacha mara moja fikra zozote mbaya dhidi ya Tanzania, MTANZANIA Jumatano limedokezwa.  Habari za uhakika na za kuaminika kutoka miongoni mwa viongozi wa juu wa SADC na maofisa wa Serikali, waliokuwa katika ujumbe wa Rais Jakaya Kikwete aliyekuwa akihudhuria Mkutano wa viongozi wa Maziwa Makuu huko Uganda hivi karibuni, zinaeleza kuwa tayari Jumuiya hiyo imekwisha mpatia ujumbe huo mmoja wa mawaziri aliyekuwa ameandamana na Kagame muda mfupi baada ya kikao chake na Kikwete. Taarifa ambazo MTANZANIA Jumatano imezinasa, zinaeleza kuwa, kiongozi mmoja wa juu wa Msumbiji ambaye alikuwa pia Uganda, alikaririwa akimueleza Waziri huyo wa Kagame kuacha kabisa fikra za kuishambulia Tanzania, kwa sababu ya uamuzi wake wa kupeleka vikosi vyake Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kong

Hakimu apigwa na wanajeshi wa JWTZ huko karagwe kwa kudhaniwa kuwa ni Mnyarwanda

Matendo Manono (kushoto) Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Matendo Manono ambaye ni Hakimu Mkazi katika Mahakama ya Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera amelalamikia kitendo cha kupigwa na kujeruhiwa vibaya na Askari wa Tanzania, katika zoezi la kuwaswaga wahamiaji haramu wa kinyarwanda wanao ishi nchini Tanzania.    Soma maelezo ya hakimu huyo hapo chini... " i have a serious contempt of this country...while they know for sure that this country has no National ID stil they want us to show Citizenship ID...   Imagine this was travelling to western part of TZ (Karagwe) today i have been arrested by the damned Immigration, police officers and JW people that am a prohibited immigrant simply because am tall with big (long,edged?)nose .. i have been seriously humiliated and beaten simply because i resemble Rwandese something which is neither sin nor unlawful under The Immigration Act or The Citizenship Act.... I don't know if those peopl

Mwandishi wa habari wa gazeti la The Citizen na mwananchi mkoani Singida, Awila Silla amenusurika kuuawa na mtu anayedhaniwa kuwa Jambazi baada ya kukatwa katwa mapanga kichwani na kusababisha kuzirai. Tukio hilo limetokea juzi saa mbili usiku jirani na mahakama ya mwanzo ya Utemini mjini Singida. Awila ambaye amelazwa wodi 2 katika hospitali ya mkoa amedai kuwa baada ya kukutana na kijana huyo aliamuriwa kutoa fedha na baada ya kudai hana, jibu hilo lilisababisha kijana huyo kuanza kumkata Mapanga na alipoangauka na kuzirai alinyang’anywa simu yake ya kiganjani . Hata hivyo Awila amedai kuwa bado hajatoa taarifa ya tukio hilo polis

Mwandishi wa habari wa gazeti la The Citizen na mwananchi mkoani Singida, Awila Silla amenusurika kuuawa na mtu anayedhaniwa kuwa Jambazi baada ya kukatwa katwa  mapanga kichwani na kusababisha kuzirai. Tukio hilo limetokea juzi saa mbili usiku jirani na mahakama ya mwanzo ya Utemini mjini Singida.  Awila ambaye amelazwa wodi 2   katika hospitali ya mkoa amedai kuwa  baada ya kukutana na kijana huyo aliamuriwa kutoa fedha na baada ya kudai hana, jibu hilo lilisababisha kijana huyo kuanza kumkata Mapanga na alipoangauka na kuzirai alinyang’anywa  simu yake ya  kiganjani . Hata hivyo Awila amedai kuwa bado hajatoa taarifa ya tukio hilo polis

Jalada la kesi ya mbuge SUGU wa Mbeya mjini latua kwa DPP

JALADA la Kesi inayomkabili Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (CHADEMA), limefikishwa katika Ofisi ya Mwanasheria wa Serikali. Mbilinyi maarufu kwa jina la ‘Sugu’, anadaiwa kumjeruhi askari wa Bunge katika vurugu zilizotokea Bungeni mwishoni mwa wiki iliyopita.  Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Susan Kaganda alisema polisi wameshapeleka jalada la mbunge huyo katika Ofisi ya Mwanasheria wa Serikali na kwamba upelelezi unaendelea. “Tayari jalada la kesi yake lipo katika Ofisi ya Mwanasheria wa Serikali na upelelezi unaendelea,” alisema. Kwa mujibu wa vyanzo kutoka Jeshi hilo, Sugu alikwenda Polisi kujisalimisha siku ya kuahirishwa Bunge na kwamba aliambiwa arudi tena kuripoti Jumatano (kesho). “Kama akiripoti Jumatano, ndiyo itajulikana na kama jalada lake litakuwa limeshafikishwa mahakamani au bado,” kilieleza chanzo hicho. Habari za uhakika kutoka katika Mahakama ya Mkoa wa Dodoma hadi jana mchana, hakukuwa na jalada lolote lililokuwa lim

Jokate afunguka baada ya kutuhumiwa kugawa URODA kwa LUCCI ili auze sura

Baada  ya  kutuhumiwa  kugawa  uroda  kwa  Lucci  ili  aweze  kuuza  sura  katika  video  mpya   ya  "dada, kaka" , Jokate  ameamua  kufunguka  na  kuzikanusha  tuhuma  hizo.... Huu  ni  ujumbe  wake  alioutoa  instagram. "Okay leo nimeamua kupitia page yangu ya Instagram ku-address the following pressing matters kwenye ulimwengu wa majungu.  1. Luciano Gadie Tsere is NOT my LOVER and noooo hatumegani kisela. Na hata kama it were true inakuhusu nini. Sioni ishu. Kwenye Sanaa kuna kitu kinaitwa kuweka uhalisia.  And that's what we did na KAKA DADA. I respect Lucci. Ni kaka yangu na tunafanya kazi nyingi sana zinakuja. Kuna watu wanefungua mpaka BBM group to discuss me and Lucci and this so called affair. Jamani kuliko maneno tufanyeni Kazi kuendeleza nchi yetu  2. Sijifanyi mtakatifu. Ila najitahidi kufanya matendo yanayompendeza Mungu. Na kwasababu kama binadamu sina ukamilifu basi only God can really judge me cause ndio anajua moyo wangu ku

Haya ndo mashitaka matatu aliyosomewa makamu wa Rais wa Kenya mbele ya mahakama ya ICC

  William Ruto amekana mashtaka yote yanayomkabili kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).    Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama hiyo, Fatou Bensouda anayesimamia kesi hiyo, alisema watuhumiwa wawili waliofikishwa mahakamani hapo jana, Ruto na mtangazaji wa Redio, Joshua arap Sang wanakabiliwa na mashtaka matatu kila mmoja, ambayo ni kuwalazimisha watu kukimbia makazi yao, mauaji na kuchochea ghasia.   Kesi hiyo imeanza kusikilizwa siku chache baada ya Bunge la Kenya kupiga kura kutaka nchi hiyo ijitoe uanachama wa ICC, wakieleza kwamba imekuwa haina tija na inatumiwa kuwakandamiza Waafrika.   Ruto ambaye alionekana kujiamini alifika kwenye jengo la Mahakama akiwa ameambatana na baadhi ya wabunge waliosafiri kutoka Kenya hadi The Hague kwa ajili ya kumuunga mkono.   Mwendesha Mashtaka wa ICC, Fatou Bensouda alianza kwa kusoma mashtaka matatu yanayomkabili ki