Skip to main content

Posts

Showing posts from August 3, 2014

Israel yaanza kushambulia Gaza

Israel imeanza kufanya mashambulizi ya angani dhidi ya Gaza katika hatua yake ya kujibu mashambulizi yaliyofanywa na wapiganaji wa kipalestina dhidi ya Israel. Mashambulizi haya yametokea baada ya makubaliano ya siku tatu ya kusitisha vita kuvunjika. Serikali ya Israel imesema kuwa iliamuru jeshi kujibu mashambulizi hayo kwa ukali. Jeshi la Israel linasema linashambulia maeneo yanayotumiwa na wapiganaji hao katia ukanda wa Gaza. Kuna taarifa za kutokea mlipuko mkubwa katika ukanda wa Gaza na wakazi wa Palestina wamekuwa wakiodnoka katika maeneo hayo. Hamas ilikanusha madai ya kuongezwa muda wa makubaliano ya kusitisha vita ikisema kuwa Israel ilikataa kukubaliana kufanya mkutano kulingana na matakwa yao kwa masharti ya Misri ikiwemo kumaliza

WHO:Hatariiio..'Ebola ni janga la kimataifa'

Shirika la afya duniani WHO limetangaza kuenea kwa ugonjwa wa Ebola Magharibi mwa afrika kama janga la kimataifa linalohitaji kushughulikiwa kwa dharura. WHO imesema kuwa mataifa yalio na maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo hayana uwezo wa kudhibiti kiwango cha virusi hivyo na hivyo basi yanahitaji usaidizi wa kimataifa. Tangazo hilo linajiri baada ya mazungumzo ya dharura mjini Geneva kuhusu uwezekano wa kutuma wataalam wa ugonjwa wa maambukizi ili kuudhibiti ugonjwa huo ambao ni hatari zaidi. Ugonjwa huo umewaua zaidi ya watu mia tisa magharibi mwa afrika . Mataifa yalioathiriwa vibaya ni Guinea,Liberia na Sierra Leone,lakini pia visa vimeripotiwa nchini Nigeria.

Hizi ndizo sababu ya Urusi kulipiza kisasi kwa Marekani na Ulaya

Urusi imetangaza marufuku ya vyakula kutoka kwa muungano wa Ulaya, Marekani na nchi zingine kadha za magharibi ambazo zilikuwa zimetangaza vikwazo dhidi ya Urusi kutokana na sera zake nchini Ukraine. Waziri mkuu nchini Urusi Dmitry Medvedev aliuambia mkutano wa serikali kuwa Urusi haitaruhusu tena uingizwaji wa Nyama, Samaki, Matunda na bidhaa zingine kutoka mwa jumuiya ya Ulaya, Marekani, Australia, Canada na Norway. Medvedev amesema kuwa vikwazo hivyo vitadumu kwa kipindi cha mwaka mmoja. Amesema kuwa Urusi inatathmini kupiga marufu mashirika ya ndege ya nchi za magharibi yanayotumia anga ya Urusi kuingia barani Asia. Wadadisi wanasema kuwa Urusi inategemea zaidi chakula kutoka nje asilimia kubwa ikiwa ni kutoka kwa nchi za magharibi.

TAMASHA LA MATUMAINI 2014 KESHO NDIYO KESHO TAIFA

SIKU iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa burudani mbalimbali imewadia ambapo kesho Agosti 8, katika Uwanja wa Taifa patakuwa hapatoshi wakati Tamasha la Usiku wa Matumaini litakapokuwa likichukua nafasi. Mabondia Mada Maugo na Thomas Mashali wakitunishiana misuli. Akizungumza na Centre Spread, mratibu wa tamasha hilo, Luqman Maloto alisema kuwa maandalizi yote yameshafanyika na tayari mkali wa muziki kutoka Nigeria anayetamba na ngoma ya Johnny, Yemi Alade ameshatua nchini, kinachosubiriwa ni burudani mwanzo mwisho. “Kila kona ya burudani imeshakamilika hivyo kama wewe ni mpenzi wa ndondi kuna ngumi kati ya mabondia Mada Maugo dhidi ya Thomas Mashali, JB dhidi ya Cloud 112, Said Memba dhidi ya Khalid Chokoraa na wengineo. Navy Kenzo. “Wapenzi wa Bongo Fleva, kutakuwa na mfalme wao, Ali Kiba akiwa sambamba na mastaa kama Shilole, Madee, R.O.M.A, Meninah, Navy Kenzo, Scorpion Girls, Juma Nature na wengine kibao,” alisema Maloto na kuongeza: “Kwa wale w

SHILOLE, MCHUMBA’KE WAZICHAPA!

Lile penzi lililopata ‘promo’ ya kutosha ndani ya muda mfupi kati ya mwanamuziki Zuwena Mohammed ‘Shilole’ na Nuh Mziwanda limeingia shubiri baada ya juzikati wawili hao kuzichapa. Kisa cha wawili hao kuzibuana kinadaiwa ni baada ya Nuh kukuta sms tata ya mwanaume kwenye simu ya Shilole ambapo inadaiwa baada ya jamaa huyo kumtaka mchumba wake huyo ampigie aliyetuma meseji hiyo kukawa na kusuasua. Mwanamuziki Zuwena Mohammed ‘Shilole’. Chanzo chetu cha habari kilichoomba jina lake lisichorwe gazetini kilitiririka: “Shilole na mchumba’ke walikuwa chumbani, mara ikaingia sms kwenye simu ya Shilole. “Nuh alipoiona alimlazimisha Shilole ampigie jamaa aliyetuma sms na aweke ‘loud speaker’, Shilole alipoipiga ile namba, akajichanganya kidogo licha ya kuwa, jamaa alikuwa anamjua na wala hakuwa mpenzi wake ila ni washikaji tu. Mwanamuziki na mpenzi wa Shilole, Nuh Mziwanda akipozi. “Kuona vile si Nuh akaanza kumpiga na hapo ndipo timbwili lilipotokea. Wote waliumia ila Nuh

AZAM FC VS MTIBWA SUGAR HAPATOSHI TAMASHA LA USIKU WA MATUMAINI TAIFA DAR

KIKOSI cha pili cha mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara, Azam fc kitakabiliana na Mtibwa Sugar katika mchezo wa kirafiki utakaopigwa leo katika Tamasha la Usiku wa Matumaini , uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Hii itakuwa mechi nzuri kwa timu zote kuangalia uwezo wa wachezaji waliowasajili na wale waliopandishwa kutoka timu za vijana. Afisa habari wa Azam fc, Jafar Idd Maganga alisema wanauchukulia mchezo huo kwa uzito wa hali ya juu kwasababu ni nafasi nzuri kwa wachezaji wao kuonesha uwezo mbele ya timu bora ya Mtibwa Sugar

MHE. PINDA AWASILI MWANZA KUFUNGA MAONESHO YA NANENANE

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mwanza, Dr. Anthony Diallo baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza  August 7, 2014  ambako anatarajiwa kuwa  mgeni rasmi katika kilele cha sherehe za wakulima Nanenane mjini Mwanza August 8, 2014.Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi, Evarest Ndikilo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula  na Ushirika, Erasto Zambi baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege  wa Mwanza August 7, 2014 ambako August 8,2014 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika  kilele cha sherehe za  wakulima Nanenane  jijini Mwanza . Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mwanza, Dr. Anthony Diallo na kulia ni mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarest Ndikilo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarest  Ndikilo kwenye  Ikulu ya Mwanza August 7, 2014 ambako August 8 anatara

Wanasayansi Duniani kukutana Dar kongamano la 25 la Wajiolojia

Mtendaji  Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST ) na Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya makongamano  ya Wajiolojia  Afrika na  wanasayansi vijana Duniani, Profesa Abdulkarim Mruma (katikati) akisisitiza jambo wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu  kongamano la 25 la Wajiolojia Afrika na   mkutano wa tatu  wa vijana wanasayansi  kutoka nchi mbalimbali duniani. Makongamano hayo yanatarajiwa kufanyika tarehe 11- 16 Agosti, 2014 jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Nishati na Madini, Badra Masoud. Wengine, kwanza kulia ni Mwenyekiti wa mtandao wa Vijana wanasayansi kwa upande wa Tanzania Steven Nyagonda, Rais wa Vijana wanasayansi Duniani  Meng Wang na Katibu wa Kamati ya Maandalizi, Profesa Nelson Boniface. Rais wa Wanasayansi Vijana duniani, Meng Wang (wa pili kulia) akiongea jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuelezea kuhusu mkutano wa tatu wa wanasayansi vijana kutoka nchi mbalimbali duniani, ku

KOCHA TAIFA STARS ASHAURI KUPUNGUZA IDADI YA WACHEZAJI WA KIGENI LIGI KUU BARA

KOCHA mkuu wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania, Mzalendo, Mshindo Msolla amesema walimu wa kigeni wanaokuja nchini kufundisha klabu kubwa za ligi kuu hawasaidii kuendeleza soka la Tanzania. Msolla alisema makocha hawa wanapewa mkataba wa mwaka mmoja au miwili, hivyo wanahangaika kusajili wachezaji nyota wa kigeni ili kupata mafanikio na kuondoka, jambo ambalo linawanyima nafasi ya kuwajenga wachezaji wazawa kwa muda mrefu.

MAN CITY WAMTAKA SERGIO AGUERO KAUNGUKA MITANO KABLA YA KUANZA LIGI KUU ENGLAND

Manchester City wanamtaka Sergio Aguero asaini mkataba mpya kabla ya kuanza msimu mpya. MANCHESTER City wanatumaini kuwa Sergio Aguero atasaini mkataba mpya utakaomfanya alipwe paundi laki mbili na elfu 10 kwa wiki kabla ya kuanza kwa msimu mpya. Mabingwa hao wa England wameweka wazi kuwa mshambuliaji huyo wa Argentina yupo katika mipango yao ya baadaye pamoja na nahodha Vincent Kompayn na mazungumzo yanaendelea vizuri. Barcelona na Real Madrid wameweka wazi siri ya kuvutiwa na mshambuliaji huyo mwenye miaka 26, lakini City wanafanya haraka ili kumuongezea mkataba wa miaka mitano. Kusoma zaidi bofya

Mshukiwa wa Al shabaab akamatwa Kenya

Maafisa wa polisi nchini Kenya wanasema wamemnasa mshukiwa mkuu wa Al-Shabaab mjini Nairobi. Mshukiwa huyo alikuwa nchini Kenya kutafuta matibabu. Duru zingine zinasema kuwa alikuwa mwanahabari zamani na anashukuwa kujihuhusisha na mauaji ya waandishi wa habari wa Somali huko Mogadishu. Ni nadra kunasa washukiwa kama hawa wanaoingia nchi jirani ya Kenya kupitia mipaka yake ambayo bado haina ulinzi wa kutosha. Mshukiwa huyo anadhaniwa kuwa Hassan Hanafi na amekuwa akizuru Kenya mara kwa mara. Maafisa wa polisi wameambia BBC kuwa alitiwa nguvuni siku chache zilizopita na anahojiwa na maafisa wa kitengo maalum cha polisi kinachoshughulikia maswala ya ugaidi. Maafisa wa Usalama wa Somali wamesema kuwa ushirikiano kati ya majasusi wa Kenya na Somali ndiko kulipelekea au kuwezesha kukamatwa kwa mshukiwa huyo ambaye anadai ameshikwa kimakosa na kufananishwa na mtu mwingine. Hanafi anashukiwa kutekeleza au kufadhili mauaji ya wanahabari mjini Mogadishu. Zaidi ya wanahaba

Nitakuwa Rais wa mwisho kuongoza TZ masikini - JK

Rais Kikwete amesema kuwa anataka na anatamani kuwa Rais wa mwisho wa Tanzania kuongoza nchi ambayo ni maskini na hivyo atatumia muda wake uliobakia katika uongozi kuelekeza nchi kwenye mwelekeo huo. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa anataka na anatamani kuwa Rais wa mwisho wa Tanzania kuongoza nchi ambayo ni maskini na hivyo atatumia muda wake uliobakia katika uongozi kuelekeza nchi kwenye mwelekeo huo. Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa jambo la msingi kabisa la kama Watanzania watanufaika na ugunduzi wa gesi asili ama watabakia katika hali yao ya sasa ya umasikini ni aina ya uongozi ambao nchi hiyo itaupata, uongozi wenye uwezo wa kufanya maamuzi sahihi kwa kadri nchi inavyozidi kusonga mbele. Rais Kikwete pia anasema kuwa Tanzania inatarajia kuanza kupokea mapato yake ya kwanza kutokana na raslimali ya gesi asilia katika miaka sita ijayo, kuanzia Mwaka 2020. Rais Kikwete ameyasema hayo jana, Jumatatu, Agosti

PENZI LA SHILOLE NA NUH MZIWANDA LAVUNJIKA..VIPI KUHUSU TATOO ALIYOJICHORA NUH ? CHECK HAPA

Siku ya jana haikua nzuri kwa Shilole na Nuh Mziwanda  baada ya kugomabana sana hadi Nuh Mziwanda akaamua  kuchukua vitu vyake na kuhama Kwa Shilole, Gazeti la  Makorokocho imezipata taarifa hizi za motomoto kupitia  kwa mtu  aliyekuepo eneo la tukio aliyedai kuwa yeye alishangaa  kuskia mikikimikiki ndani ya Harrier na baadae milango ya  gari ikafunguliwa wakatokeza wasanii wawili wa bongo flava  ambao ni Shilole na Nuh Mziwanda na walikua  wakirushiana maneno ghafla wakatokeza watu  wengine wakiongozwa na Msanii Chege  Chigunda wakaamulizia ugomvi huo bila Mafanikio  kwani Nuh Mziwanda alikua anamuambia Shilole amrudishie simu yake lakini Shishi alishindwa kufannya  hivyo kwa madai eti ufunguo upo nyumbani, Kweli? wakati  dakika chache zilizopita walikua ndani ya Gari. Nilipomtafuta Nuh Mziwanda hakutaka kubisha na akatiririka  A to Z ya sakata hilo, Nuh Mziwanda: Jana Usiku tulialikwa  Chakula Usiku kwa Producer Dibanjo, mitaa ya  Mango Garden Kinondoni, mimi na

Viongozi wa Afrika wakutana Marekani

Moja ya mikutano ya kwanza ilikuwa kati ya Rais wa DRC Joseph Kabila na waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry Takriban viongozi hamsini kutoka nchi za Afrika wanatarajiwa kuhudhuria mkutano wa siku tatu utakaohitimshwa Jumatano. Mkutano huo wa Marekani na viongozi 50 wa nchi za Afrika uliandaliwa na idara ya biashara ya Marekani. Katibu wa maswala ya Biashara wa Marekani Penny Pritzker amesema kuwa tangazo rasmi litatolewa kwenye mkutano huo kuhusiana na takriban dola milioni 900 zitakazotolewa kwa mipango ya kibiashara. Hayo yakijiri, Marais watatu, rais wa Liberia, wa Guinea, na wa Sierra Leone wamevunja safari zao kuhudhuria mkutano huo kufuatia janga la Ebola. Ebola imesababisha vifo vya watu Zaidi ya 800 katika kanda ya Afrika Magharibi kwa ujumla. Kufanyakia kwa mkutano huu ni kutimia kwa ahadi ya Rais Obama aliyotoa mwaka uliopita alipozuru nchi tatu za Afrika Senegal, Tanzania, na Afrika Kusini. Kongamano hilo litaangazia biashara kati ya Mar

Wazazi wamtelekeza mtoto mgonjwa wa akili

Mama wa kupangisha bi Chanbhua akiwa na mwanawe (Gammy) Familia moja kutoka Australia imekanusha kumtelekeza mtoto waliomlipa mama mmoja nchini Thailand kuwabebea kufuatia ripoti za daktari kuwa alikuwa na upungufu wa kiakili. Pattharamon Chanbua, 21, aliingia mkataba wa kuwasaidia Waaustralia hao kupata mtoto baada ya mwanamke huyo kushindwa kubeba mimba mwenyewe. Hata hivyo alipojaaliwa akazaa mapacha wazazi hao walikuja wakamchukua mmoja ambaye akili zake zilikuwa timamu na wakamuacha nyuma mtoto Gammy baada ya ripoti ya daktari kuonesha kuwa alikuwa na akili taahira. Chanmbua anasema kuwa punde baada ya madaktari kugundua kulikuwepo na hitilafu wazazi hao wa Gammy walimshauri aavye mimba hiyo lakini akkataa kwani haiambatani na dini yake ya Kibudhaa. Wazazi hao wa Gammy wamejitetea wakisema kuwa walimchukua mtoto mmoja baada ya madaktari kutarajia kuwa Gammy angekuwa na matatizo ya ugonjwa wa moyo na maambukizi ya mapafu. Baba ya mapacha hao wawili aliwate