Moja ya mikutano ya kwanza ilikuwa kati ya Rais
wa DRC Joseph Kabila na waziri wa mambo ya
kigeni wa Marekani John Kerry
Takriban viongozi hamsini kutoka nchi za Afrika
wanatarajiwa kuhudhuria mkutano wa siku tatu
utakaohitimshwa Jumatano.
Mkutano huo wa Marekani na viongozi 50 wa nchi
za Afrika uliandaliwa na idara ya biashara ya
Marekani.
Katibu wa maswala ya Biashara wa Marekani
Penny Pritzker amesema kuwa tangazo rasmi
litatolewa kwenye mkutano huo kuhusiana na
takriban dola milioni 900 zitakazotolewa kwa
mipango ya kibiashara.
Hayo yakijiri, Marais watatu, rais wa Liberia, wa
Guinea, na wa Sierra Leone wamevunja safari zao
kuhudhuria mkutano huo kufuatia janga la Ebola.
Ebola imesababisha vifo vya watu Zaidi ya 800
katika kanda ya Afrika Magharibi kwa ujumla.
Kufanyakia kwa mkutano huu ni kutimia kwa ahadi
ya Rais Obama aliyotoa mwaka uliopita alipozuru
nchi tatu za Afrika Senegal, Tanzania, na Afrika
Kusini.
Kongamano hilo litaangazia biashara kati ya
Marekani na Bara la Afrika. Kwa mujibu wa mhariri
wetu China inaongoza kwa kiwango cha biashara
wanayofanya na nchi za Afrika
Mlipuko wa homa ya Ebola umelazimisha rais
kukatiza safari yake Marekani
China inafanya biashara ya takriban dola bilioni 200
na bara la Afrika. Kiwango hicho ni Zaidi ya
maradufu kiwango cha biashara ya Marekani na
nchi za bara Afrika.
Ingawa China imeongoza, kulingana na utafiti wa
Shrika la Fedha Duniani, China ina uhusiano wa
kibiashara nan chi chache tu.
China inafuatiwa na Japan, India na Ulaya.
Hayo yakijiri, Ghana imesema itatafuta msaada
kutoka kwa Shirika la fedha duniani (IMF) ili
kuimarisha uchumi wao kwani Ghana imekuwa kati
ya nchi zilizovuta mkia kiuchumi kote ulimwenguni
mwaka huu.
Mwaka 2013, 67% ya biashara ya Afrika na
Marekani ilifannywa na nchi tano tu - Nigeria, South
Africa, Angola, Misri and Algeria.
Marekani hununua bidhaa nyingi kutoka nchi hizi
inapolinganishwa na bidhaa wanazouzia nchi hizo.
Mafuta huchangia Zaidi ya asilimia hamsini ya
bidhaa zinazouzwa kwenda Marekani.
Takrimu za uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja
(FDI) figures zinaonyesha mtindo fulani – mwaka
2012 74% ya fedha zilizowekezwa na nchi za kigeni
barani Afrika ziliendea nchi tano - Nigeria, Afrika
kusini, Misri, na Algeria huku Mauritius ikichukua
nafasi ya Angola na kuwa nchi ya tano katika
orodha hiyo.
Mwaka 2011, 75% ya bidhaa zilizouzwa kwenda
China kutoka nchi zilizo kusini mwa Jangwa la
Sahara zilitoka nchi tano tu, huku nchi sita
zikichukua Zaidi ya 80% ya bidhaa zilizouzwa na
China barani Afrika.
Ghana inalenga kupata msaada kufadhili miradi
yake ya kawi
Huku zaidi ya nchi hamsini zikitarajia kufaidika
kutoka kwa mkutano wao na rais wa Marekani
Barck Obama, kuna nchi ambazo hazikualikwa -
Jamhuri ya Afrika ya Kati, Eritrea, Sudan na
Zimbabwe.
Waziri wa habari wa Zimbabwe Jonathan Moyo
alipuuzilia kutoalikwa na Marekani kuhudhuria
mkutano huo wa Viongozi wa Afrika kuwa “si
jambo.”
“Tunaelewa kuwa Marekani inalenga kutimiza
matakwa yake, na inahofia kuwa Uchina imekuwa
kwa haraka na kuongoza katika mahusiano na
Afrika,” Mugabe aliarifu Gazeti linalomilikiwa na
taifa, Herald.
Watakaohudhuria wameandaliwa chajio na Rais
Obama, White House, baada ya mkutano wa leo.
Mada zitakazoangaziwa kesho (Jumatano) ni
biashara, usalama, na uongozi.
Wanaokosoa kongamano hilo wamesema kuwa
Obama hakufanya mikutano ya moja kwa moja na
marasi wan chi za Afrika.
Bwana Kerry alikutana na waziri mkuu wa Libya
Libyan Abdullah al-Thinni
Kualikwa kwa Rais Yoweri Museveni kumevutia
wanaharakati wa haki za wanaofanya mapenzi ya
jinsia moja baada ya Museveni kuidhinisha,
mapema mwaka huu, muswada ulioweka adhabu
kali dhidi ya wanaofanya mapenzi ya jinsia moja.
Mara kwa mara, Obama,ameshutumiwa kwa
kupuuza uhusiano wa Marekani na bara la Afrika
huku ikizingatiwa kuwa Obama ni Rais wa kwanza
ambaye ni Chotara wa Mwafrika na Mmarekani.
Kando na ziara ya Obama mwaka uliopita, Obama
amezuru mara mbili nchi zilizo kusini mwa jangwa
la Sahara, katika kipindi chake cha uongozi. Alipitia
Ghana kwa muda mfupi, Julai 2009, na pia
kuhudhuria mazishi ya hayati Nelson Mandela,
shujaa wa Afrika kusini.
Comments
Post a Comment