Skip to main content

Posts

Showing posts from August 17, 2014

Hatimaye Diomond atangaza rasmi kufunga ndoa na Wema unajua ni kwa nini stori kamali soma hapa!!

Msanii huyo ghali zaidi nchini kwa sasa, ametamka hayo alipozungumza na Mwanaspoti nyumbani kwake Sinza jijini Dar es Salaam juzi Jumatano. Alisema kuna mambo mengi yaliyomchelewesha kufikia hatua hiyo, ikiwamo maandalizi kwani amepanga mashabiki wake wahudhurie harusi hiyo. “Ndoa ni kitu cha heri na baraka, lakini kitu kinachofanya kidogo mambo yachelewe ni kwamba sisi au mimi ni mtu ninayefahamika, kwa hiyo hata ndoa yangu watu wengi wanatamani waihudhurie,” alisema Diamond. Pia amesisitiza kwamba ndoa si jambo la masihara kwani ni tendo la kiimani na ndio maana amekuwa makini katika mipango yake. “Nataka kila kitu kishuhudiwe na mashabiki, ninaweza hata kuifanyia Uwanja wa Taifa,” aliongeza. “Unajua nilishindwa kufanya mambo haya haraka kwa sababu wengi nadhani wangeamini kwamba ninafanya hivyo ili kutafuta umaarufu zaidi, tunataka tufanye kiusahihi yasije tokea mambo kama ya Instagram tunataka tuje kuwa mfano wa kuigwa.” Alipoulizwa tarehe ya ndoa hiyo Diamond