Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amezungumzia kasi aliyoanza nayo rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli pamoja na baraza lake la mawaziri. Akizungumza jana na mwandishi wa habari wa Azam TV, Mbowe alisema kuwa rais Magufuli ameanza vizuri kiutendaji na kwamba ameanza kuzifanyia kazi hoja zilizokuwa zikihubiriwa na Chadema ndani na nje ya Bunge. “Hoja ya kubana matumizi ya serikali, hoja ya kupunguza sherehe za kitaifa, hoja ya kupunguza safari za nchi za nje kwa viongozi wetu, hoja ya kupunguza watumishi wa umma ambao hawana umuhimu, hoja ya kuwa na serikali ndogo. Haya mambo tulizungumza siku zote na hawa hawa wa Chama cha Mapinduzi ndio waliokuwa wanayapinga haya,” alisema Mbowe. Mbowe alieleza kuwa dhana ya upinzani sio kupinga kila kitu kinachofanywa na serikali hivyo chama chake hakitakuwa tayari kupinga mambo mema yanayofanywa na serikali ya awamu ya tano kama baadhi ya watu wanavyotarajia, bali kitajikita katika kujadili na kuibua hoja za