Skip to main content

Posts

Showing posts from January 26, 2014

HIVI NDIVYO MSANII BONGO MOVIES ALIVYOJINYONGA

Stori: MUSA MATEJA na Imelda Mtema SAKATA la kujinyonga kwa msanii wa filamu Bongo, Victor Peter limegubikwa na matukio tofauti ya kustaajabisha ambayo marehemu aliyafanya siku kadhaa kabla hajapatwa na umauti, Ijumaa limefukunyua kila kitu. Mwili wa marehemu Victor Peter ukipelekwa mochwari. Kwa mujibu wa rafiki wa marehemu, Hamisi Koba, msanii huyo alijinyonga usiku wa Februari 27, mwaka huu mkoani Tanga ambapo marehemu alifika jijini humo kuigiza filamu yake iitwayo Our Family. Hamisi alisema Victor aliwasili jijini humo akiwa na timu ya wasanii sita na kufikia kwenye nyumba ya kulala wageni iitwayo Safari Junior iliyopo maeneo ya Kisosora ambapo punde walianza kushuti filamu hiyo ambayo yeye na Mzee Jengua ndiyo walikuwa wahusika wakuu. Marehemu Victor Peter enzi za uhai wake. “Mimi ndiye nilikuwa kama mwenyeji wake mkubwa hapa Tanga, alikuwa ni mpole na siku zote tulipokuwa kazini kwa ajili ya kushuti filamu hiyo aliniambia mambo mengi kuonesha amejipanga kuhakikisha

Huyu ndiye BABU ALIYENASWA NA DENTI GESTI LAIVU!

Stori: WAANDISHI WETU YELEUUUWI! Ile tabia ya wazee ya kupenda dogodogo imemtokea puani mzee aliyetajwa kwa jina moja la mzee Omari, ni Ijumaa pekee lenye ubavu wa kuripoti sinema hiyo ya bure. AIBU YA MWAKA:  Babu akifunika uso wake baada ya kunaswa na denti gesti. Mzee huyo alinaswa laivu akiwa gesti na denti wa shule moja ya sekondari jijini Dar (jina la denti na shule vinahifadhiwa kimaadili). Tukio hilo la aibu lilijiri juzikati kwenye gesti moja iliyopo maeneo ya Kawe, Dar na kusababisha timbwili zito. TAARIFA MEZANI KWA OFM Hivi karibuni, kikosi maalum cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) chini ya Global Publishers, kilipokea lalamiko kutoka kwa mzazi wa denti huyo ambaye alieleza juu ya mabadiliko ya mwanaye kitabia na kushuka kitaaluma kutokana na kusumbuliwa na ‘mbaba’ huyo. Mzazi huyo aliiambia OFM kuwa amekuwa akifuma mawasiliano ya kwenye simu ya mkononi ya mwanaye na mwanaume huyo ambaye alikuwa hamfahamu. FUNDISHO KWA WAZEE:  Babu akijiandaa kuvaa nguo yake ya

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AAGANA NA WAZIRI MKUU WA FINLAND BAADA YA KUMALIZA ZIARA YAKE NCHINI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Waziri Mkuu wa Finland, Jyrki Katainen, wakati alipokuwa akiagana naye kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam. Waziri huyo ameondoka jana usiku kurejea nchini kwao baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini. Picha na OMR Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Waziri Mkuu wa Finland, Jyrki Katainen, wakati alipokuwa akiagana naye kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam. Waziri huyo ameondoka jana usiku kurejea nchini kwao baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini. Kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo. Picha na OMR Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Waziri Mkuu wa Finland, Jyrki Katainen, wakati alipokuwa akimsindikiza na kuagana naye kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyer

PINDA AZINDUA RASMI MAPITIO YA MFUMO WA UWEKEZAJI TANZANIA

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi zitakazonufaika katika masuala ya uwekezaji nchini endapo itatekeleza kikamilifu Mapitio ya Mfumo wa Uwekezaji yaliyowasilishwa na  Taasisi ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD) . Ametoa kauli hiyo leo mchana  (Ijumaa, Januari 31, 2014), wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ku zindua kitabu cha  Mapitio ya Mfumo wa Uwekezaji kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Akizungumza katika uzinduzi huo, Waziri Mkuu Pinda  alisema kuwa malengo ya mapitio ya  mfumo huo ni kuboresha hali ya uwekezaji na biashara nchini ambayo matokeo yake yatasaidia kuongeza wawekezaji katika maeneo mengi.   “Kuna maeneo ya uwekezaji yanayopata uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje ya nchi (Foreign Direct Investment -FDI) ambayo ni umeme, mafuta, gesi, madini, viwanda, ujenzi na huduma za jamii.   Amesema kuwa matokeo ya jitihada hizi ni makubwa na yameonekana ndani ya miaka mi

HUYU NDIYE MCHUNGAJI WA TANZANIA ANAYELINDWA KAMA RAIS

Maisha ya Askofu wa Huduma ya Ngurumo ya Upako, Geor Davie anayevuma zaidi jijini Arusha na Dar es Salaam ni ya kifahari, anaabudiwa zaidi ya manabii na analindwa kuliko marais mbalimbali duniani. Davie ambaye hujulikana zaidi kwa jina la Mtume, ana msafara mrefu kwenye ziara zake anazokwenda kutoa huduma ambao husheheni magari mengi ya kifahari kuliko marais wengi. OneloveTz tuna mlolongo wa matukio ya Davie ambayo yanajieleza kwa picha ambazo zinabainisha namna mtumishi huyo wa Mungu anavyokula bata. MSAFARA WA SHS. MIL. 200 Matukio yanaonesha kuwa, baadhi ya misafara ya Davie imekuwa na msururu mrefu wa magari ambayo hayapungui kumi. Uchunguzi umeonesha kuwa, magari hayo, kila moja linanunuliwa kati ya shilingi milioni 20 na 40, hivyo thamani ya ‘mikoko’ peke yake inaleta wastani wa jumla ya zaidi ya shilingi milioni 200 bila ya mafuta ambayo nayo hugharimu fedha nyingi. ULINZI DAH! Kila sehemu ambayo Davie hufika kwa lengo la kutoa huduma, huzungukwa na walinzi kat

HIVI NDIVYO MSANII MAARUFU WA KUNDI LA FUTUI ALIVYOZIKWA

Mwigizaji wa filamu Swahilihood Marehemu Majuto Omary enzi za Uhai wake. MAMIA ya wakazi wa jiji la Mwanza wamejitokeza kumzika mwigizaji na mchekeshaji nyota kutoka kundi la Futuhi Mzee Majuto Omari ‘ DUDE ‘ msanii huyo amefariki Leo SAA kumi na moja na kuzikwa leo hii huko jijini Mwanza. Wadau wa sanaa wakiombea dua mwili wa Mzee Omary Dude Mzee dude Watu wakimzika msanii huyo Maandalizi ya kaburi la Mzee Dude Enzi za uhai wake Mzee Omary Ndugu na jamaa marafiki na wapenzi wa kundi la Futuhi walijitokeza kumzika msanii huyo nyota, ambaye alijizolea umaarufu kupitia kipindi cha vichekesho maarufu kama Futuhi kinachorusha vichekesho vyake kupitia kituo cha Televisheni cha Star tv cha jijini Mwanza, FC tunatoa Pole kwa wafiwa wote. MUNGU AIWEKE ROHO YAKE MAHALA PEMA PEPONI ‘ AMEN. CREDIT : SWAHILI HOOD

HII NDIYO MAANA YA MSTARI WA "ZITTO AKILOGA KASULU SISI TUNAMLOGEA PANGANI" SOMA ALICHOFUNGUKA ROMA HAPA

  Mara nyingi mistari mingi katika nyimbo za HipHop humfanya msikilizaji atumie akili nyingi sana ili kuelewa msanii alimaanisha nini katika wimbo huo. Mfano mzuri wa wasanii ambao ukisikiliza nyimbo zao kuna baadhi ya mistari lazma ufikiri sana hadi uje uielewe ni Roma Mkatoliki. Mfano wa mstari ambao uliwatoa jasho wengi ni "ZITTO AKILOGA KASULU SISI TUNAMLOGEA PANGANI"   Kupitia website yake Roma Mkatoliki ameelezea maana ya mstari huo kwani wengi walikua wakiutafsiri kwa maana tofauti kabisa. Na hiki ndo alichokisema Roma.   BANDARI CHANUU!! RAILWAY CHALII!! MAKAMBA IINUE KATANI/ ZITTO AKILOGA KASULU SISI TUNAMLOGEA PANGANI/   Meanz- Miaka ya nyuma jiji letu la tanga lilikuwa ni miongoni mwa sehemu/mkoa ambao tanzania inajivunia kwa kujipatia pato kubwa kutokana na kilimo cha zao la katani!!   Ulikuwa ni mkoa ambao upo katika maendeleo na utajiri mkubwa kutokana na  BANDARI NA RILWAY!!   W

Hizi ndizo Sababu za Man Utd kumuuza Rooney

  MANCHESTER, ENGLAND MREMBO Coleen Rooney anasubiri kwa hamu kubwa mazungumzo ya mkataba mpya wa mumewe, Wayne Rooney wa kuendelea kubaki klabu Manchester United. Taarifa zinabainisha kwamba mchezaji huyo anaandaliwa mshahara wa pauni 300,000 kwa wiki. Mrembo huyo anadaiwa kumtaka mumewe asaini mkataba mwingine wa miaka mitano wa kubaki Manchester ili kuwasubiri watoto wao; Kai, 4, na Klay mwenye umri wa miezi minane kuwa na umri mkubwa kabla ya kuhama. Mkataba ambao Manchester United inataka kumpa Rooney una thamani ya pauni 65 milioni na utamfanya straika huyo kuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi England. Kwa sasa analipwa kiwango sawa na mchezaji mwenzake wa Manchester United, straika wa Kidachi, Robin van Persie, pauni 250,000 kwa wiki. Rafiki wa mrembo Coleen, 27, anasema: “Kitu kikubwa Coleen hataki wahame kutoka Kaskazini Magharibi na jambo hilo ni muhimu sana kwa Wayne. Hataki kuondoka eneo hilo na kutokana na kupokea ofa nzuri ya pesa nyingi

Hichi ndicho choo cha Birdman aliyonyesha kilichotengenezwa na dhahabu, kinakadiriwa kuwa na thamani ya $1mil.

Birdman boss wa record label ya YMCMB ambaye mara nyingi huwa anajisifia kwa matumizi yake makubwa ya pesa kwenye vitu luxury, ameendeleza hivyo vitendo  vya kufanya matumizi makubwa ya pesa. Hivi karibuni ame-share picha ya choo chake ambacho kime-kuwa covered na material ya dhahabu pande zote. Mfuniko wake na sehemu ya juu ya choo hicho ni dhahabu tupu na sehemu nyingine yote hautaweza kukiona hicho choo kwasababu kimefunikwa na dhahabu. Gharama yake inakadiriwa ni dola millioni moja.

Magazeti ya leo January 28 2014 na stori za Udaku, Michezo na Hardnews

. Kila siku hapa millardayo.com huwa naweka magazeti ya siku husika, kuanzia udaku michezo na hardnews nikiamini kwamba wakati mwingine unaweza kuwa mbali na yanakopatikana au yakawa yanachelewa kukufikia asubuhi. Lengo la millardayo.com ni kuhakikisha kila Mtanzania anaweza kusoma stori kubwa za Magazeti kabla ya saa mbili kamili asubuhi ambapo kwa mwaka 2014 lengo ni kuhakikisha Magazeti yanakuepo hapa millardayo.com hata kabla ya saa moja asubuhi. Unaweza kujiunga na familia ya Millard Ayo kwenye facebook, twitter na instagram kwa jina la Millard Ayo ili kuwa karibu zaidi ya habari zote zinazowekwa hapa ambazo huwa link zinawekwa kwenye mitandao hii ya kijamii muda mfupi tu baada ya habari kupandishwa hapa. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .