Skip to main content

Posts

Showing posts from November 17, 2013

HUYU NDIYO MNYAMA WA AJABU NA ILISADIKIKA KWAMBA HUWENDA AKAVUNJA REKODI YA UMBO KUBWA KULIKO WANYAMA WOTE DUNIANI.

MNYAMA huyu wa maajabu mkubwa kupita kiasi alionekana huko Vietnam mwaka 2013. Ni nooooma...!!!

KAMANDA WA POLISI AHUSISHWA NA TUKIO LA MAUAJI

Anayedaiwa kuwa mpenzi wa marehemu, Christina. Mauaji hayo yalitokea juzi nje ya nyumba ya wanafamilia waliokumbwa na dhahama hiyo iliyopo Ilala jijini Dar es Salaam. Katika mauaji hayo, Gabriel alidaiwa kumuua kwa risasi shemejiye aliyejulikana kwa jina la Alfa Nando, kumjeruhi mchumba wake, Christina Nando, mama mkwe wake (mama wa Christina), dereva wa familia aitwaye Francis kisha kujimaliza mwenyewe. Akizungumza na Amani kwa njia ya simu rafiki mmoja wa marehemu Gabriel (jina lipo) alisema marehemu ambaye alikuwa mfanyabiashara wa magari jijini Mwanza aliaga kwenda Dar kumchunguza mchumba wake (Christina) kwa sababu alidokezwa kuwa shemeji yao huyo anamsaliti kwa kutembea na RPC ambaye jina lake halikupatikana. Alidai kuwa, baada ya kufika Dar marehemu alimpigia simu na kumwambia kuwa, habari za Christina kutembea na RPC huyo ni za kweli na kwamba amepata habari anataka kusafiri hivyo hatakubali aende hiyo safari bila kumfanyia kitu kibaya.

DENTI WA KAPUYA AZUA JIPYA

Na Waandishi Wetu Global Publishers Ltd ilipoamua kufuatilia sakata la denti anayedai kubakwa na Mbunge wa Urambo Magharibi (CCM), Juma Athuman Kapuya, lilijua yapo mengi yatajitokeza, Amani lina jipya lingine. Denti akiwasikiliza wana GPL wakati wa mahojiano                                        Mbunge wa Urambo Magharibi (CCM), Profesa Juma Athuman Kapuya. Huu ni muendelezo wa utekelezaji wa ahadi ya Global, iliyotoa Jumamosi iliyopita kwenye Gazeti la Risasi kwamba waandishi wake watafuatilia kisha magazeti yake yataandika kila kitu. Katika Ijumaa Wikienda, Kapuya alifunguka, Uwazi liliandika utapeli mzima wa denti husika. Amani linalo jipya la denti huyo tapeli, Halima Hamad au Felista, aliyeamua kufunguka mbele ya waandishi wetu kwamba ni kweli yeye ni mama wa mtoto mmoja. Denti akiwasikiliza wana GPL wakati wa mahojiano. Kuhusu kubakwa, Felista ambaye pia hutumia majina ya Leylat au Leila, alisema: “Kapuya hakunibaka i

Hofu yatanda Kamati Kuu Chadema

  Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe (katikati) akiwa na walinzi wake akiwasili katika Jengo la Ubungo Plaza, Dar es Salaam, jana kushiriki kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho. Picha na Michael Jams Dar es Salaam. Hali ya wasiwasi iligubika eneo  kinapofanyika kikao cha Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kilichoanza Dar es Salaam jana. Ulinzi mkali wa walinzi wa Chadema (Blue Guard), uliimarishwa katika ukumbi wa Ubungo Plaza kinapofanyika kikao hicho ambacho kinatarajiwa kumalizika leo, huku kukiwa na maagizo yaliyoashiria kuwapo kwa mambo mazito. Maazimio ya kikao hicho yanasubiriwa kwa hamu na wafuatiliaji wa mambo ya siasa nchini kwani kinafanyika katika kipindi ambacho chama hicho kikuu cha upinzani nchini kinapita katika misukosuko na hasa ya malumbano baina ya makamanda wake wa juu. Maelekezo ya ulinzi Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliwasili ukumbini hapo saa 5.20 asubuhi na baada ya kuingia, wapiga picha

HII NDO SABABU INAYOKUSABABISHA UPIGE MIAYO

Kwa kawaida upigaji wa miayo huashiria kuchoka kwa mwili, akili au kujisikia kuchoshwa na jambo au hali fulani. Hali hii hutokea bila kutarajia wala haiepukiki, kama ilivyo kuhema. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa kuhusu miayo, binadamu huanza kupiga miayo tangu akiwa tumboni na umri wa wiki 11! Kuna maelezo mengi tofauti kuhusu suala la kupiga miayo, lakini yanayovutia zaidi ni yale yanayofanywa na mtafiti wa Chuo Kikuu cha Princeton Marekani ambaye amegundua kuwa kitendo cha kupiga miayo huwa kinafanya kazi muhimu sana ya kuupoza ubongo. Utafiti huo unasheheresha kwa kusema kuwa miayo huwa sawa na ‘reguleta’ ya kurekebisha joto la ubongo, pale joto linapokuwa limezidi kwenye ubongo kutokana na sababu mbalimbali, miayo hutokea kuupoza. Imeelezwa kuwa watu wengi hupiga miayo wakati wa kipindi cha baridi kuliko kipindi cha joto kwa sababu kipindi cha baridi ubongo huchemka na kitendo cha kupiga miayo huwa kinatokana na mahitaji ya mwili ya kiasili ya kurekebisha hali ya j

MABONDIA KUSHUSHIA NDONGA KESHO MORO

Na Daudi Julian, Morogoro MAPAMBANO zaidi ya sita ya ngumi za kulipwa yanatarajiwa kufanyika Ijumaa, wiki hii, katika ukumbi wa Yohana Pub ulioko maeneo ya Msamvu, katika Manispaa ya Morogoro. Akizungumza na mtandao huu, msemaji wa mapambano hayo ambayo awali yalipangwa kufanyika Novemba 24 kabla ya kurudishwa nyuma, Mohamed Jeilan alisema maandalizi yanakwenda vizuri na kwamba mabondia wote watakaopanda ulingoni wapo katika mazoezi makali. Jeilan alisema lengo la mapambano hayo yanayosubiriwa kwa hamu kubwa mjini Morogoro, ni kuibua vipaji vya mabondia chipukizi na kuendeleza mchezo huo kiujumla. Alisema mbali ya mabondia wa Morogoro, mabondia wachache kutoka jijini Dar es Salaam pia wanatarajiwa kualikwa kwa lengo la kutoa changamoto katika mapambano hayo. “Kimsingi maandalizi yanakwenda vizuri na mabondia wote hivi sasa wanaendelea kujinoa chini ya makocha wao ili kuhakikisha wanafanya vizuri siku hiyo”, alisema. Msemaji huyo amewataja baadhi ya mabo

ziara ya Naibu Waziri wa Uchukuzi katika madaraja ya Bahi-Kintinku

Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba (wa tatu kutoka kulia), akiongea na fundi ambaye anafanya shughuli za ujenzi katika Daraja la Reli la Bahi-Kintinku. Dk. Charles Tizeba amefanya ziara kwenye daraja  hilo na kupata taaarifa kuwa limekamilika kwa asilimia 98.  Aidha daraja hilo limegharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 3.5. Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba (wa pili kutoka mbele), akishuka chini ya daraja la bahi-kintinku kuangalia maendeleo ya ujenzi wake. Daraja hilo linajengwa na Kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC). Kukamilika kwa daraja hilo kutasababisha Treni za abiria na mizigo kupita kwa uhakika majira yote ya mwaka. Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba, akitoa maelekezo kwa Mhandisi Mkazi wa mradi  kutoka kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC), Bw. Wang Chao(aliyevaa fulana ya rangi ya karoti), wakati alipotembelea mradi huo mapema wiki hii. Ujenz

23 KUIWAKILISHA BARA KOMBE LA CHALENJI, MECHI DHIDI YA STARS, ZIMBABWE YAINGIZA MIL 50/

Kocha Mkuu wa Kilimanjaro Stars, Kim Poulsen ametaja kikosi cha wachezaji 23 watakaoshiriki michuano ya Kombe la Chalenji inayofanyika nchini Kenya kuanzia Novemba 27 mwaka huu. Kilimanjaro Stars iliyotwaa kombe hilo mara ya mwisho mwaka 2010 chini ya Kocha Jan Poulsen, na ambayo imepangwa kundi B katika michuano ya mwaka huu itacheza mechi yake ya kwanza Novemba 28 mwaka dhidi ya Zambia kwenye Uwanja wa Machakos. Wachezaji wanaounda kikosi hicho cha Tanzania Bara ni makipa Deogratius Munishi (Yanga), Ivo Mapunda (Gor Mahia, Kenya) na Aishi Manula (Azam). Mabeki ni Erasto Nyoni (Azam), Himid Mao (Azam), Ismail Gambo (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Michael Pius (Ruvu Shooting) na Said Moradi (Azam). Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Ramadhan Singano (Simba) na Salum Abubakar (Azam). Safu ya ushambuliaji inaundwa na Elias Maguli (Ruvu Shooting), Faridi M

ABDULRAHMAN KINANA NA UJUMBE WAKE WAINGIA MBAMBA BAY WALAYA YA NYASA

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abd ulrahman Kinana akishiriki kazi za mikono wakati akifa nya kazi ya kusomba matofali pamoja na wananchi wa kata ya Luhangarasi wakati alipokagua ujenzi wa ofisi hiyo Kata Wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma leo, Kinana pia aehutubia mikutano mbalimbali ya hadhara na kuwatembelea mwenyeviti wa mashina katika kuimarisha uhai wa chama, Katika ziara hiyo Kinana ameambatana na Dr,Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kiamtaifa na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi. kesho ataendelea na ziara yake ya kikazi huko Lituhi baada ya kufanya mkutano wa had dhara kwenye uwanja wa mpira wa Mbamba Bay leo jioni.(PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-MBAMBA BAY- NYASA) Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abd ulrahman Kinana akifungua ofisi ya chama cha mapinduzi wilaya ya Nyasa mjini Mbamba Bay leo kushoto ni Mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi Mh.Kapteni John Komba Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abd ulrahman Kinana akiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Mbinga