Skip to main content

Posts

Showing posts from March 10, 2013

LYRICS YA DIOMOND FEAT NEY WA MITEGO HII HAPA

LYRICS: MUZIKI GANI / NEY WAMITEGO FEAT DIAMOND SONG: MUZIKI GANI ARTIST: NEY WAMITEGO FEAT DIAMOND PRODUCER: MR T TOUCH CHORUS STUDIO: SEDUCTIVE RECORDS Hivi nyi ma mc mnachoimba kitu gani, mara bangi mara matusi sa ndo muziki gani (diamond). Hii no hip-hop h.o.p muasisi wa burudani, tushachoshwa kutwa mapenzi, kabane Pua nyumbani (ney) X2 DIAMOND Hata bibi yangu mi aliniambia , mwanamke anahitaji kubembelezwa Kupetipeti matunzo pia, ukienda rafu utampoteza, Muziki ni mfano wa binti muzuri, Na ndio maana namtunza kwa vazi na uturi NEY WA MITEG Aaah piga kimya, we ndo haufai kabisa hauna maana Wabana pua kila siku mnarogana, bibi yako alikuambia muziki ni kama binti Mbona unawachezea unawatema kama big g Mara wema, mara Jo keti, mara Naj, mara Penny, je mnafanya mziki mpate mabinti DIAMOND Uuuhhuuuu, hata wazee wazamani, walishasemaga kazi na dawa Chamuhimu jukwaani, ni kuhakikisha wanapagawa, Kwa michezo ya kuringa ringa ndo huwa wan

Kamati za Bunge zaanza kucharuka! bofya hapa kwa habari zaidiiiiiii

Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), Deo Filikunjombe aliliambia Mwananchi kuwa kwa sasa atakachoweza kusema ni kwamba anawatumia salamu Makatibu Wakuu na Wakurugenzi wa mashirika ya Umma ambao hesabu zao haziko vizuri.

PAPA FRANCIS AKATAA VIATU VYA KIFAHARI KWA HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Siku chache baada ya kuchaguliwa kuwa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amewashangaza wengi mengi kwa kukataa kuvaa viatu vya kifahari na msimamo wake kuwekwa wazi kuwa hatavumilia makasisi watakaotenda uovu. Tayari, Papa Francis ameelezwa kuwa kiongozi asiyetaka makuu, mhafidhina na mtu ambaye hataweza kubadili mengi katika kanisa hilo lenye waumini bilioni 1.2 duniani. Katika siku mbili za uongozi wake, Papa Francis amelithibitisha hilo kwa kutokea hadharani akiwa amevaa viatu rahisi, vyeusi na kuachana na vyekundu vya kifahari vilivyopendelewa na mtangulizi wake, Benedict VXI.

UONGOZI SIMBA WAKANUSHA KUWEPO KWA MKUTANO MKUU KESHO

OFFICIAL: UONGOZI SIMBA WAKANUSHA KUWEPO KWA MKUTANO MKUU KESHO TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Ndugu wana habari, KUMEKUWAPO na taarifa za kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Simba uliopangwa kufanyika Kesho (Machi 17, 2013) jijini Dar es Salaam kujadili mustakabali wa klabu. Ikumbukwe kwamba Mkutano Mkuu wa Wanachama ndiyo chombo cha juu kabisa cha maamuzi kwa klabu yetu. Katiba ya Simba SC imeupa Mkutano Mkuu hadhi ya juu mno na ndiyo maana imeweka utaratibu wa kufanyika kwake. Miongoni mwa utaratibu ni kwamba ni lazima uitishwe na Mwenyekiti aliye madarakani wa klabu. Kwa kushirikiana na Kamati ya Utendaji, ndiye atakayepanga ajenda, mahali na wakati wa kufanyika kwa mkutano wenyewe. Katika miaka ya nyuma, zilikuwepo nyakati ambapo klabu ilikaa hadi miaka mitatu pasipo kuitishwa kwa Mkutano Mkuu wowote wa wanachama. Hakuna mwanachama au kikundi chochote kilichojitokeza kudai mkutano wa dharura wakati huo ingawa ilik

KALA GEREMAYA AIBUKA NA KUZUNGUMZIA JUU YA VIDEO YA NGOMA YAKE MPYA YA KARIBU DARAMBAYO ANAIACHIA KESHO BOFYA HAPA UJUE KASEMA NINI

BROTHERMAN ANATEMBEA TOKA KEKO KWA MIGUU ANAKWENDA MLIMAN CITY KUNUNUA MKATE TU hahahahaha HII NI BAADHI YA MISTARI INAYOPATIKANA KWENYE KARIBU DAR NGOMA YANGU MPYAAA UKIITAKA NENDA GOOGLE ANDIKA kala jeremiah ft ben pol karibu dar mp3 UTAIPATA BUREEEEE. YEEEEEEES KAZI NDO KWANZA INAANZA NAWASHUKURU WOOTE WANAOENDA SAWA NA MIMI MUNGU AWABARIKI SANA KESHO WALE AMBAO HAMNA VING'AMUZI MTAKIONA KIDEO HAPA HAPA KUPITIA PAGE HIII PA MOJA SANA

polisi mjini nairobi watumia nguvu kuwatawanya mamia ya wafuasi wa Raila Odinga! habari zaiidi bofya hapaaa!

                                                                                                    Polisi mjini Nairobi, Kenya, wamefyatua moshi wa kutoa machozi kuwatawanya mamia ya wafuasi wa Waziri Mkuu Raila Odinga, nje ya mahakama makuu . Mawakili wa Bwana Odinga waliwasilisha kesi mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa mapema mwezi huu, ambapo Bwana Odinga alishindwa kwa kura elfu chache na Bwana Uhuru Kenyatta. Hapo awali Bwana Odinga aliwasihi wafuasi wake wasijihusishe na vurugu. Mawakili wa Bwana Odinga wamekwenda mahakamani wakidai kuwa kumepita udanganyifu kwenye uchaguzi