Skip to main content

Posts

Showing posts from December 8, 2013

Hawa ndio Watu watatu wanazuiliwa na polisi nchini Uingereza baada ya kupanga matokeo

Sam Sodje alikuwa mchezaji wa timu ya kitaifa ya Nigeria Sam Sodje alirekodiwa kwenye kanda ya video na mwandishi wa habari mmoja wa jarida la Sun akizungumzia alivyompiga mchezaji wa timu hasimu usoni katika ligi ya daraja la kwanza, ili apate kadi nyekundu na kisha baadaye alipwe pauni 70,000. Alisema pia alipangia mchezaji mwingine aweze kulipwa pauni 30,000 kwa kupokea kadi ya manjano katika mechi ya ligi. Klabu ya Portsmouth imeelezea kushtushwa sana na madai hayo. Katika Kanda hiyo liyorekodiwa kisiri, bwana Sodje raia wa Nigeria, pia alidai ana uwezo wa kupanga mechi za ligi kuu na kuwa yuko tayari kupanga mechi katika kombe la dunia mwaka ujao. Katika taarifa kwa vyombo vya habari, msemaji wa klabu hiyo, alisema kuwa ikiwa madai haya ni ya kweli, basi ijulikane kuwa ni ya kushtua na kushangaza sana , jambo la kupanga mechi bila shaka linaathiri pakubwa maadili ya mchezo wa soka. Sodje hachezei tena klabu ya Portsmouth lakini itambidi ashirikiane na maa

MECHI YA KILIMANJARO STARS KUPIGWA MACHAKOS!!

Mechi ya kwanza ya nusu fainali ya michuano ya mwaka huu ya Kombe la Chalenji kati ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) na wenyeji Kenya (Harambee Stars) itapigwa Uwanja wa Machakos. Kwa mujibu wa ofisa wa CECAFA, Amir Hassan mechi hiyo itachezwa Uwanja wa Machakos ulioko takribani kilometa 64 kutoka jijini Nairobi. Mechi hiyo itachezwa Jumanne (Desemba 10 mwaka huu) kuanzia saa 10 kamili jioni na itaoneshwa moja kwa moja  na kituo cha televisheni cha SuperSport kupitia chaneli ya SS9. Kilimanjaro Stars imetinga hatua hiyo baada ya kuivua ubingwa Uganda (The Cranes) kwa mikwaju 3-2 ya penalti katika mechi ya robo fainali ya michuano hiyo iliyochezwa jana Uwanja wa Aga Khan katika Jiji la Mombasa. Hadi dakika 90 za kawaida zinamalizika timu hizo zilikuwa zimefungana mabao 2-2. Mabao ya Kilimanjaro Stars yalifungwa na Mrisho Ngasa wakati katika mikwaju ya penalti walofumania nyavu ni Amri Kiemba, Athuman Idd na nahodha Kelvin Yondani. Boniface Wambura Mgoyo Kaim

Kampeni ya Nani Mtani Jembe yatikisa Ukonga Banana Dar es salaam, mashabiki wala raha kubwa mno!!

Mtoa huduma katika Kampeni ya Nani Mtani Jembe (kushoto), akizungumza na Mteja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager wakati wa tamasha lililofanyika Ukonga Banana Dar es Salaam leo kwaajili ya Mashabiki wa timu ya Simba na Yanga. Wacheza shoo wa kundi la muziki wa Dansi la Extra Bongo wakitoa burudani katika Tamasha la Kampeni ya Nani Mtani Jembe lililofanyika Banana Dar es Salaam leo kwaajili ya Mashabiki wa Simba na Yanga na kuendeshwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager Bonge la Kiburudisho kwa Watanzania. Mpiga gataa wa bendi  ya muziki wa dansi wa kundi la Extra Bongo (kushoto), akicheza na Shabiki wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager inayoendesha Kampeni  ya  Nani Mtani Jembe ilifanyika Banana Dar es Salaam leo kwaajili ya Mashabiki wa timu ya Simba na Yanga Kiongozi wa Bendi ya Extra Bongo Ally Choki (kushoto) akicheza  muziki  pamoja na wacheza shoo wake wakati wa Tamasha la Nani Mtani Jembe lilifanyika Banana Dar es Saam leo tamasha hilo ni kwaajili ya Mashab

Hii ndio kauli ya Irene uwoya ya kufunga mwaka huu wa 2013. Inakuhusu na wewe

  “Napenda kuchukua nafasii hiii kuomba samahan kwa wote nilio wakosea...napia mim nimewasamehe...nataka nimaliza mwaka kwa amani na upendo...nawapenda wote sina kinyongo na mtu...asante mwenyez mungu kwakunipa nguvu…”