Skip to main content

Posts

Showing posts from August 11, 2013
MADRID, HISPANIA KUNA madai mengi ya msingi yamejitokeza kuhusu uhusiano baina ya staa wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo na kocha wa zamani wa timu hiyo, Jose Mourinho, ulivyokufa. Wote ni raia wa Ureno. Hata hivyo, vielelezo vya msingi vinapatikana zaidi wakati huu ambapo wawili hao wameachana njia huku Mourinho akirudi Stamford Bridge na Ronaldo akibakia Real Madrid. Hivi ndivyo............

Urafiki wa Cristiano Ronaldo, Mourinho ulivyofikia tamati

MADRID, HISPANIA KUNA madai mengi ya msingi yamejitokeza kuhusu uhusiano baina ya staa wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo na kocha wa zamani wa timu hiyo, Jose Mourinho, ulivyokufa. Wote ni raia wa Ureno. Hata hivyo, vielelezo vya msingi vinapatikana zaidi wakati huu ambapo wawili hao wameachana njia huku Mourinho akirudi Stamford Bridge na Ronaldo akibakia Real Madrid. Hivi ndivyo uhusiano wao ulivyokufa. Ronaldo akwepa kumkumbatia Ronaldo alifunga mabao yote matatu wakati Madrid ikiizamisha..........

Ponda adaiwa kujeruhiwa kwa risasi

  Morogoro. Hali ya wasiwasi imetanda mjini Morogoro baada ya Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda, kudaiwa kupigwa risasi begani wakati polisi wakiwa katika harakati ya kumkamata. Habari kutoka katika eneo hilo zinadai kuwa Ponda alipigwa risasi saa 12:25 jioni, wakati akisindikizwa na wafuasi wake kuelekea katika Msikiti wa Mungu Mmoja Dini Moja, baada ya kumaliza kutoa mhadhara katika kongamano lilifanyika mjini Morogoro jana. Tukio hilo lilitokea katika Barabara ya Tumbaku, baada ya kumalizika kwa mkutano wa kongamano lililoandaliwa na Jumuiya ya Wahadhiri wa Kiislamu Mkoa wa Morogoro. Mwenyekiti wa Kongamano hilo, Sheikh Idd Mussa Msema aliliambia Mwananchi Jumapili jana kuwa Ponda alipigwa risasi sehemu ya bega, na askari polisi na kwamba aliwahishwa kutibiwa katika Hospitali ya Kiislamu iliyopo eneo Msamvu mjini Morogoro. Hata hivyo, wakati Sheikh huyo akisema hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, F