Skip to main content

Ponda adaiwa kujeruhiwa kwa risasi




 


Morogoro. Hali ya wasiwasi imetanda mjini Morogoro baada ya Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda, kudaiwa kupigwa risasi begani wakati polisi wakiwa katika harakati ya kumkamata.


Habari kutoka katika eneo hilo zinadai kuwa Ponda alipigwa risasi saa 12:25 jioni, wakati akisindikizwa na wafuasi wake kuelekea katika Msikiti wa Mungu Mmoja Dini Moja, baada ya kumaliza kutoa mhadhara katika kongamano lilifanyika mjini Morogoro jana.
Tukio hilo lilitokea katika Barabara ya Tumbaku, baada ya kumalizika kwa mkutano wa kongamano lililoandaliwa na Jumuiya ya Wahadhiri wa Kiislamu Mkoa wa Morogoro.
Mwenyekiti wa Kongamano hilo, Sheikh Idd Mussa Msema aliliambia Mwananchi Jumapili jana kuwa Ponda alipigwa risasi sehemu ya bega, na askari polisi na kwamba aliwahishwa kutibiwa katika Hospitali ya Kiislamu iliyopo eneo Msamvu mjini Morogoro.
Hata hivyo, wakati Sheikh huyo akisema hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile alikanusha madai ya kuwa polisi wamempiga risasi.
Alisema polisi walifika katika eneo hilo kwa ajili ya kumkamata Ponda, baada ya kumaliza mhadhara wake na kwamba wakati wakitaka kumkamata ndipo wafuasi wake wakawazuia polisi na kulazimika kupiga mabomu ya machozi na risasi hewani kuwatawanya.
Katika tukio hilo inadaiwa kuwa Sheikh Ponda aliyekuwa katika gari ndogo huku wafuasi wake wakimsindikiza kwa miguu, walipofika eneo la gereji mabomu ya machozi yalipigwa na polisi waliokuwa katika magari aina ya defender wakati wakijaribu kuwatawanya wafuasi hao.
Baada ya tukio hilo baadhi ya wafuasi wake walimchukua Sheikh Ponda kutoka katika gari lake na kumkimbizia katika gereji moja, kisha wakatoka wakiwa wamempakia katika pikipiki na kumpeleka katika Hospitali ya Rufaa ya Morogoro.
Mlinzi mmoja wa lango namba moja alisema kuwa ulifika msululu wa pikipiki zaidi ya 50, lakini pikipiki zote zilizuiliwa isipokuwa iliyokuwa imembeba Sheikh Ponda na kwenda naye mpaka mapokezi.
Aidha, alisema wakiwa katika eneo hilo magari kadhaa ya polisi yaliingia katika lango la hospitali hiyo. Hivyo wafuasi wa Sheikh Ponda wakalazimika kumbeba begani na kutoroka naye kupitia lango namba mbili.
Taarifa zilizopatikana baadaye zinadaiwa kuwa Sheikh Ponda alikimbizwa katika Hospitali ya Kiislamu ya Msamvu.
Baadhi ya watu walidai kumwona Sheikh Ponda akiingizwa katika Hospitali ya Rufaa Morogoro, lakini walishangaa alivyotoweka.

Comments

Popular posts from this blog

VIDEO YA NGONO YA WANAOSADIKIKA KUWA NI WANAFUNZI WA IFM YAVUJA

Watu wawili wanaosadikika ni wanachuo wa IFM wajirecord video wakifanya ngono ndani ya........... chumba ambacho kinaonesha kama ni cha hosteli, fungua na uone upuuzi uliofanyika humu ndani…. KUANGALIA VIDEO HII LAZIMA UWE NA UMRI WA ZAIDI YA MIAKA 18+ KUANGALI BOFYA HAPA

Huyu Mzee Ndio Aliyetia Aibu Kwenye Bar Hii yenye Makahaba wanaocheza Nusu Uchi

 vijimambo kwenye bar zetu  

HUYU HAPA NDIYE MCHUNGAJI ADAI KUWAUA KANUMBA NA SHARO MILIONEA, AELEZEA JINSI ALIVYOFANYA....WAUMINI WAPIGWA NA BUTWAA..

Mwanaume aliyetambulishwa kwa jina la Mchungaji Mayanga amewashangaza waumini baada ya kudai kanisani kuwa yeye ndiye aliyewaua mastaa wawili Bongo, Hussein Ramadhan Mkiety ‘Sharo Milionea’ na Steven Kanumba ‘ The Great’ . Mchungaji Mayanga (mwenye kipaza sauti) akitoa ushuhuda. Tukio hilo lilitokea Jumapili iliyopita ya Oktoba 13, mwaka huu, huko Mzambarauni, Mbagala-Charambe jijini Dar katika Kanisa la Powerful Gospel Ministry lilipo chini ya Mchungaji Meshak Punkanya ambapo Mayanga alipewa nafasi ya kutoa ushuhuda. VIFO MILIONI 605  Mchungaji huyo alielezea kujuta kwake mbele ya kanisa kwa kudai kuwa kabla ya kuokoka alikuwa mchawi mkubwa aliyeishi kuzimu na kufanya kazi za mauaji sambamba na shetani mkuu (Lusifa) kwa kuwatumia vibaraka wake na majini. Mchungaji Mayanga alikiri kutekeleza vifo vya watu wapatao milioni 605 wakiwemo waigizaji hao. WAMO FIVE STARS, MTOTO WA DANDU Alisema kuwa kati ya watu aliowaua kwa njia za kishirikina wamo waimbaji wa Taarab wa Kun...