ARUSHA NA MWANDISHI WETU; AMANI JAMES Uongozi wa mtaa wa nanja kata ya moshono umekanusha kuwa sio wananchi wa mtaa huo ndio wanahusika na utupaji tataka ovyo ndani ya mtaa huo, na kusema ni watu kutoka nje ya mtaa huo ndio huleta taka hizo majira ya usiku na kuzitupa. Hivyo mwenyekiti wa mtaa huo Lilian Mmasi amesema kuwa tayari ameshaweka walinzi kwaajili ya kuwakamata watu wanao tupa taka ndani ya mta wake, na atakayekamatwa atalipa faini ya shilingi elfu hamsini (50000) na atawajibilka kufanya usafi ndani ya mtaa hiyo. Sambamba na hilo amesema kuwa walishapitisha sheria ya kila nyumba ndani ya mtaa wake kutoa shilingi elfu moja kwa kila mwezi kwa lengo la kusaidia usafi ndani ya mtaa huo, lakini hadi sasa mwitikio ya watu kutoa mchango huo ni mdogo. Hata hivyo ameendelea kusema kuwa kwa sasa kila mwananchi ni lazima alipe mchango huo na asipolipa atapelekwa mahakamani na kushitakiwa kwa kosa la kukataa kushiriki usafi ndani ya mtaa huo. Mbali na hayo pia mw