Skip to main content

Posts

Showing posts from November 2, 2014

HIZI NDIZO NYUMBA WALIZOKABIDHIWA WASANII WA ORIJINO KOMEDI NA NSSF

Meneja Mipango na Uwekezaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Abdallah Mselly (kulia) akimkabidhi msanii wa Orijino Komedi,  Mjuni Silvery ‘ Mpoki  funguo ya moja ya nyumba za gharama nafuu walizokopeshwa wasanii  wa kikundi hicho na NSSF wakati wa hafla fupi ya kukabidhi wasanii hao zilizopo Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam hivi karibuni, mkopo huo utalipwa kwa kipindi cha miaka 15. (Na Mpiga Picha Wetu) ya nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na kukopeshwa wasanii wa kikundi cha Orijino Komedi Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam. Baadhi ya nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) zilizopo katika mradi wa ujenzi wa Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam. Mac Reagan ‘Kipara’ na Mjuni Silvery ‘ Mpoki wakiangalia moja kati ya nyumba walizokabidhiwa na NSSF baada ya kukopeshwa na Shirika hilo na mkopo utalipwa kwa kipindi cha miaka 15. Kushoto, Mac Reagan, Joti na Mpoki

FAIDA, HASARA ZA WAPENZI KUFANYA KAZI OFISI MOJA

Ni Ijumaa nyingine nzuri ninapokukaribisha msomaji wangu katika zulia jekundu la uwanja wetu huu ambao ni maalum kwa mambo yahusuyo uhusiano wa kimapenzi. Mada ambayo ningependa kujadiliana nawe msomaji wangu ni kama inavyojieleza kwenye kichwa cha habari. Yawezekana wewe ni mwanaume au mwanamke ambaye unafanya kazi na umpendaye, awe ni mke, mchumba au mpenzi. Je, kuna faida gani unazozipata kutokana na kufanya kazi ofisi moja na umpendaye? Vipi kuhusu hasara na changamoto? Bila kujali kama mmekutana sehemu ya kazi na kuanzisha uhusiano wa kimapenzi au mlianza kabla lakini baadaye mkajikuta mkifanya kazi sehemu moja, lazima ujue kwamba zipo faida lakini kama hiyo haitoshi, zipo changamoto nyingi ambazo ni lazima ujue namna ya kuzishughulikia ili kuwa na uhusiano bora wa kimapenzi na amani ya nafsi yako. FAIDA KUBWA Faida kubwa ya kufanya kazi pamoja ni kwamba unapata muda wa kutosha wa kuwa karibu na mwenzi wako. Kwa wale ambao wana hulka ya wivu au wanashindwa kuwaamini wenzi

PENNY: DIAMOND HANA CHAKE, NIMESHAPOSWA

Stori: Chande Abdallah na Mayasa Mariwata MTANGAZAJI  aliyewahi kujiachia kimalovee na Nasibu Abdul ‘Diamond’, Penniel Mungilwa ‘Penny’ amesema mwanamuzi huyo kwa sasa alie tu kwani ameshachumbiwa na hawezi kumpata tena. Mtangazaji Penniel Mungilwa ‘Penny’. Kauli ya mwanadada huyo ilikuja baada ya kuulizwa kama anaafikiana na kauli ya mama wa Wema Sepetu, Miriam Sepetu kwamba, kwa kuwa Wema kamuacha Diomond basi staa huyo wa Wimbo wa Mdogomdogo bora akampose yeye. Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’. “Mmh! Hapa suala la Diamond kurudiana na mimi halipo kabisa maana simhitaji yeye wala mwanaume mwingine yeyote, mimi ninaye wangu tayari ambaye ameshanichumbia hivyo sitarajii kabisa kuwa na mwingine zaidi yake,” alisema Penny.

ANASWA! NJEMBA ADAIWA KURUBUNI WAKE ZA WATU KINGONO

Dustan Shekidele, Morogoro Mji wa Morogoro umekumbwa na matukio mfululizo ya mafumanizi ambapo baada ya ticha wa shule ya msingi kufumaniwa na dereva wa bodaboda kisha jamaa kubondwa kwa kukutwa akifanya ngono na mke wa mtu vichakani na denti wa upadri kufumaniwa, mwanzoni mwa wiki hii fumanizi lingine kiboko la njemba mwenye asili ya Kiarabu limetokea. Wakinamama (kushoto) wakimficha mwenzao (mke wa mtu) aliyenaswa kwenye ghetto la njemba mwenye asili ya Kiarabu, Hemed. Kwenye Kata ya Mazimbu mjini hapa mwanaume aliyefahamika kwa jina moja la Hemed, anadaiwa kunaswa laivu na mke wa mtu kwenye chumba anachoishi kilichopo Mtaa wa Boma mjini hapa. Ikiwa kazini, Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers ilinyetishiwa kuwepo kwa ishu hiyo hivyo kufika eneo la tukio ndani ya dakika sifuri na kunasa tukio hilo likiwa bichi. Wakinamama hao wakifanya juhudi kumtoa mke wa mtu (mwenye sidiria) eneo la tukio. Katika fumanizi hilo lililojaza ‘inzi’ (umati), Hemed alidaiwa kuw

WOLPER AMSALITI KAJALA KWA WEMA

Na Musa mateja UNAFIKI 100%!  Wakati kila mtu akiamini kwamba staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe ni shosti wa Kajala Masanja ‘Kay’, ameibua mshangao baada ya kunaswa akikumbatiana na Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ ambaye kwa sasa haziivi na Kay. Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper akishoo love na Wema Sepetu. TUJIUNGE KWENYE BETHIDEI Tukio hilo lililoibua maswali mengi yasiyokuwa na majibu ya harakaharaka lilijiri hivi karibuni katika bethidei ya shosti wa damu wa Wema, Aunty Ezekiel Grayson ambayo ilifanyika kwenye Mgahawa wa Rodizio, Masaki jijini Dar. WAKUMBATIANA Huku paparazi wetu akishuhudia na kuwafotoa picha, Wema alipoingia tu ukumbini humo, alimkuta Wolper akila raha zake ambapo alimkimbilia kisha akamkumbatia kwa dakika kadhaa huku wakimwagiana mabusu kuonesha wamemaliza tofauti zao na kwamba walikuwa ‘wamemisiana’. Wakati wamekumbatiana na kupigana mabusu walikuwa wakinong’onezana mambo yao ambapo walipomaliza waliachia vicheko vilivyosikika u

HIVI NDIVYO UJENZI HOLELA UNAVYOENDELEA SHINYANGA

Leo naibu mstahaki meya manispaa ya Shinyanga David Nkulila amefanya ziara mjini Shinyanga kuangalia sura ya mji huo kubwa zaidi ikiwa ni kuangalia ujenzi wa majengo mbalimbali kama yanazingatia sheria ya mwaka 2001 inayotaka kujengwa kwa maghorofa tu katikati ya mji na si vinginevyo.Pichani ni jengo lililoko mkabala na Bakurutu linalotiliwa  wasiwasi kuwa limejengwa bila kufuata utaratibu ambapo wataalam kutoka ofisi ya mipango mji wameahidi kulifanyia uchunguzi baada ya leo kulikagua na kubaini kuwa mipaka ya jengo hilo haionekani Kushoto ni naibu meya wa manispaa ya Shinyanga David Nkulila akilinyoshea mkono jengo hilo na kuongeza kuwa kuna taarifa kuwa halijajengwa kwa kufuata taratibu zinazotakiwa,katikati ni  mhandisi wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga  Simon Ngagani akifuatiwa na kaimu mkuu wa idara ya mipango mji,ardhi na maliasili manispaa ya Shinyanga bwana Uria Lunda   Hata hivyo M handisi wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga    Simon Ngagani alisema y