|
Leo naibu mstahaki meya manispaa ya Shinyanga David Nkulila amefanya ziara mjini Shinyanga kuangalia sura ya mji huo kubwa zaidi ikiwa ni kuangalia ujenzi wa majengo mbalimbali kama yanazingatia sheria ya mwaka 2001 inayotaka kujengwa kwa maghorofa tu katikati ya mji na si vinginevyo.Pichani ni jengo lililoko mkabala na Bakurutu linalotiliwa wasiwasi kuwa limejengwa bila kufuata utaratibu ambapo wataalam kutoka ofisi ya mipango mji wameahidi kulifanyia uchunguzi baada ya leo kulikagua na kubaini kuwa mipaka ya jengo hilo haionekani
|
|
Kushoto ni naibu meya wa manispaa ya Shinyanga David Nkulila akilinyoshea mkono jengo hilo na kuongeza kuwa kuna taarifa kuwa halijajengwa kwa kufuata taratibu zinazotakiwa,katikati ni mhandisi wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Simon Ngagani akifuatiwa na kaimu mkuu wa idara ya mipango mji,ardhi na maliasili manispaa ya Shinyanga bwana Uria Lunda |
Hata hivyo Mhandisi wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Simon Ngagani alisema yapo baadhi ya majengo mjini Shinyanga yamejengwa kwa kukiuka sheria huku akidai kuwa kuna baadhi ya wananchi wanajenga usiku ili wasibainike kuwa wanajenga kinyume cha sheria.Wengine wanaweka uzio na usipoangalia unaweza kufikiri wanajenga ghorofa kumbe la hasha!!
|
Hili jengo ni mali ya la Edgar Kasembo lililopo mtaa wa Buzuka ambapo naibu meya David Nkulila amemwagiza mhandisi wa manispaa ya Shinyanga kusimamia zoezi la kubomolewa kwani hakuna taarifa za ujenzi wa jengo hilo lililozungushiwa uzio kana kwamba kuna ghorofa linajengwa ndani hata mhandisi hana taarifa juu ya ujenzi huo |
|
Naibu meya akionesha jengo hilo ambalo linadaiwa kujengwa kinyume cha sheria huku mwenye mali akidaiwa kuwa yuko nje ya nchi.Pamoja na mambo mengine Nkulila alisema kuendelea kujengwa kwa majengo kinyume cha sheria kunatokana na kuwepo kwa mianya ya rushwa miongoni mwa watendaji wa serikali |
|
Hili jengo linatakiwa kubomolewa mara moja,limezungushiwa uzio utafikiri kuna ghorofa linajengwa |
|
Naibu meya huyo aliwataka wananchi kufuata sheria na taratibu zilizowekwa ili kuepuka lawama zisizokuwa za lazima pale wanapoamuliwa kubomoa nyumba zao. |
|
Hapa ni katika mtaa wa Kaunda mjini Shinyanga.Pichani ni jengo lililojengwa kinyume cha sheria.Mhandisi wa manispaa amesema hajui linajengwa saa ngapi.Jengo linabomolewa vipande vipande na kujengwa wakati majengo yasiyo maghorofa hayaruhusiwi katikati ya mji |
Msafara wa naibu meya wa manispaa ya Shinyanga ukishuhudia jengo linalojengwa kinyemela,na haijulikani linajengwa mchana ama usiku.Jengo hilo liko katika sura ya kuwa jengo kwa ajili ya biashara.
Comments
Post a Comment