Mgombea wa Urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu amesema wamemaliza awamu ya kwanza ya Kampeni za Uchaguzi Mkuu katika kanda kumi za Chama hicho. Hata hivyo uzoefu katika Kanda hizo umeonesha kwamba wananchi wana kiu kubwa ya uwepo wa mabadiliko ya kisiasa nchini. “Hatujidanganyi itakuwa rahisi kuishinda CCM sababu chaguzi zetu sio huru Tume huru ya Uchaguzi inapendelea waziwazi, wasimamizi wote ni wateule wa Rais, muda wowote anaweza kuwaondoa muda wowote kwa sababu yoyote ile” Tundu Lissu “Kesho tunaanza kampeni awamu ya pili baada ya kumaliza awamu ya kwanza ya uzinduzi kwa kanda 10, tumeona matamanio ya Watanzania, wanataka mabadiliko na tumeona nguvu yetu” Tundu Lissu “Tumejipanga vizuri, tutakuwa na vituo vya kukusanya matokeo, kama CCM walivyofanya 2015, kituo chetu kikavamiwa na watu wa usalama , hakuna sheria inayokataza