Mgombea wa Urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu amesema wamemaliza awamu ya kwanza ya Kampeni za Uchaguzi Mkuu katika kanda kumi za Chama hicho.
Hata hivyo uzoefu katika Kanda hizo umeonesha kwamba wananchi wana kiu kubwa ya uwepo wa mabadiliko ya kisiasa nchini.
“Hatujidanganyi itakuwa rahisi kuishinda CCM sababu chaguzi zetu sio huru Tume huru ya Uchaguzi inapendelea waziwazi, wasimamizi wote ni wateule wa Rais, muda wowote anaweza kuwaondoa muda wowote kwa sababu yoyote ile” Tundu Lissu
“Kesho tunaanza kampeni awamu ya pili baada ya kumaliza awamu ya kwanza ya uzinduzi kwa kanda 10, tumeona matamanio ya Watanzania, wanataka mabadiliko na tumeona nguvu yetu” Tundu Lissu
“Tumejipanga vizuri, tutakuwa na vituo vya kukusanya matokeo, kama CCM walivyofanya 2015, kituo chetu kikavamiwa na watu wa usalama , hakuna sheria inayokataza kukusanya matokeo kutoka kwa mawakala” Tundu Lissu
“Tunataka Tume ya Uchaguzi ichapishe fomu za kutosha, sheria inataka kila wakala apewe nakala ya matokeo, wameleta kanuni uchaguzi huu eti wakala atapewa nakala kama itakuwepo, hatutakubali mbinu hizi za kutaka kuiba” Tundu Lissu
“Kitu kinachotakiwa ni kuvunja huu mfumo wa kiutawala wa kikoloni, sisi hatukufanya mabadiliko ya mfumo huu, bila kwenda kufanya hivyo hakuna kitu, Tume ya Nyalali na Warioba zilionyesha vision, sasa tuna mahali pa kuanzia, nimeandika kitabu kitatoka wiki ijayo” Tundu Lissu
Comments
Post a Comment