Skip to main content

Posts

Showing posts from November 16, 2014

PENNY AKUMBWA NA MAUZAUZA!

Prizenta wa Kituo cha Radio E-FM cha jijini Dar, Penniel Mungilwa ‘VJ Penny’ anadaiwa kukumbwa na mauzauza yaliyodaiwa ni mapepo na kujikuta akipiga makelele barabarani. Prizenta wa Kituo cha Radio E-FM cha jijini Dar, Penniel Mungilwa ‘VJ Penny’. Habari kutoka kwa shuhuda wetu zilidai kwamba, ishu hiyo ilijiri maeneo ya Makongo jijini Dar es Salaam, juzikati wakati staa huyo akielekea msibani ambapo rafiki yake kipenzi aitwaye Skitter alifariki dunia. Chanzo hicho kilidai kwamba Penny alikuwa akiendesha gari kwa mwendo wa kawaida, alipofika maeneo hayo aliegesha gari pembeni na kuanza kupiga kelele akilia kwa uchungu hivyo kuwaacha watu waliomshuhudia wakiwa midomo wazi wakitaka kujua kilichompata mtangazaji huyo. Mpashaji wetu huyo alizidi kueleza kwamba baada ya kama  dakika kumi, Penny aliondoa gari na kuendelea na safari. Paparazi wetu aliponyetishiwa ishu hiyo alimtafuta Penny na kumuuliza kuhusu tukio hilo ambapo alisema alikuwa akienda kwenye msiba wa raf

WABUNGE WA TANZANIA WALIOKUFA KWA AJALI

WIKI iliyopita tuliwaletea marais waliouawa kwa risasi wakiwa madarakani. Wiki hii tunawaletea wabunge wa Tanzania waliokufa kwa ajali, iwe ndege, gari au usafiri wowote ule! Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime (Chadema), marehemu Chacha Zakayo Wangwe enzi za uhai wake. Hussein Ramadhan Shekilango; alikuwa Mbunge wa Jimbo la Korogwe (CCM) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (utawala). Alifariki dunia Mei 11, 1980 kwa ajali ya ndege iliyotokea kwenye milima ya Arusha. Kumuenzi, serikali iliipa jina Barabara ya Shekilango iliyopo Sinza, Dar. Juma Jamaldin Akukweti; alikuwa Mbunge wa Jimbo la Tunduru (CCM) na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge). Alifariki Januari 4, 2007 Hospitali ya Johannesburg, siku chache baada ya ajali ya ndege iliyoanguka ikitaka kupaa Desemba 16, 2006 jijini Mbeya alikokuwa kwa shughuli za kikazi. Aliyekuwa Mbunge wa Baraza la Wawakilishi Jimbo la Uzini, Zanzibar, Mussa Khamis Silima enzi za uhai wake. Chacha Zakayo Wangwe; alikuwa M

MAMA AJIFUNGUA MTOTO WA AJABU MTAZAME HAPAA.....

Na Dustan Shekidele, Morogoro My God! Mama aliyetambulika kwa jina la Swaumu Sadick (25), mkazi wa Manzese jijini Dar, amejikuta yeye na manesi wakitimua mbio kwa woga baada ya kujifungua kiumbe wa ajabu. Swaumu Sadick akiwa hospitali baada ya kujifungua mtoto huyo. Kwa mujibu wa shuhuda wetu, tukio hilo ambalo kwa sasa ni gumzo, lilijiri hivi karibuni mishale ya saa 8:00 usiku kwenye Kituo cha Afya Cha Kijiji cha Mlali kilichopo wilayani Mvomero mkoani hapa. Katika tukio hilo, ilielezwa kwamba Swaumu alijifungua kiumbe huyo wa ajabu anayedaiwa kuwa na mkia mrefu huku akiwa hana miguu. Ilidaiwa kwamba baada ya kutokea kwa tukio hilo, baadhi ya ndugu walishikwa na taharuki kubwa huku wengine wakitoa taarifa kwa mwanahabari wetu ambaye alifunga safari kutoka mjini Morogoro na kuwasili kwenye kituo hicho cha afya majira ya saa 12:00 asubuhi. Katika mahojiano maalum na gazeti hili juu ya tukio hilo, nesi wa zamu aliyekutwa kituoni hapo aliyejitambulisha kwa jina moja

SKENDO CHAFU MISS TZ 2011 BOY WAKE ASAMBAZA PICHA ZAKE ZA UTUPU MTANDAONI ZIPO HAPA ZICHEK

HAMNAZO?  MISS Sinza 2001 na aliyekuwa mshiriki wa Miss Tanzania 2011, Husna Maulid ameonesha kuwa ni sikio la kufa baada ya kupiga picha za utupu kwa mara nyingine. MISS Sinza 2001 na aliyekuwa mshiriki wa Miss Tanzania 2011, Husna Maulid. Picha hizo zilizotapakaa kwenye mitandao mbalimbali zimewashangaza watu ambapo Husna anaonekana akiwa kama alivyozaliwa huku akiwa katika mapozi tofauti hali inayoonesha kwamba alikuwa akipigwa picha hizo na mpenzi wake. Husna Maulid akiwa kwenye pozi lenye utauta!.   Kwa mujibu wa mdau ambaye aliziweka picha hizo kwenye mtandao wa Instagram, mwanadada huyo alipigwa picha hizo na mpenzi wake ambaye hakumtaja jina.Alisema mpenzi wake huyo alimuomba ampige picha ili awe anaziangalia kila wakati kwani anampenda sana ambapo Husna alikubali kupigwa picha hizo lakini matokeo yake zikazagaa mitandaoni.   Watu mbalimbali waonesha kushangazwa na picha hizo huku wengine wakimkashfu kwa maneno machafu. Baada ya kuzinyaka picha hizo, Ama

KINANA ASHIRIKI KILIMO KATIKA SHAMBA LA UFUTA LA KIKUNDI CHA (UMOJA RIKA) KATIKA KIJIJI CHA MKOTOKUYANA NACHINGWEA

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Nachingwea Mh.  Mathias Chikawe wakati alipowasili katika kijiji cha Mkotokuyana jimbo la Nachingwea katika mwendelezo wa ziara yake ya mikoa ya Lindi na Mtwara itakayomchukua siku 16 akikagua utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 inayotekelezwa  na srikali kwa pamoja na wananchi huku akihimiza uhai wa Chama cha Mapinduzi katika vijiji mbalimbali , Majimbo na wilaya Katika ziara hiyo Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi. ( PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-NACHINGWEA-LINDI) Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi akizungumza na  Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mhe. Regina Chonjo mara baada ya msafara wa Katibu Mkuu kuwasili katika kijiji cha Mkotokuyana Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana aki msikiliiza Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mhe. Regina Chonjo mara baada ya kufika kwenye shamba la ufuta la Kikundi cha Umoja Rika  l

WAKULIMA WA SHAYIRI MONDULI WAELEZEA MAFANIKIO YA UFADHILI WA TBL

Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika cha Monduli Juu cha Wakulima wa Shayiri,  Barrick Kivuyo akizungumzia mafanikio ambayo wakulima wameweza kuyapata tangu walipoanza kuingia mikataba ya kulima zao hilo na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL). Pichani ni baadhi ya nyumba za Mkulima wa Shayiri, Barrick Kivuyo zikionekana baada ya kuwa amezifanyia ukarabati ikiwa ni pamoja na kuweka umeme wa jua (Solar)  Mkulima wa Shayiri akionesha moja ya Ghala lake (Stoo) kwa ajili ya kuhifadhia zana mbalimbali za kilimo ikiwamo utunzaji wa pembejeo, ambapo jengo hilo amelijenga kutokana na fedha za Shayiri. Baadhi ya Wanawake wanaojishughulisha na kilimo cha Shayiri wakiwa katika picha ya pamoja na Ofisa wa  Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Editha anayesimamia wakulima katika eneo hilo la Monduli Juu, wilayani Monduli mkoani Arusha. Mkulima wa Shayiri wilayani Monduli Meporoo Losulu akionesha Trekta zake mbili ambazo amezinunua kutokana na kilimo cha Shayiri, pichani nying

Mkwaja FC mabingwa wapya Mwidau CUP 2014

  Mabigwa wa Mwidau CUF 2014, Timu ya Mkwaja FC wakishangilia ushindi baada ya kukabidhiwa kombe. Mdhamini wa Kombe la Mwidau CUF, Amina Mwidau akiwa na wabunge wenzake, Yussuf Salim (Chambani) na Khatib Said Haji (Konde) Mbunge Amina Mwidau akikabidhi kombe ya ushindi kwa kapteni wa timu ya Mkwaja FC, Salim Rashid akiwa pamoja na wabunge wenzake. Kombe la likiwa mezani huku mchezo wa fainali ukiendelea. Na mpigapicha Wetu …………………………………………………………………………. Na Mwandishi Wetu,Pangani Timu ya soka ya Mkwaja FC imetwaa ubingwa wa kombe la Mwidau CUP mwaka 2014 baada ya kuifunga timu ya soka ya Kiman’ga kwa mabao 4-2 katika mtanange uliipigwa kwenye Uwanja wa Mwera wilayani Pangani. Mchezo huo ambao ulikuwa ni wakuvutanikuvute katika kipindi cha kwanza lakini timu ya Kiman’ga ilionyesha kuzidiwa uwezo kwa kuweza kuruhusu mvua ya magoli katika dakika za awali toka mpira kuanza. Mchezaji wa Mkwaja FC Masoud Ticha ndio alionekana kinara katika mchezo baada ya kuifungia timu

TIMU YA UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO YAKAGUA MADARAJA LUHEKEI MKOANI RUVUMA

Meneja wa wakala wa barabara (TANROADS) mkoani Ruvuma, Mhandisi Abraham Kissimbo akizungumza na timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipofika ofisini kwake. Kiongozi wa Timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (mwenye koti jekundu) pamoja na timu yake wakijinea Daraja la Luhekei C lenye urefu wa mita 60. Kiongozi wa Timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (mwenye koti jekundu) pamoja na timu yake wakijinea Daraja la Luhekei C lenye urefu wa mita 60. Timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikiwa katika picha ya pamoja na  mwenyeji wao Mhandisi Lusage Mulenzi katika kibao cha ufunguzi rasmi wa Darala la Luhekei C. Daraja hili lina urefu wa mita 60, lilifunguliwa rasmi tarehe 18 Julai, 2014 na Mheshimiwa Rais, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

NITAZAA WATOTO MPAKA NIAMBIWE BHAAASI.....SHAMSA FORD AFUNGUKA CHEKI HAPA

Staa wa Filamu za Kibongo,  Shamsa  Ford  amesema kuwa kutokana na kupenda watoto anaona hawezi kutosheka kuzaa watoto wawili au watatu ila atakachofanya ni kuzaa tu mpaka atakapoambiwa hospitali inatosha. Staa wa Filamu za Kibongo,   Shamsa Ford.   Akichezesha taya na mwandishi wa habari hii, Shamsa alisema kuwa tangu alipoanza uhusiano na mchumba wake aitwaye Dick kisha kuzaa naye, walikuwa wamepanga wazae angalau watoto saba ila wapishane kidogo ili waweze kuwalea vizuri.   “Siwezi kutosheka kuzaa watoto wawili au watatu, nitakachofanya nitazaa mpaka basi. Sijali kwamba eti nikizaa nitachuja na kuharibu umbo langu kwani naamini kuwa hata kama nisipozaa bado umri utazidi kwenda na nitakapofikia kuzeeka nitazeeka bila kuwa na watoto,” alisema Shamsa.