SIYO habari tena, kwani dunia nzima inajua kuhusu kifo cha shujaa wa Afrika, nembo ya mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi, komredi aliyefungwa jela miaka 27 akitetea usawa baina ya wananchi wa Afrika Kusini, Nelson Rolihlahla Mandela. Risasi Jumamosi, kwa msaada wa vyanzo mbalimbali, linamulika kwa undani chanzo hasa cha kifo cha Mandela, aliyefikwa na mauti usiku wa kuamkia jana, Desemba 5, mwaka huu akiwa na umri wa miaka 95. Mandela akiwa na mkewe Graca Machel ( kushoto ) na mtalaka wake, Winnie Mandela ( kulia ). Ripoti za ndani zaidi, zinabainisha kuwa afya ya Mandela ilianza kuleta mushikeli tangu akiwa kijana na kwa mantiki hiyo, sehemu kubwa ya maisha yake alisumbuliwa na maradhi. UNDANI WA MARADHI YALIYOMUUA Ripoti za wataalamu mbalimbali kuhusu afya ya Mandela, kwa pamoja zinatoa majibu kwamba chanzo cha maradhi ya mapafu ambayo ndiyo hasa yaliyokatisha uhai wake ni matokeo ya ukatili aliokuwa anafanyiwa gerezani, kipindi akiwa mfungwa wa kisiasa. Habari zinase