Skip to main content

Posts

Showing posts from January 19, 2014

HII NDO NYUMBA ALIYONUNUA MSANII YOUNG DEE MAENEO YA KIMARA. ICHEKI HAPA

Star wako Young Dee ameweza kupost picha za Crib yake mpya ambayo ameinunua na kuiweka  katika akaunti yake ya instagram.com na kuweza kusema  “When i say i love music this is wats uup!!! Jus bought a crib oohh lord..” Crib hii ambayo ipo maeneo ya Kimara suka Star wako Young Dee amepiga story na perfecttz.com kwamba mpaka mwezi wa Saba au Nane atakua tayari ameshahamia rasmi kwa sababu ryt now ipo katika matengenezo!

HII NDIO SKENDO INAYOMKABILI SNURA

Stori:  Shani Ramadhani na Mayasa Mariwata STAA wa wimbo wa Majanga, Snura Mushi ameingia kwenye majanga baada ya kudaiwa kukacha na deni la prodyuza Mohammed Kandoro wa Studio za Fire Music ambaye alimrekodia nyimbo kadhaa wakati akisaka kutoka. Snura Mushi. Habari kutoka kwa chanzo cha kuaminika zinasema kuwa Snura ameingia mitini na kiasi cha Tsh. 400,000 za prodyuza huyo na kwamba sasa amehamia studio nyingine. Risasi Mchanganyiko lilimvutia waya Kandoro na kumwuliza kuhusu ukweli wa minong’ono hiyo, ambapo alikiri na kusema: “Ni kweli namdai laki nne. Nimefanya naye kazi kwa muda mrefu lakini sasa naona ameamua kuondoka na deni langu.” Snura alipopigiwa simu na kuelezwa kuhusu madai hayo, alifunguka: “Kama kuna deni basi meneja wangu HK (Hyper Man) ndiye anayehusika, maana kila kitu nilimkabidhi yeye na naamini alilipa, sasa kama hakulipa hayo ni mambo yanayomhusu yeye, si mimi tena.” Katika kutafuta mzani wa habari, gazeti hili liliwasiliana na meneja wa Snura, HK am

BABY MADAHA: NIMEUMBUKA!

Stori: Mwandishi Wetu Jambo limezua jambo! Ile skandali ya kunaswa baada ya kuingia mkenge kwenye mtego wa kujiuza imemtokea puani staa wa sinema na Bongo Fleva, Baby Joseph Madaha ambaye amekiri kuumbuka. Baby Madaha akiwa na meneja wake Joe Kariuki. Habari hiyo iliruka hewani kwenye gazeti dada la hili, Ijumaa wiki iliyopita toleo namba 862 la Januari 17 hadi 23 likiwa na kichwa cha habari ‘BABY MADAHA ANASA MTEGO WA KUJIUZA. SAFARINI Ilielezwa kuwa wakati skendo hiyo ikiingia mitaani, mwanadada huyo alikuwa safarini kuelekea Nairobi, Kenya ambako ndiko yaliko Makao Makuu ya Kampuni ya Candy n Candy iliyompa mkataba mnono wa takribani Sh. milioni 200 ili wasambaze na kuuza kazi za Baby Madaha. MAPOKEZI Kwa mujibu wa chanzo chetu makini nchini humo, imezoeleka kuwa kila Baby Madaha anapotua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, Nairobi kwa ajili ya kazi za kampuni hupokelewa na timu maalum kisha kuchukuliwa na lile gari la bei mbaya aina ya Audi TT. Iliele

MBUNGE WA CHALINZE, SAID BWANAMDOGO (CCM) AFARIKI DUNIA

Mbunge wa Chalinze, Said Ramadhani Bwanamdogo enzi za uhai wake. HABARI zilizotufikia hivi punde ni kwamba Mbunge wa Chalinze, Said Ramadhani Bwanamdogo (CCM), aliyekuwa amelazwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU), katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu (MOI)  amefariki dunia!

HIVI NDIVYOJAHAZI WALIVYOTIKISA KWA MUZIKI MKALI WA TAARAB DAR LIVE

Mzee Yusuf akiwadatisha mashabiki waliofurika Dar Live. Mzee Yusuf na wanenguaji wake kazini. Umati wa mashabiki ukiserebuka. Leila Mohamed akiwa kazini. Shabiki akiserebuka. Chidi Boy akikunguta kinanda. Pozi la kinadada ndani ya Dar Live. Mashabiki na raha zao. WAPENZI wa muziki usiku wa kuamkia leo waliburudika kwa mapigo ya bendi ya taarab ya Jahazi katika onyesho la nguvu la kwanza kwa mwaka 2014 ndani ya uwanja wa Taifa wa Burudani Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.

HUU HAPA NDIO UHAMISHO NA UTEUZI WA MAWAZIRI NA NAIBU MAWAZIRI

Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue akitangaza baraza jipya la mawaziri wakiwemo walioziba nafasi tano zilizokuwa wazi na wengine kuhamishiwa wizara nyingine! ………………………………………………………………………………… Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amewahamisha na kuwateua baadhi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri kama ifuatavyo:- 1.0 OFISI YA RAIS Hakuna mabadiliko. 2.0 OFISI YA MAKAMU WA RAIS 2.1 Waziri wa Nchi (Muungano) – Hakuna mabadiliko 2.2 Mhe. Eng. Dr. Binilith Satano MAHENGE (Mb) Waziri wa Nchi (Mazingira). 2.3 Mhe. Ummy Ali MWALIMU (Mb) Naibu Waziri  3.0 OFISI YA WAZIRI MKUU Hakuna mabadiliko 4.0 WIZARA 4.1 WIZARA YA FEDHA 4.1.1 Mhe. Saada Mkuya SALUM (Mb) Waziri wa Fedha Mhe. Mwigulu Lameck NCHEMBA (Mb)  Naibu Waziri wa Fedha 4.1.2 Mhe. Adam Kighoma Ali MALIMA (Mb) Naibu Waziri wa Fedha 4.2 WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA Hakuna mabadiliko 4.3 WIZARA YA KATIBA NA SHERIA 4.3.1 Mhe. Dkt. Asha-Rose Mtengeti MIGIRO (Mb) Waziri wa Katiba na She