Skip to main content

Posts

Showing posts from February 2, 2014

MAMA SHARO MILIONEA ALIA NA KAZI ZA MWANAE…

Ikiwa ni tariban mwaka mmoja na miezi kadhaa imepita tangu SHaro Milionea afariki dunia kwa ajali ya gari huko Muheza mkoani Tanga tayari imeshaonekana watu kumsahau na kuendelea kula kupitia jina lake na sura yake. Kupitia 255 ya XXL ndani ya Clouds FM inayoruka kila siku za Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 7 hadi saa 10 jioni Mama Sharo alikuwa na haya ya kueleza; “Hata mimi naziona tu hizo kazi zenye sura ya mwnangu ndani yake na hata mara kadhaa kuulizwa na baadhi ya marafiki zake wa karibu kuwa napokea chochote juu ya muvi fulani iliyotoka au sipokei. mara zote nawajibu kuwa sipokei kitu kwa sababu ukweli upo hivyo kuwa sishirikishwi kwa chochote kwenye kazi zinazoendelea kutoka tangu mwanangu afariki dunia.” – Mama Sharo. Baabkubwa inaungana na Mama Sharo katika kukemea watu wa aina hii ambao wanapenda kula kupitia migongo ya wenzao.

TAZAMA JINSI RAISI OBAMA ALIVYOAMUA KUKATIZA MITAANII KUJICHANGANYA NA WANANCHI WAKE

Rais Barack Obama hivi karibuni alikataa walinzi na kuamua kutembea mwenyewe kwenye mi mitaa yenywe wahuni  wengijambo lililoleta hofu kwa wananchi wengi huku wakipigwa na butwa

RAIS DR. JAKAYA KIKWETE AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA SHERIA

Jaji Mkuu  wa  Tanzania  Mohamed  Chande Othman (kushoto)  mstari  wa kwanza akiwa katika maandamano ya siku ya sheria leo na  baadhi ya  majaji  kwenye   viwanja  Mahakama Tanzania vilivyoko Ocean Roads . Bendi ya polisi ikiongoza maandamano ya siku ya sheria katika  viwanja  Mahakama Tanzania  vilivyoko Ocean Roads yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam Rais Jakaya Kikwete akipokelewa (kushoto) na  Jaji Mkuu  wa  Tanzania  Mohamed  Chande Othman (kulia) leo mara baada ya  kuwasili  kwenye   maadhimisho ya   siku  ya sheria   mara baada na  baadhi ya  majaji  kwenye   viwanja  Mahakama Tanzania vilivyoko Ocean Roads Rais Jakaya Kikwete akitoa hotuba  leo  kwenye   maadhimisho ya   siku  ya sheria    kwenye   viwanja  Mahakama Tanzania vilivyoko Ocean Roads Jakaya Kikwete akipokelewa (katikati ) na  Jaji Mkuu  wa  Tanzania  Mohamed  Chande Othman (kulia) leo mara baada ya  kuwasili  kwenye   maadhimisho ya   siku  ya sheria   mara baada na  baadhi ya  majaji  kwenye   viwanja  Mahakam

KINANA AZURU NYUMBANI KWA MAREHEMU MGIMWA, IRINGA

Katibu Mkuuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsalimia Mama Mzazi wa aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa, Consolata Mgovano, alipokwenda nyumbani kwa marehemu Mgimwa, Kijiji cha Magunga, jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini, leo jioni. Wengine ni watoto wa marehemu Mgimwa, Stanisla Mgimwa, na Rozalina Mgimwa. Kinana akizungumza na familia huyo ya marehemu Mgimwa. Wapili kushoto ni Johakim Mgimwa Kinana akimuaga Mama Mgimwa baada ya mazungumzo Kinana akiaga Mmoja wa wanafamilia akilia Kinana alipotembelea familia hiyo ya Mgimwa Nyumbani kwa marehemu Mgimwa Kinana akipokea saluti ya Kijana wa CCM, alipowasili Ifunda, Iringa Vijijini kabla ya safari ya kwenda nyumbani kwa marehemu Mgimwa. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msavatavangu: Picha na  theNkoromo Blog

DK.SHEIN AENDELEA NA ZIARA YAKE INDIA.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiangalia taa iliyotengenezwa na Akinamama wa Zanzibaar Kisiwani Pemba alipotembelea Chuo cha Barefoot kinachotoaa mafunzo ya Amali kwa wanawake pekee katika Kijiji cha Tilonia Wilaya ya Ajmer Jimbo la Rajastan ncchini India akiwa katika siku ya pili ya ziara yeke katika kukuza uhusiano na ushirikiano katika nchi mbili hizo.[Picha na Ramadhan Othman,India.] Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (mwenye suti nyeusi katikati)akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Chuo cha Barefoot kinachotoaa mafunzo ya Amali kwa wanawake pekee katika Kijiji cha Tilonia Wilaya ya Ajmer Jimbo la Rajastan nchini India pamoja na ujumbe wake akiwa katika siku ya pili ya ziara yake katika kukuza uhusiano na ushirikiano katika nchi mbili hizo.[Picha na Ramadhan Othman,India.] Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ( katikati)akiwa na Viongozi wa  Chuo cha Ba

HIZI NDIZO SABABU ZILIZOSABABISHA JIDE KUOMBA TALAKA

Stori:  Shani Ramadhan UNAWEZA ukakataa lakini ndivyo ilivyotokea, ndoa ya mtangazaji mahiri Bongo, Gardner Gabriel Fikirini Habash ‘Kapteini’ na Mbongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ iliyofungwa miaka 9 iliyopita inadaiwa kuingia kidudu kufuatia mke huyo kuomba aandikiwe talaka, ni Ijumaa Wikienda pekee lenye uthubutu wa kuripoti mkasa wote. Jide akiwa na jumewe Gardner. Kwa mujibu wa chanzo chetu cha kuaminika, Jide au Lady Jaydee alifikia uamuzi huo baada ya Gardner kupata kazi ya kutangazia redio moja nchini Kenya. HABARI KAMILI Mnyetishaji wa kisanga hiki, aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa mara baada ya mume huyo kupata mchongo mzima alirudi nyumbani akiwa na furaha na kumwambia mkewe kuhusu bahati hiyo. “Baada ya Gardner kupata mchongo wote wa kazi alikwenda mbio nyumbani kwake Kimara (Dar) ili akamwambie mkewe. “Pia katika safari ya kwenda Kenya kupiga mzigo ilikuwa aende na mkewe huyo kwa sababu lilikuwa suala la kuhamisha makazi yao Tanzania,” kilisema chanzo h

HIZI NDIO SABABU ZA VIDEO YA MAJANGA YA SNURA KUFUNGIWA!!

  Inawezekana ukawa unashangaa baada ya kuona ukimya mara baada ya kutambulishwa kwa video ya Msanii Snura kisha kutoiona ikionekana mara kwa mara kwenye televisheni yako,kiu ya swali hili naikata kwa kusikiliza alichokisema Bosi anaesimamia kazi za Snura meneja wake ‘HK’. Hk ameanza kwa kusema>>’Kilichotokea ni kwamba video ya Nimevurugwa ni video tuliyokua tunakata kiu ya mashabiki wetu waliokua wamemis vitu fulani kwenye video ya Majanga’ ‘Wengi tulivyotoa video ya Majanga walizungumza mengi sana wakidai kwamba video haikuwa nzuri sana,video ya kawaida na sababu kubwa ilikua ni Snura hakukata mauno kwenye hiyo video,tukaona tukate kiu ya wapenzi wetu ambao ukiacha tu nyimbo za Snura watu wanapenda kumuona Snura akitumia maumbile yake kwenye kucheza’ ‘Kwenye video ya Nimevurugwa kumekua na style tofauti sana kwenye upande wa kucheza,matokeo yake video ilipotoka siku chache vituo vya televisheni viliacha kupiga wimbo wa msanii wangu,nikiwa kama meneja nikaanza kuzunguka kujua

haya ndiyo yaliyosemwa na baadhi ya wanafunzi wanaosoma na waliowahi kusoma chuo cha uandihi wa habari na utangazaji kupitia mtandao wa faceebok baada ya raisi wa chuo hicho kujiuzulu

haya ni baadhi ya maoni yaliyotolewa na baadhi ya wanafunzi wanaosoma na walio wahi kusoma chuo hicho baada ya raisi  wa chuo kijiuzulu Hussein Said   Kiongoz vp tena ukaamua kuchukua maamuz magumu nn shida.? about an hour ago  ·  Like Precious Keyler Prosper   pole dogo hata sisi tulitamanigi kujiuzulu lkn tulikomaa mpaka mwisho...ndo uongozi 51 minutes ago  ·  Like Annie Gasper   Y u do this jaman y? 50 minutes ago  ·  Like Charles Kikoricho   Binafsi bila kung'ata maneno nawataka viongozi wa chuo watambue kuwa taasisi hiyo imekuwa sasa sio kama taasisi ya mwaka juzi ifike sehemu waelewe kuwa hakuna uongozi usiokuwa na katiba serikali yeyote ile inaongozwa kwa katiba sasa iweje wapinge mimi  nasema kuna lao jambo .unazalisha mwandishi ambae hajaongozwa kwa katiba huku atakuja kuandika habari za watu wenye katiba ataweza du hakika bongo bora angekuwepo mandela na nyerere NIMEIPENDA HII SHADY MAANA HATA KWEN

HICHI NDICHO ALICHOKISEMA RAISI WA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI ARUSHA BAADA YA KUJIUZULU

Raisi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji arusha(AJTC) akitangaza kujiuzulu nafasi ya uraisi Raisi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji bwana George Silange aliyechaguliwa kwa ushindi mkubwa na wanafunzi wa chuo hicho katika uchaguzi uliofanyika baada aliyekuwa raisi wawakati huo bwana Daved George kusimamishwa pamoja na uongozi wake wotee! Na alipewa dhamana ya kuendeleza kijiti hicho ni George Silange ila naye ameamua kujiuzulu na kuiachia kijiti hicho.Ila baada ya kujiuzulu tu aliandika ujumbe huu katika akaunt yake ya faceebook: NAWAPENDA WOTE MLIONIPA USHIRIKIANO WA KUTOSHA NIKIWA MADARAKANI NATANGAZA RASMI KUANZIA SASA NIMEJIUZULU NAFASI YA URAIS NDANI YA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI ARUSHA  PIA NAWAPONGEZA WALE MASNECH NA WANAFIKI MLIOKUWA NDANI YA UONGOZI WANGU  NA MWISHO NIKUSHANGAE WEWE UNAEDAI WANACHUO WAWE NA NIDHAMU WAKATI WEWE HUONYESHI MFANO SIJAWAHI KUMTUKANA MKUFUNZ WALA MWANA CHUO MWENZANGU ALAFU WEWE UNANIITA KICHWA CHA NDIZI

HIVI NDIVYO VIPAJI VILIVYOIBULIWA NDANI YA CHUO CHA UANDISHI NA UTANGAZAJI (AJTC)

Baadhi ya washiriki waliokuwa wakichuana katika kinyanganyiro cha kuwasaka wanafunzi wenye vipaji katika shindano la kuwasaka wanafunzi wenye vipaji vya dj's, dancers, uimbaji na na kumtafuta miss na mr  katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji arusha, baadhi ya wanafunzi wameweza kushinda mataji hayo kwa kufanya vizuri kwa upande wa miss A.J.T.C Taji hilo limechukuliwa na bi Irene Lyimo,huku mr A.JT.C akinyakua Benson Mwakakungole  Miss Irene Lyimo akiwa pamoja na Mr Benson kwa upande wa dancers taji ushindi umechukuliwa na Bi. Vaileth Gabriel Akifuatiwa na bi lilian deus huku nafasi ya mwisho ikishiliwa na juma AKA Fall Ipupa mmshindi wa kwanza bi VailetGabriel akionesha uwezo wake jukwaani                                         Mshind wa pili katika kundi la dancers Bi.liliaj Deus wakati akidance                                                         mshiriki w aliyeshikilia nafasi ya Tatu juma A.K.A Fall Ipupa Kwa Upande wa dj b

NAIBU WAZIRI WA FEDHA ADAM MLIMA ASISITIZA UMUHIM WA MASHINE ZA EFD KWA WAFANYABIASHARA NCHINI.

Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima (kushoto) akizungumza na Mkuu wa mkoa wa Mara John Tuppa (kulia) mara baada ya kuwasili katika ofisi za makao makuu ya mkoa wa Mara. Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima akiongea na wa wafanyabiashara wa mkoa wa Mara juu ya umuhimu wa utumiaji wa mashine za kodi za kielektroniki (EFDs) kwa wafanyabiashara hao kukusanya kodi ya ongezeko la thamani (VAT) ili Serikali iweze kutoa mahitaji ya kijamii na uchumi kwa wakati. Kamishna wa Kodi za Ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Patrick Kasera akifafanua kwa wafanyabiashara wa mkoani Mara juu ya mashine za EFDs na kusema kuwa mashine hizo kazi yake kuu ni kutunza kumbukumbu za biashara hasa manunuzi na uuzaji na sio mfumo wa kodi kama ilivyopokelewa mwanzoni na wafanyabiashara nchini. Baadhi ya wafanyabiashara wa mkoa wa Mara wakimsikiliza  Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima (hayupo pichani) alipokuwa alipozungumza na wafanyabiashara hao jana mjini Musoma katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa huo. Baadhi w