Serikali ya Syria bado haikusema kitu kuhusu taarifa kutoka wakuu wa Marekani kwamba ndege za Israel zimefanya mashambulio katika ardhi ya Syria, ambako inaarifiwa ghala ya silaha imeshambuliwa. Wakuu wanasema makombora yalifyatuliwa kutoka ndege za Israel ambazo ziliruka kwenye anga ya Libnan, nchi ya jirani. Huku nyuma kuna taarifa za mauaji zaidi katika miji ya pwani ya Syria kukiwa na tuhuma kuwa raia wengi wamechinjwa na wanajeshi wa serikali na wanamgambo. Wanaharakati wanaripoti kuwa mauaji ya pili yamefuatia yale ya kwanza katika eneo hilo-hilo la mwambao kaskazini-magharibi mwa Syria. Wanasema mauaji ya kwanza yalifanywa kwenye kijiji cha al-Beida cha Wasunni, ambacho kilivamiwa na wanajeshi wa serikali siku ya Alkhamisi. Wanaharakati wamewataja watu 50 ambao wanasema walichinjwa kati yao wakiwemo wanawake