Skip to main content

Posts

Showing posts from June 29, 2014

Hizi ndizo sababu ya DUDE, TINO KUWEKWA MBARONI KENYA

Stori:  Gladness Mallya WASANII nyota wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ na Hisan Muya ‘Tino’ hivi karibuni walitiwa mbaroni katika mji wa Kilifi ulio mbele ya Mombasa nchini Kenya baada ya kukutwa wakipiga picha za filamu yao bila kuwa na kibali. Msanii nyota wa filamu Bongo, Hisan Muya ‘Tino’. Hata hivyo, waigizaji hao baadaye waliachiwa, ingawa hali ilikuwa ngumu kidogo kwa Tino, ambaye polisi wa Kenya walidai hakuwa Mtanzania, bali ni raia wa Somalia. Dude alithibitisha kutokea kwa tukio hilo akisema liliwatokea kutokana na mazoea ya huku nyumbani ambako hufanya shughuli zao za kupiga picha za filamu zao bila kuhitaji kibali. Msanii nyota wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’. “Yaani tumepata aibu ya mwaka, kwani tulienda kushuti bila kuomba kibali kutokana na mazoea ya huku kwetu Bongo, tulipekuliwa sisi na gari letu, baada ya hapo kibali kikaletwa nikaachiwa lakini Tino waliendelea kumshikilia wakisema ni Msomali mpaka

OFISI YA RAIS, TUME YA MIPANGO YAKAGUA MAENDELEO YA MRADI WA CHUMA LIGANGA MKOANI NJOMBE

 Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (wa tatu kushoto) akipata maelezo kuhusu Mradi wa Chuma Liganga kutoka kwa Nie Zhiyan (kulia), ambae ni Makamu Ofisa Muendeshaji Mkuu wa Tanzania China International Mineral Resources Ltd (TCIMRL). Hili  ni eneo ambalo kiwanda cha chuma chenye uwezo wa kuzalisha tani milioni moja kwa mwaka kitajengwa. Kutoka kushoto, wengine ni Bw. Ramson Mwilangali, Kaimu Mkurugenzi wa Viwanda Mama – NDC , Bw. Erasmus Masumbuko, Mchumi – Tume ya Mipango, Bw. Maduka Kessy, Naibu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango, anaeshughulikia Sekta za Uzalishaji, Bw. Israel Mkojera Makamu Meneja Utawala – TCIMRL, Bi. Florence Mwanry Naibu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango anaeshughulika na Huduma za Jamii na Idadi ya Watu na Bw. Mlingi E. Mkucha, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NDC.  Mlima wenye madini ya chuma, ambapo  shughuli ya uchimbaji wa chuma unategemea kuanza  kut

Watoto waishio kwenye mazingira magumu hususani wanaoishi na VVU wazidi kunyanyapaliwa.

Mahmoud Ahmad,Arusha. WATOTO waishio kwenye mazingira magumu  na yatima hususani wanaoishi na virusi vya ukimwi wamekuwa wakikabiliwa na changamoto kubwa ya kunyanyapaliwa na wazazi na hata walimu mashuleni hali ambayo imekuwa ikiwawia vigumu watoto hao kuendelea na masomo.Aidha unyanyapaa kwa watoto yatima wanaoishi na virusi vya ukimwi imekuwa ni changamoto kubwa kwao ambapo asilimia kubwa ya watoto wamekuwa wakikosa haki zao za msingi hususani elimu kutokana na hali hiyo. Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi wa shirika la Sorode Organization la jijini hapa, Sophia Justine wakati akizungumza na watoto na walezi waliohudhuria katika harambee ya kuchangia bweni  kwa ajili ya watoto yatima wa kike  wanaolelewa katika kituo cha Faraja ambapo shs 1 milioni zilipatikana huku zikihitajika shs 50 milioni. Alisema kuwa, kumekuwepo na unyanyapaa wa hali ya juu unaofanywa na walimu katika  shule mbalimbali baada ya kupewa taarifa kuhusu watoto hao hali ambayo imekuwa ikisaba

WAZIRI MKUU: OMBEENI TAIFA NA UCHAGUZI MKUU UJAO

*Askofu Niwemugizi ataka UKAWA warudi bungeni mwezi ujao, asema siyo ombi …………………………………………………………… WAZIRI MKU U Mizengo Pinda amewaomba viongozi wa dini kote nchini na wananchi waungane pamoja ili kuombea uchaguzi mkuu wa viongozi wakuu wa Rais, wabunge na madiwani unaotarajiwa kufanyika mwakani. Ametoa wito huo leo mchana (Jumanne, Julai mosi, 2014) wakati akizungumza na maelfu ya waumini na viongozi mbalimbali waliohudhuria ibada ya Jubilei ya miaka 25 ya Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Iringa, Mhashamu Tarsicius Ngalalekumtwa katika uwanja wa Kichangani wa Kanisa Kuu la Kihesa. “Maaskofu wote mliopo hapa, najua mnavyoipenda Tanzania… kila kanisa lina sala maalum ya kuliombea Taifa na viongozi wake, ninawaomba viongozi wetu mliombee Taifa letu ili mambo yaende salama na hasa uchaguzi wa mwakani,” alisema. Akirejea mahubiri yaliyotolewa kwenye ibada hiyo na Mhashamu Askofu Mkuu Paulo Ruzoka wa Jimbo Katoliki la Tabora ambaye alitoa mfano wa Daudi na Goliathi,

Tazama video ya Roma akifunguka juu ya BIFU NA WEUSI - ROMA MKATOLIKI

Swali: Kuna wasanii wengi kutoka Tanga lakini wewe umetoka mapema. Unazungumziaje msoto uliopitia hadi ukatusua kimuziki? Roma Mkatoliki (kulia) akifunguka wakati akihojiwa na prizenta wa Global TV Online, Pamela Daffa 'The Mic Queen' Roma: Ni kweli Tanga kuna wasanii wengi kama ilivyo Kigoma. Tuna-fight sana na Kigoma. Kuhusu msoto siyo kwa wasanii wa Tanga tu hata sehemu nyingine kuna msoto. Kwa Roma ilikuwa rahisi kwa sababu alisoma gemu akagundua kuna vitu fulani havijaguswa ndipo nikapita hukohuko. Swali: Roma ni staa mkubwa wa Hip Hop Bongo. Je, ni kichwa kipi kingine unakikubali? Roma: Wapo watatu. Wa kwanza ni Roma, wa pili ni Roma na wa tatu ni Roma. Swali: Kwa nini Roma? Roma: Najikubali sana ndiyo maana najiona namba moja, mbili na tatu. Swali: Wewe ni mmoja wa wana-hip hop wasomi. Umemaliza UDSM Mlimani. Kwa nini ukaegemea kwenye muziki badala ya kuajiriwa? Roma: Siyo kwamba sijawahi kuajiriwa. Kwanza hata fedha ya kwenda studio nilidunduliza mshahar

Hii ni zaidi ya unyamaaa!!MUME AMPIGA NYUNDO NA KUMKATA MAPANGA MKEWE

DAH! Inasikitisha sana jamani. Faustina Selali, 38, mkazi wa Mgeta, Mvomero mkoani hapa, yupo kwenye mateso makali akijiuguza kutokana na kipigo alichopata kutoka kwa mumewe wa ndoa aliyemtaja kwa jina la Lugasiani John Miasiku, kisa kikiwa ni mumewe huyo kutaka kuoa mke wa pili. Faustina Selali, akiwa katika maumivu makali baada ya kushambuliwa na mumewe. Mwanamke huyo amelazwa katika wodi nambi 3 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, ambapo amesimulia kisa chote mbele ya kamera ya Uwazi. KISA CHENYEWE Akizungumza kwa tabu, Faustina alisema tukio hilo lililobadilisha historia ya maisha yake na kumwachia machungu moyoni mwake, lilitokea Juni 25, mwaka huu majira ya saa nne usiku ndani ya nyumba yao. “Mimi na mume wangu tumeishi kwenye ndoa kwa muda wa miaka 20 na kufanikiwa kupata watoto watano. Kwa kipindi kirefu nilihisi ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamke mwingine, wakati naendelea kumchunguza, mume wangu akaniambia anataka kuoa mke wa pili,” alise

WAZIRI MKUU: MAANDALIZI YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA YANAENDELEA

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao unatarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu yanaendelea japo kwa kiasi ki kubwa hatma yake inategemea kukamilika kwa mchakato wa Katiba mpya. Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumatatu, Juni 30, 2014) wakati akizungumza na Mameya wa Majiji, Manispaa na Wenyeviti wa Halmashauri za Miji na Wilaya Tanzania katika kikao cha siku moja kilichofanyika kwenye ukumbi wa Regal Naivera jijini Tanga. Waziri Mkuu yuko Tanga kwa ajili ya sherehe za Serikali za Mitaa ambayo kilele chake kitafanyika kesho Julai mosi kwenye uwanja wa Tangamano jijini hapa. Ameamua kukutana na viongozi hao ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya kukutana nao aliyoitoa Mei 14, 2014 wakati akifungua Mkutano Mkuu wa ALAT. “Uchaguzi wa Serikali za Mitaa bado ni kitendawili kwa sababu kwa kiasi kikubwa inategemea sana kukamilika kwa Mchakato wa Bunge la Katiba,” alisema na kuongeza: “Kama Wizara tunaendelea na maandalizi tukiamini uch

Rais Kikwete akutana na makamu wa Rais wa Kampuni ya Viettel ikulu

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Viettel Group ya nchini Vietnam Bwana Le Dang Dung ikulu jijini Dar es Salaam leo(picha na Freddy Maro)

WATANZANIA WAENDELEA KUMIMINIKA KATIKA BANDA LA PPF SABASABA KUJIPATIA HUDUMA MBALIMBALI

 Afisa Michango kutoka PPF Makao Makuu, Bi Glory Maboya (kulia) akimpatia maelezo ya Huduma mbalimbali mmoja wa wateja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF wakati alipotembelea Banda la PPF katika Viwanja vya Mwl Nyerere maarufu kama Sabasaba.  Mkazi wa Jiji la Dar Es Salaam akipatiwa maelezo juu ya huduma ya Fao la Kujitoa kutoka kwa afisa uendeshaji wa Mfuko wa PPF kanda ya Ziwa, Bi Grace Balele wakati mteja huyo alipotembelea banda la Mfuko wa Pensheni wa PPF katika Maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa katika Viwanja vya Sabasaba. Mchambuzi wa Mfumo wa Teknolojia (System Analysist) kutoka Mfuko wa Pensheni wa PPF Makao Makuu, Bi Irene Togolai akimpatia fomu ya Kujiunga na Mfuko wa Pensheni wa PPF mmoja wa Wakazi wa Jiji la Dar aliyetembelea Banda la PPF katika Maonyesho ya 38 ya Kibiashara ya Kimataifa yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Sabasaba Mchambuzi wa Mfumo wa Teknolojia (System Analysist) kutoka Mfuko wa Pensheni wa PPF Makao Makuu, Bi Ire

SAFU MPYA YA UONGOZI WA SIMBA SC CHINI YA RAIS AVEVA INASIMAMA HIVI..

RAIS mpya wa klabu ya Simba sc, Evans Elieza Aveva alipata kura 1,455 dhidi ya mpinzani wake Andrew Peter Tupa, aliyepata kura 388. Mjumbe wa Kamati ya Uchaguzi na aliyesimamia zoezi hilo, Amin Bakhresa, wakati akitangaza matokeo hayo alisema kuwa mshindi wa nafasi ya Makamu wa Rais ni Geofrey Nyange ‘Kaburu’ aliyepata kura 1,046 na kuwashinda Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ (412), Swedy Mkwabi (373) na Bundala Kabula kura 25

COUTINHO AANGUKA MKATABA WA MIAKA MIWILI YANGA SC

Andrey Coutinho akisaini mkataba wa kuitumikia Yanga kwa kipindi cha miaka miwili mbele ya Katibu Mkuu Beno Njovu leo makao makuu ya klabu Kiungo mshamabuliaji Andrey Marcel Ferreira Coutinho raia wa Brazil leo amesaini mkataba wa miwili kuitumikia timu ya Young Africans kwa ajili ya michuano mbalimbali ikiwemo ya Ligi Kuu ya Vodacom pamoja na mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika. Katibu mkuu wa Young Africans  Bw Beno Njovu amesema usajliwa mchezaji Coutinho ni sehem ya muendelezo wa maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu na kama ilivyokawaida wao mambo yao ni kimyakimya. Coutinho ambaye alizaliwa tarehe 12 Januari 1990 amekulia kwenye mji wa Berem ambapo alianza kucheza soka la kulipwa katika klabu ya Paysandu Sports Club kabla ya kwenda nchini Asia katika nchi ya Myanmar katika klabu ya Rukhapura United.

TAASISI YA FARIDAS FOUNDATION YAZINDULIWA

 Farida A. Sekimonyo Mkurugenzi  wa Faridas Foundation Akiomba Sala ya  Uzinduzi Rasmi katika uzinduzi wa taasisi hiyo wakati wa uzinduzi wake uliofanyika kwenye hoteli ya Blue Pear jengo la Ubungo Plaza jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.  Mshehereshaji wa Shughuli ya uziinduzi wa Faridas Foundation Taji Liundi  Elias Masaki katibu mkuu ‘CHAWATA’ na pia Mweka Hazina Shirikisho la watu wenye ulemavu akichangia  mawazo kuhusiana na jinsi Farida Foundation Inavyofanya kazi zake kwa Jamii  Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia maada mbalimbali zilizokuwa zikiendelea katika uzinduzi wa Faridas Foundation Kassim  Kibwe Katibu wa “SHIVYAWATA” Temeke na Mwenyekiti wa Albino  akichangia maada Iliyokuwa ikiendelea katika uzinduzi wa Faridas foundation Wageni waalikwa wakifuatilia kwa umakini Uzinduzi wa Faridas Foundation Afisa Miradi wa Faridas Foundation Bw.Lumanus  akijadiliana Jambo Na Mkurugenzi Wa Faridas Foundation Bi Farida A.Sekimonyo

NIGERIA YARUDISHA MACHUNGU AFRIKA, YATANDIKWA 2-0 NA UFARANSA, YOBO AJIFUNGA GOLI LA HASARA!

  Paul Pogba akirudi juu na kupiga kichwa  akiifungia Ufaransa bao la kwanza dhidi ya Nigeria. NIGERIA maarufu kama Super Eagles imetupwa nje ya kombe la dunia baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Ufaransa usiku huu katika mchezo wa hatua ya 16. Paul Pogba aliifungia Ufaransa bao la kuongoza katika dakika ya 78, huku beki wa Nigeria,  Joseph Yobo akijifunga bao katika dakika za lala salama mjini Brasilia. Paul Pogba akinyosha vidole juu baada ya kuifungia Ufaransa .

Hawa ndiyo washindi wa tuzo za watu zilizotolewa siku ya jana

Tuzo za watu za Tanzania au Tanzania People’s Choice Awards zimetolewa Ijumaa hii kwenye ukumbi uliopo Serena Hotel jijini Dar es Salaam. Jumla ya vipengele 11 vilikuwa vinashindaniwa. Mshindi katika kila kipengele ameibuka na zawadi ya shilingi milioni moja pamoja na trophy. Host wa tuzo hizo alikuwa mtangazaji mkongwe wa radio, Jimmy Kabwe. WASHINDI 1. MTANGAZAJI WA REDIO ANAYEPENDWA Millard Ayo – Clouds FM 2. KIPINDI CHA REDIO KINACHOPENDWA Amplifaya – Clouds FM 3.MTANGAZAJI WA RUNINGA ANAYEPENDWA Salim Kikeke – BBC Swahili 4. KIPINDI CHA RUNINGA KINACHOPENDWA Mkasi – EATV 5. MWANAMICHEZO ANAYEPENDWA Juma Kaseja – Yanga 6. MUONGOZAJI WA VIDEO ZA MUZIKI ZINAZOPENDWA Nisher 7. VIDEO YA MUZIKI INAYOPENDWA YA MWANAMUZIKI WA KIUME My Number – Diamond 8. VIDEO YA MUZIKI INAYOPENDWA YA MWANAMUZIKI WA KIKE Yahaya – Lady Jaydee 09. MUIGIZAJI WA KIUME KWENYE FILAMU ANAYEPENDWA King Majuto 10. MUIGIZAJI WA KIKE KWENYE FILAMU ANAYEPENDWA Elizabeth ‘Lulu’ Michael 11. FILAMU INAYOPENDWA Ndo