Skip to main content

Posts

Showing posts from March 9, 2014

HUYU NDIYE MSANII WA KUIGIZA BONGO MWENYE SIFA YA PEKEE

Wastara Juma  Hii inatokana na jinsi anavyojituma kwenye kazi zake za sanaa na kuwa karibu na mashabiki wake jambo linalofanya azidi kupendwa kila kukicha Wakipiga stori baadhi ya mashabiki wake wanasema Wastara ni msanii anaeipenda kazi yake na sio mbaguzi wala hana majivuno yani ni mtu wawaatu “Unajua wastara ni tofauti na wasanii wengine yani pamoja nakua kwenye game kwa miaka mingi bado ashuki samani kila msanii anatamani kufanya nae kazi“

RAIS KIKWETE ASHIRIKI MSIBA WA MEJA JENERALI BAKARI SHAABANI

Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kwenye kitabu cha maombolezo nyumbani kwa aliyewahi kuwa mkuu wa kitengo cha maafa katika ofisi ya Waziri Mkuu Meja Jenerali Bakari Shaabani huko Ada Estate jijini Dar es Salaam jana.Marehemu amezikwa nyumbani kwao huko Unguja Zanzibar Jana. Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mjane wa aliyewahi kuwa mkuu wa kitengo cha Maafa katika ofisi ya Waziri Mkuu Meja Jenerali Bakari Shaabani nyumbani kwake Ada Estate jijini Dar es Salaam jana. Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima zake za mwisho mbele ya jeneza la aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha maafa meja Jenerali Bakari Shaabani nyumbani kwake Ada Estate jijini Dar es Salaam jana.Mwili wa marehemu ulisafirishwa jana kwenda Zanzibar na kuzikwa.(picha na Freddy Maro)

KATIBU MKUU WA WIZARA YA UCHUKUZI APOKEA MAGARI MAWILI KWA AJILI YA MAFUNZO YA UDEREVA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka (kushoto), akimsikiliza Mkuu wa Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT), Dkt. Zakaria Mganilwa ofisini kwake kabla ya kupokea magari mawili ambayo yamekabidhiwa kwa chuo hicho na Shirika la Transaid la nchini Uingereza, hafla ya kukabidhi magari hayo imefanyika leo asubuhi katika viwanja vya NIT. Taswira ya  tanker trailer la futi 40  na  Folk Lift  ambayo yamekabidhiwa kwa Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT) na Kampuni ya Transaid leo asubuhi katika viwanja vya chuo hicho. Magari hayo yatasaidia wanafunzi wanaosoma kozi za udereva chuoni hapo. Sehemu ya Wafanyakazi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), wakimsikiliza Mgeni Rasmi (hayupo pichani), wakati wa hafla fupi ya kukabidhi magari mawili kwa ajili ya kufundishia mafunzo ya udereva chuoni hapo, magari hayo yalimekabidhiwa leo asubuhi na Shirika la Transaid la nchini Uingereza.       Mkurugenzi wa Mradi ya Usalama Barabarani wa Shirika la Transaid la Nchini Uingere

HAYA HAPA MATUKIO BUNGE MAALUM LA KATIBA LEO MJINI DODOMA

Mjumbe wa bunge Maalum la Katiba Bw.  Augustino Mrema akimweleza jambo Mjumbe mwenzie Bw. Islaim Aden Rage leo Mjini Dodoma. Wajumbe wa Bunge Maalumla Katiba na Wajumbe wa kamati ya kuandaa rasimu ya kanuni zitakazotumika katika Bunge maalum la Katiba Bw. Prof. Costa Mahalu (Kulia) na Tundu Lissu wakielekea katika ukumbi wa bunge kwa ajili ya semina ya kuandaa kanuni zitazotumika katika bunge maalum la katiba, leo Mjini Dodoma. Wajumbe wa Bunge maalum la katiba Bw. Hamadi Rashidi (kushoto) Juma Alawi (katikati) na Thumwein Thuwein wakielekea katika ukumbi wa bunge kwa ajili ya semina ya kuandaa kanuni zitazotumika katika bunge maalum la katiba, leo Mjini Dodoma. Mjumbe wa Bunge maalum la katiba Bw. Ally Kessy akiwaeleza jambo jambo Wajumbe wenzie Bw. Edward Lowassa (katikati) na Almas Maige ndani ya ukumbi wa bunge leo mjini Dodoma. Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samwel Sitta (kulia) akimweleza jambo Waziri Mkuu

MAMA PINDA: WANAWAKE KUWENI NA NIDHAMU YA MATUMIZI YA FEDHA

MKE WA WAZIRI MKUU, Mama Tunu Pinda amewaasa wanawake nchini kwa kuwataka wawe na nidhamu ya matumizi ya fedha za mikopo wanayochukua kwa ajili kuendeshea miradi kama kweli wanataka kufanikiwa na kutimiza malengo waliyojiwekea. Ametoa wito huo jana jioni (Jumapili, Machi 9, 2014) wakati akifungua Tamasha la Wanawake (Women Dialogue Front -2014) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani lililofanyika kwenye hoteli ya JB Belmont, jijini Mwanza.   Akizungumza na washiriki wa tamasha hilo lililoandaliwa na asasi ya  Mikaela Women Empowerment Initiatives   ya jijini Mwanza, Mama Tunu Pinda alisema: “Japokuwa kwenye ujasiriamali kuna changamoto nyingi lakini kuna wenzenu walioweza kufanikiwa. Hivyo nina imani kubwa kuwa nanyi mtafanikiwa, ili mradi muwe na nia ya dhati katika kutekeleza malengo mliyojiwekea.” Akisisisitiza haja ya kuwa na uthubutu kwenye ujasiriamali, Mama Pinda alisema: “…Lakini niwatake wanawake wenzangu kuwa wajasiri na wenye kuthubutu na kuwa na m

HAYA NDIYO MAMBO SITA USIYOYAFAHAMU KUHUSU NDEGE YA MALAYSIA ILIYOPOTEA

Ndege ya shirika la ndege la Malaysia (Malaysia Airlines). Kuna mambo ambayo watu hawajafahamishwa kuhusu ndege ya shirika la ndege la Malaysia (Malaysia Airlines) safari namba Flight 370 ambayo imepotea ikiwa eneo la juu ya bahari katika Ghuba ya Thailand na watu 239. Ndege hiyo aina ya Boeing 777  iliyopotea Jumamosi asubuhi wiki iliyopita na kutoonekana mpaka leo imewababaisha wataalam wengi duniani wa mambo ya usalama wa vyombo vya anga. Muonekano wa ndani wa Ndege ya shirika la ndege la Malaysia. Hata hivyo, pamoja na mkanganyiko huo, gazeti la Wall Street Journal limeorodhesha mambo ambayo watu wengi hawayafahamu kuhusiana na kupotea kwa ndege hiyo. Mambo hayo ni yafuatayo: Ndege zote za Boeing 777 zina kisanduku maalum cha kutunza kumbukumbu za mawasiliano ya marubani wa ndege na waongoza ndege walioko ardhini (black box) ambacho hakiwezi kuharibika katika mlipuko wowote unaoweza kutokea kwenye ndege. Kijisanduku hicho (black box) kina nguvu za kurusha mawimbi ku