Kuna mambo ambayo watu hawajafahamishwa kuhusu ndege ya shirika la ndege la Malaysia (Malaysia Airlines) safari namba Flight 370 ambayo imepotea ikiwa eneo la juu ya bahari katika Ghuba ya Thailand na watu 239.
Ndege hiyo aina ya Boeing 777 iliyopotea Jumamosi asubuhi wiki iliyopita na kutoonekana mpaka leo imewababaisha wataalam wengi duniani wa mambo ya usalama wa vyombo vya anga.
Hata hivyo, pamoja na mkanganyiko huo, gazeti la Wall Street Journal limeorodhesha mambo ambayo watu wengi hawayafahamu kuhusiana na kupotea kwa ndege hiyo.
Mambo hayo ni yafuatayo:
- Ndege zote za Boeing 777 zina kisanduku maalum cha kutunza kumbukumbu za mawasiliano ya marubani wa ndege na waongoza ndege walioko ardhini (black box) ambacho hakiwezi kuharibika katika mlipuko wowote unaoweza kutokea kwenye ndege.
- Kijisanduku hicho (black box) kina nguvu za kurusha mawimbi kuonyesha kilipo kwa siku zisizopungua 30 baada ya kuanguka baharini.
Hata hivyo, wataalam wameshindwa kunasa mawimbi ya chombo hicho na hivyo kuwa na wasiwasi kwamba huenda kimeharibiwa na nguvu kubwa isyokuwa ya kawaida.
- Sehemu nyingi zilizoharibika za ndege huwa zinaelea juu ya maji baada ya ndege kuanguka baharini au majini.
Katika tukio hili hakuna kilichoonekana, na hivyo kuzua hofu kwamba ndege hiyo huenda imetoweka katika eneo la Dunia.
- Iwapo kombora lingeipiga ndege hiyo, basi kombora hilo lingeonekana katika vyombo vya uchunguzi vya kijeshi na vya usalama wa safari za anga. Hii ni pamoja na kwamba huenda imepigwa na kombora na kuikatakata ndege hiyo katika vipande vidogo-vidogo.
Katika nadharia hii, hakuna dalili zozote zilizonaswa na vyombo vya ulinzi na usalama kuonyesha kulikuwa na kombora lililohusika.
- Pamoja na eneo ambalo ndege hiyo ilikata mawasiliano na kupotea kufahamika, bado wataalam wameshindwa kujua iko wapi.
Kufahamu eneo la tukio, mwelekeo na kasi ya ndege hiyo, bado hakujasaidia kupatikana kwa ndege hiyo, hivyo kuzidisha hofu inayowachanganya wataalam.
- Iwapo Flight 370 ilitekwa, isingeacha kuonekana kwenye vyombo vya kudadisia nyendo za vyombo vya angani (radar).
Nadharia ya kutekwa haina msingi wowote, kwani ndege zinazotekwa huwa hazitoweki katika radar.
HITIMISHO: Ndege hiyo ya Boeing 777 haikulipuka angani, bali imetoweka!
Comments
Post a Comment