Ikulu ya Rais iliwahi pia kushambuliwa mwezi Februari Vikosi vya serikali Somalia vimefanikiwa kuidhibiti upya ikulu ya rais katika mji mkuu Mogadishu baada ya wapiganaji wa Al Shabaab kuishambulia. Maafisa wanasema washambuliaji wapatao watano kutoka kundi la al-Shabab - waliuawa walipoingia katika eneo la ikulu hiyo. Taarifa zinazohusiana Somalia Washambuliaji hao wanadaiwa kulipua bomu lililotegwa kwenye gari karibu na langu kuu la Ikulu hiyo. Waziri wa habari wa Somalia Mustaf Dhuhulow Waziri wa habari na mawasiliano wa Somalia Mustaf Dhuhulow ameambia BBC kuwa tayari mmoja wa washambuliaji hao amekamatwa na anahojiwa na polisi. Waziri Mustaf amesema, '' Walishambulia ikulu