WATU 8 WAJERUHIWA NA BOMU
NA Ferdinand Shayo, ARUSHAWATU wanne ambao ni raia wa Asia wamejeruiwa vibaya na kitu
kinachiosadikiwa kuwa ni bomu wakati wakila katika Hotel ya Wama iliyopo
maeneo ya Gymkhana Jijini Arusha.
Tukio hilo limetokea majira ya saa 4 usiku ambapo bomu hilo lililotupwa kwa
mkono na watu wasio julikana na kuwajeruhi watu hao ambapo mmoja
amejuruhiwa vibaya na amewekwa katika chumba cha uangalizi katika
Hospitali ya Seliani Arusha.
Akizungumza na waandishi wa habari kaimu Mganga mkuU wa hospitali ya
seliani Dr Paulo Kisanga alisema kuwa hospitali hiyo iliyopokea majeuhi
8,wanaume 5 wanawake 3 na wamejeruhiwa katika maeneo miguu na majeruhi
mmoja amekatwa mguu mmoja na hali yake bado ni mbaya.
Dr Kisanga aliwataja majeruhi hao kuwani Vinod Sureshi,Rutwik Khamd
Val,Raji Rajin,Prateek Saveq,Manc Gumpka,Manisha Gupta,Mahushi Gupta na
Deepale Gupta wote walikuwa raia wa Asia.
Kwa upande wake mbunge wa jeshi maalumu Mkoa wa Arusha Mh Catherine Magiye
alisema kuwa vitendo vya Milipuko ya mabomu vinaendelea kutokea katika
Mkoa wa Arusha vinatishia kuwepo kwa hali ya amani pamoja na kutishia
maisha ya wageni wanaokuja kutalii hapa nchini.
Aidha Mh. Magiye aliwataka wakazi wa Jiji la Arusha kuwa watulivu sambamba
na na kuhirikiana na jeshi la polisi ili kuwabaini watu wanaohusikana
matukio hayo ambapo pia wameomba Serikali kuchukua hatua za haraka
kuondoa majanga hayo kwani inaonyesha kuwa serikali haijachukua hatua
stahiki.
Naye Amanda wa polosi mkoa wa Arusha ASCP Liberatus Sabasi alias kuwa yeye
hawezi kuzngumzia tukio hilo lakini limeshathibitishwa na mkuu wa makosa ya
jinai Nchini Bwana Isaya Mwigulu.
Hata hivyo mlipuko huo wa bomu umetokea sikuchache baada ya kutokea mlipuko
mwingine mmnamo tarehe 3/8 mwaka huu eneo la majengo ya chini jijini Arusha
na kumjeruhi kiongozi wa taasisi ya AnswaarMuslim Youth Center kanda ya
kaskazini ShekhSud Ally Sudi na Muhaj Huseni 38 wakati wakijiandaa kula
daku nyumbani kwao.
HABARI PAMOJA NA PICHA NI KWA MUJIBU YA MUHANDISHI WETU Ferdinand Shayo, ARUSHA
Comments
Post a Comment