Skip to main content

Posts

Showing posts from September 1, 2013

Siri 20 usizozijua za kufurahia mapenzi

              NI Jumatano nyingine tena imewadia marafiki zangu ambapo tunakutana katika uwanja wetu ule ule wa kupeana darasa hili maridhawa. Ninaamini mtakuwa wazima wa siha njema na mpo tayari kupokea kile nilichowaandalia kwa wiki hii. Karibuni. Ndugu zangu, kuna mambo mengi sana yanazunguka, ambayo yanatakiwa kufanywa ili mtu aweze kufurahia mapenzi na mwenzake. Wakati mwingine kuna vitu ambavyo tunavikosea bila kufahamu, matokeo yake vinaleta matatizo kwenye ndoa hapo baadaye. Leo nataka kukupa siri muhimu ishirini ambazo kwa hakika kama ukizizingatia, kwako mapenzi yatakuwa burudani ya aina yake. Huwezi kulia asilani katika maisha yako kwa sababu utakuwa umeshajua cha kufanya. Ukweli ni kwamba, baadhi ya matatizo ambayo yanakuwepo kwenye ndoa, husababishwa na mwanzo mbaya wa wahusika, wakati walipokutana na kuamua kuanzisha uhusiano. Wengi hawafikirii kuhusu hili, lakini ndiyo ukweli wenyewe. Hata kama upo kwenye ndoa, usiwe na shaka, mada hii ni kwa ajil

Linex amwagana na DEMU wake wa Kizungu...kisa ni Pesa na Muziki.

Kilichokua kinafata ni ndoa ambayo ilikua imepangwa na wote wawili baada ya Linex kukamilisha hatua muhimu ambayo ni kumvisha pete mchumba wake anaitwa Suvi raia wa Finland mwezi March 2013. Millardayo amepata nafasi ya kuzungumza na Linex  kwenye exclusive interview ambayo amekiri ni kweli imebidi kila mmoja aendelee na maisha yake na mapenzi yao kuisha kwa sababu kadhaa zilizojitokeza. Sababu kubwa ni Suvi kutaka Linex ahamie Finland moja kwa moja na kwenda kuanza maisha mengine kwenye hiyo nchi ambayo ndio ingekua mara yake ya kwanza kufika, namkariri Linex akisema ‘kwa nia nzuri kabisa imekua ngumu kwangu kukubali hayo maamuzi, nataka kuendelea kufanya muziki wangu nyumbani’ ‘Tayari nimetumia miaka zaidi ya 10 kutengeneza jina langu kwenye muziki hapa Tanzania, bongo mimi naishi vizuri na familia yangu naisaidia… sina tatizo la kuhangaikia maisha kwa kiasi hicho cha kwenda kuanza tena, yani ni sawa na mtu ameshaanza chuo mwaka wa kwanza alafu mtu anata

Polisi na Mawaziri wadaiwa kujihusisha na biashara haramu ya NGONO

BAADHI ya mawaziri na polisi wametajwa kuwa ni wateja wakubwa wa wanawake wanaouza miili yao, maarufu kwa jina la Changudoa. Hayo yameelezwa jana na Jukwaa la Wanaharakati Wanawake Vijana (YFF), walipokuwa wakiwasilisha ujumbe wao kwa njia ya sanaa ya ngonjera, katika tamasha la 11 la Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) linaloendelea eneo la Mabibo jijini Dar es Salam. Wanaharakati hao wanawake vijana, walisema tatizo liko kwenye jamii ambayo inawahukumu changudoa bila kujiuliza kuwa wateja wao ni kina nani. ‘’… jamani hebu tuulizane, kwani changudoa mteja wake nani? Kwa taarifa yako, mawaziri, wabunge na mapolisi wamo; na hii ni changamoto kwa jamii,’’ walisema wanaharakati hao.   Akizungumza na Tanzania Daima baada ya kutoka jukwaani, kiongozi wa wanaharakati hao, Aisha Kijavala, alisema wameamua kutoa ujumbe huo kwa washiriki wa tamasha hilo ili jamii ijue wateja wa changudoa hao. Alisema wateja hao wakiacha kununua ngono, pia wanawake wanaouza miili yao, wataac

Ripoti maalumu ya gazeti la MWANANCHI kuhusu vurugu zilizotokea jana bungeni

  Jana, Bingwa wa Dunia wa uzani wa kati (super middle), unaotambuliwa na Shirikisho la Ngumi Duniani (WBF), Francis Cheka alitembelea Bunge baada ya kutwaa taji hilo karibuni na jana hiyohiyo, Bunge hilo lilishuhudia ngumi kavukavu katika vurugu kubwa pengine kuliko zote zilizowahi kutokea katika ukumbi wake. Katika masumbwi hayo yasiyo rasmi, Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ anadaiwa kumpiga kichwa Askari wa Bunge na kumchania sare na kung’oa kipaza sauti. Mbilinyi jana alisema alikuwa anatafutwa na polisi huku akisema hilo limemshangaza akidai kwamba yeye ndiye aliyeshambuliwa na askari huyo. Vurugu hizo zilitokea baada ya Naibu Spika, Job Ndugai kuamuru kutolewa nje kwa Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe. Katika vurugu hizo Mbilinyi alibebwa juujuu na polisi hadi nje ya ukumbi huku ak

Wananchi walilaani Bunge la Tanzania kutokana na vurugu zinazoendelea

Baada ya kuibuka mvutano mkali bungeni jana, kati ya Naibu Spika, Job Ndugai na wabunge wa Kambi ya Upinzani, wasomi, wanaharakati, Chama cha Madaktari Tanzania (Mat), Chama cha Walimu Tanzania (CWT) na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), vimesema kinachoendelea sasa ndani ya Bunge ni masilahi ya vyama vya siasa siyo taifa. Walitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya Naibu Spika, Job Ndugai kuwataka askari kumtoa nje ya Ukumbi wa Bunge, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe. Mbowe aligoma kukaa chini na kuungwa mkono na wabunge wa upinzani, akishinikiza kuahirishwa kujadiliwa kwa Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, hadi hapo Zanzibar itakaposhirikishwa, muda mfupi baada ya wabunge kupiga kura na 156 kutaka ujadiliwe na 56 wakitaka uondolewe. Wabunge hao wa upinzani kutoka vyama vya Chadema, CUF na NCCR- Mageu

HIZI NDIZO SIFA ZA "MWANAUME ANAYETAKA KUWA SERIOUS NA WEWE" NA "MWANAUME ANAYEKUCHEZEA''

ATAKAYEKUOA SIFA ZAKE NI KAMA IFUATAVYO... 1. ANABADILIKA  Mwanaume Ambaye Ana Malengo Ya Kuoa Hubadilika Kitabia. Muda Mwingi Hutaka Kuonekana Mtu Mzima Mwenye Sifa Nzuri. Hatakuwa Mtu Wa Kulewa Kupita Kiasi Na Kutapanya Mali Na Wanawake Wengine. Tabia Zake Mbaya Za Zamani Ataziacha Kisa Cha Mabadiliko Hayo Kinatajwa Na Wataalamu Wa Masuala Ya Ndoa Kuwa Ni Pamoja Na Kumshawishi Mwanamke Aliyemchagua Aitikie Mwito Wa Kuwa Pamoja Katika Maisha. Lakini Pia Ni Kuwapa Kielelezo Chema Ndungu Au Wazazi Wake Wamuunge Mkono Katika Harakati Zake Za Kuoa. 2. ATAONGEZA JITIHADA ZA KUJITEGEMEA Mara Nyingi Wanaume Walio Makini Na Tayari Kufunga Ndoa, Wanahitaji Kuwa Na Kipato Cha Kutosha Kuweza Kuwahudumia Wake Zao Na Familia Ambazo Watakuwa Nazo Hapo Baadaye Hivyo Wanajitahidi Kutafuta Njia Za Kupandisha Hali Yao Kiuchumi. Kama Ni Muajriwa Anaweza Akaanza Kutafuta Miradi Mingine Nje Ya Kazi Yake Ili Imsaidie Kuongeza Kipato Cha Kujikimu Na Hali Ya Maisha. Kama Alikuwa A

Wabunge wa Chadema, NCCR-Mageuzi na CUF watoka nje

  Wabunge wa Vyama vya CUF, NCCR-Mageuzi, na Chadema wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge kupinga muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba bungeni dodoma jana.Picha na Fidelis Felix Dodoma.Wabunge wa Kambi ya Upinzani Bungeni jana jioni walitoka ndani ya Ukumbi wa Bunge, baada ya kupuuzwa kwa mwongozo wao wa kutaka kuahirishwa kujadiliwa kwa Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, hadi hapo Zanzibar itakaposhirikishwa. Wabunge waliotoka bungeni jana yapata saa 12.15 ni kutoka vyama vya Chadema, CUF na NCCR- Mageuzi huku Mbunge wa Vunjo na Mwenyekiti wa Taifa wa Tanzania Labour Party (TLP, Augustine Mrema akiendelea kubaki ukumbini. Kitendo cha wabunge hao wa upinzani kilionekana kuwakera baadhi ya wabunge wa CCM, ambao walisikika wakiwakejeli kwa kupiga meza huku wakisema: “Kwendeni zenu, tumewazoea.” Wakati wabunge hao wakiondoka, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, alikuwa akiwasisitiza wabunge wanaobakia wawe watuliv

SHINDANO JIPYA LA TANZANIA TOP MODEL LAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM

BOLT AMFAGILIA FELLAINI, ASEMA ATANG`ARA MAN UNITED, AWATAKA MASHABIKI KUMPA SHAVU LA NGUVU!

BINGWA wa kukata upepo katika riadha, Usain Bolt amewataka mashabiki wa Manchester United kuwa nyuma ya  Marouane Fellaini na kumuunga mkono kwa hali ya juu mara tu atakavaa jezi nyekundu ya Old Trafford. Nyota huyo anayeshikilia rekodi ya dunia  katika mbio za mita 100 na 200 ,  na shabiki mkubwa wa United alisema hayo huku akishikilia jezi ya timu ya taifa ya Ubelgiji yenye jina la Fellaini mgongoni. Hii imekuja muda mfupi tu tangu Bolt amtake kocha wa Man United, David Moyes kusajili kabla ya dirisha la usajili la majira ya kiangazi kufungwa. Shabiki wa kufa wa United: Usain Bolt akionesha jezi ya timu ya taifa ya Ubelgiji yenye jina la Marouane Fellaini mgongoni “David Moyes, tunahitaji kiungo mjuzi, ambaye anaweza kupiga pasi na kutengeneza nafasi, mwenye uwezo mkubwa kumiliki mpira na mtu thabiti, tunataka muda huu”. Alisema Bolt akimuambia kocha wa Man United. Lakini baaada ya Fellaini kusajiliwa, labda Bolt ametulizwa moyo kwa ushabiki wake wa soka. Pia

OZIL AWACHANGANYA WACHEZAJI MADRID, RONALDO AONGOZA MGOMO KWA KUMPOTEZA MJERUMANI FUNDI!

MCHEZAJI ghali zaidi Duniani, Gareth Bale hajagusa hata nyasi za Bernabeu baada ya kuvunja rekodi ya Dunia ya usajili kwa dau la pauni milioni 86, lakini shida zimeshaanza katika chumba cha kubadilishia nguo katika klabu ya Real Madrid. Thamani ya Mesut Ozil kwa wachezaji wenzake wa Real Madrid ilionekana jumatano jana wakati wachezaji walikuwa wanapiga kelele za kumkubali huku wakisema  haina shida Bale atarithi mikoba yake. Kwa upande wa nyota wa Ureno na klabu hiyo, Cristiano Ronaldo amenyong`onyea baada ya kumpoteza Ozil, wakati huo huo nao  Alvaro Arbeloa, Isco na hata nyota wa wapinzani wao, FC Barcelona, Cesc Fabregas wamekerwa na kitendo cha Mjerumani huyo mwenye kipaji cha juu kuondoka ligi ya Hispania. Hasira: Cristiano Ronaldo ameripotiwa akilaumu mbele ya wanandinga wenzake wa timu ya taifa ya Ureno kuwa amechukizwa na kuuzwa kwa Mesut Ozil Akiongoza mazoezi: Ronaldo, akifanya mazoezi na timu ya taifa ya Ureno, na ana amini Ozil alikuwa mpikaji mzu

MNYAMA KUJIPIMA UBAVU NA KMKM KESHO TAIFA….MCHAKATO WA KATIBA WASHIKA KASI KIDIJITALI ZAIDI, MASHABIKI KUTUMA MAONI KWA E-MAIL!!

Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe, Mbeya WEKUNDU wa Msimbazi, Simba  wanatarajia kushuka dimbani katika mchezo wa kirafiki utakaofanyika kesho Ijumaa, Septemba 6 mwaka huu dhidi ya mabingwa wa soka wa Ligi Kuu ya visiwani Zanzibar, KMKM, Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa taarifa iliotolewa na Afisa habari wa klabu ya Simba, Ezekiel Kamwaga inafafanua kuwa lengo kuu la mechi hiyo ni mazoezi ya klabu hiyo kujiandaa na mchezo wake wa ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya Mtibwa Sugar,  Septemba 14 mwaka huu uwanja wa Taifa.  “Kikosi kamili cha KMKM kimewasili mjini Dar es Salaam tayari na leo saa tano na nusu kamili nahodha wake, Abdi Kassim Babi na kocha mkuu wa timu hiyo wanatarajiwa kuzungumza na waandishi wa habari katika mgahawa wa City Lounge katikati ya jiji”. Alisema Kamwaga. Kamwaga ameongeza kuwa Simba inaendelea na mazoezi yake jijini Dar es salaam na wachezaji wake wote wapo katika hali nzuri na tayari kwa ajili ya mechi hiyo. Afisa hab

HIZI HAPA PICHA ZINAZONESHA JINSI VURUGU ILIVYOTOKEA BUNGENI LEO

Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akijibu maswali Bungeni mjini Dodoma  Septemba 5, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, William Lukuvi akiteta na Mwanaheria  Mkuu wa Serikali, Frederick Werema, bungeni Mjini Dodoma Septemba 5, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai akimwamuru Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe kukaa chini, Bungeni Mjini Dodoma Septemba 5, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, William Lukuvi  akifafanua jambo Bungeni Mjini Dodoma Septemba 5, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mbunge wa Bumbumbuli na Naibu waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Tekinolojia, January Makamba, Bungeni Mjini Dodoma Septemba 5,2013. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu) Wabunge wa Chadema wakiwa wamesimama kukaidi amri ya Naibu spika, Job Ndugai ya kuwataka wakae chini

KOCHA JKT OLJORO AWAKANDIA UBINAFSI WAO, ASEMA KWA SERA ZAO WATABAKI KUWA WASHIRIKI TU WA LIGI KUU!!

Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe, Mbeya Tabia ya baadhi ya watu kuendekeza hila, fitina na tamaa ndio chanzo cha kumaliza soka la klabu za Tanzania kuanzia ligi za chini mpaka ligi kuu. Hayo yemesemwa na aliyekuwa kocha wa JKT Oljoro, Riziki Shawa ambaye kwa sasa amebwaga manyanga ambapo amesema wakati ikifundisha klabu hiyo kuna baadhi ya watu walikuwa na tamaa na kutaka kuendesha timu watakavyo wao. “Kuna watu wanajifanya ile timu wanaijua sana, kuna watu wana tamaa sana, kutoka ukatibu mkuu mtu anataka ukocha mkuu, soka haliko hivyo, na hawatafanikiwa kwa misingi hiyo”. Alisema Riziki. Riziki alisema kwasababu wao ni wanajeshi, basi wanataka kuendesha timu wenyewe kwa wenyewe na wanaamini wanaweza kufanikiwa kwa haraka, jambo ambalo ni sumu sana kwa klabu ya soka. “Pia kuna wakati wanaendekeza ukabila, kwasababu mkubwa ni kabila lake, basi wanataka kubebana na kuendesha klabu watakavyo”. Alisisitiza Riziki. Riziki aliongeza kuwa kila binadamu anataka sifa,

Daktari FEKI akamatwa katika hospitali ya KCMC Moshi

  Hali ya wasiwasi imejitokeza kwa baadhi ya wagonjwa wanaopatiwa huduma za  matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC Moshi Kilimanjaro baada ya uongozi wa hospitali hiyo kumkamata mtu anayejifanya kuwa ni daktari wa watoto akiwa kwenye wodi ya upasuaji. Daktari huyo feki aitwae Alex Sumni Massawe amewekwa chini ya ulinzi na Jeshi la Polisi baada ya kukutana na mmoja wa wagonjwa ambae alimuahidi kumfanyia mwanae wa kiume upasuaji wa ngozi.   Alex anadaiwa kutaka kumfanyia upasuaji kijana MAKASI TIPESA mkazi wa Manispaa ya Moshi ambae amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya ngozi kwa muda mrefu sasa. Afisa Uhusiano wa Hospitali ya KCMC Gabriel Chisseo amesema daktari  aliwekewa mtego na uongozi wa hospitali hiyo kutokana na baadhi ya wagonjwa kuripoti kutapeliwa na mmoja wa madaktari ambae amekuwa akijinadi kwamba anafanya huduma hiyo hospitalini hapo. Chisseo anasema ‘Katika jitihada za wazazi kumuokoa mtoto wao wakawa wamewasiliana na mtu mmoja mtaani a

Mheshimiwa SUGU anasakwa na polisi kwa kosa la kuwakashifu walinzi wa Bunge

  Taarifa kutoka Dodoma zinadai kuwa kuna Askari mmoja ambaye ni miongoni mwa walinzi wa Bunge ameenda kufungua faili Polisi Dodoma na kusema kuwa ametishiwa kupigwa na Mbunge Sugu... Baada ya kufungua Jalada hilo polisi wamechukua Difenda 6 na wameingia mitaani kumtafuta ili awekwe ndani mpaka kesho ndio afikishwe mahakamani asubuhi

"Mbowe ni Mjinga na Mpuuzi"...Hii ni kauli ya Kigwangalla bungeni

  Mbunge wa Nzega Dr. Kigwangalla, ametumia muda wake karibu wote wa kuchangia Muswada wa Katiba kwa kumshambulia Mwenyekiti wa CHADEMA, Mhe. Mbowe kuwa ni Mjinga, Mpuuzi, ametia aibu aibu  Kigwangalla  amempongeza  Naibu  Spika  kwa  kumtimua  Mbowe  bungeni  na  kusema  kuwa  kitendo  hicho  kimemshikisha  adabu... Aidha, mbunge  huyo  wa  Nzega amedai kuwa Mbowe sio Mchaga bali ni mhuni fulani  aliyejivika  sura  ya  Uchaga  kwa  masilahi  yake  binafsi !. Kigwangalla  alihitimisha  mchango wake  kwa  kudai  kuwa wapinzani wana akili za shetani  zisizovumilika!

Tazama Picha tano za Rais Kikwete alipokutana na Kagame wa Rwanda huko Uganda

Rais Jakaya Kikwete leo amefanya mazungumzo na Rais Paul Kagame wa Rwanda katika mkutano wa saba wa kimataifa wa nchi za maziwa makuu, unaofanyika Kampala, Uganda. Haijafahamika mara moja walichozungumza, hizi ni picha za mkutano wao. Marais hao wamekutana wakati ambapo uhusiano kati ya nchi hizo mbili unaendelea kuzorota

Sean Kingstone ashitakiwa kwa kumbaka mtungo msichana mwenye miaka 20

Sean Kingston na walinzi wake (Bodyguard) wamemla mtungo msichana (20) aliekuwa amelewa, katika chumba cha Hoteli, 2010. Carissa Capeloto  ambae kwa sasa ana miaka 22,  anadai  kulazimishwa kufanya ngono na Sean, walinzi wake na member wa bendi ya Sean katika hoteli iliyoko Seattle, Julai, 2010, baada ya yeye kuvuta bangi na kufuta shots 7-10 za vodka. Capeloto - ambaye amewashitaki watu wote 3, anadai alialikwa katika chumba cha hoteli hiyo na Kingston kwa kukutana-na-kusalimiana (meet and greet) kufuatia tamasha la Bieber, ambapo Kingston pia alikuwa aki- perform, lakini wakati alipofika chumbani, Kingstone alikuwa ameshatupa kule kila kilichokuwa mwilini mwake (naked) yuko juu ya kitanda akimsubiri Capeloto amedai kuwa mlinzi alimnyanyua na kumuweka juu ya Kingston, na wote watatu waliendelea  kumbaka wakati yeye alikuwa "ni wazi amelewa, na kutokuwa na uwezo wa kutoa ridhaa." Capeloto anasema rafiki yake baadaye aliingia katika chumba na kumu

Drake kumshirikisha baba yake mzazi kwenye album yake "Nothing Was The Same"

Ikiwa siku za kuachia album yake "Nothing Wa The Same" zinakaribia (Sep 24), habari zaidi zinazid kutoka. Habari zilizoenea sasa ni kuwa Drake atamshirikisha baba yake mzazi kwenye ngoma ambayo itakuwa ni bonus kwenye album hiyo " Heat of the moment." “Naishi katika ndoto za baba yangu. Baba yangu alitaka kuwa muimbaji maarufu, kulikuwa na interview zingine ambazo waliniuliza kuhusu baba yangu, na sikutaka kuongelea kuhusu hilo, na kuna ngima ambazo sijamfanya baba yangu kuonekana ni mtu mkubwa, mwisho wa siku, baba yangu anajua kuwa nampenda na kuwa ni rafiki yangu mkubwa." amesema Drake. Bado haijawekwa wazi kama baba mzazi wa Drake, Dennis Graham ataimba kwenye ngoma hiyo au sauti yake tu ndio itakayoskika kama sample, kama kwenye ngoma ya zamani ya Drake  “Jodeci Freestyle” aliyomshirikisha J. Cole

KALAMA NYILAWILA AJIFUA KUMTAFUTA THOMAS MASHALI!

Bondia Kalama Nyilawila akijifua kujimalisha kusubili mpambano wake yeyer na Thomasi Mashari baada ya kumdhiaki yeye pamoja na Bondia mada Maugo aliyepigwa hivi karibuni kwa kuwaita midori yake Picha na  www.superdboxingcoach.blogspot.com Bondia Kalama Nyilawila akijifua kujimalisha kusubili mpambano wake yeyer na Thomasi Mashari baada ya kumdhiaki yeye pamoja na Bondia mada Maugo aliyepigwa hivi karibuni kwa kuwaita midori yake Picha na  www.superdboxingcoach.blogspot.com Bondia Kalama Nyilawila kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Shadrack Ignas wakati wa mazoezi yanayoendelea katika klabu yao iliyopo sinza makaburini Dar es salaam Kalama anafanya mazoezi kwa ajili ya kumtafuta bondia Thomasi Mashali baada ya kumdhiaki kwa kumuita yeye na mwenzie Mada Maugo kuwa ni Midori yake ambapo maugo amepigwa na bondia huyo hiv

SERIKALI YAJIBU MAPIGO KWA MTANDAO WA KENYA ULIOANZA KUICHOKONOA TANZANIA

Msemaji wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari- (MAELEZO) Assah Mwambene  akizungumza  na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam   kuhusu  mtandao wa kijamii wa nchini Kenya ulioituhumu  Serikali ya Tanzania.  -------------- Na Fatma Salum-MAELEZO   SERIKALI  ya Tanzania imetoa ufafanuzi kuhusu tuhuma mbalimbali dhidi yake zilizotolewa na mtandao wa kijamii wa nchini Kenya ujulikanao kama   www.standardmedia.co.ke  unaosadikika kuendeshwa na kampuni ya gazeti la The Standard la nchini humo.   Akizungumza  na waandishi wa habari leo  jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari- (MAELEZO) Assah Mwambene , alisema mtandao huo umeripoti kuwa  Serikali ya Tanzania imekataa kuiuzia Kenya gesi asili ya Songosongo jambo ambalo halina ukweli  kwa kuwa  gesi inayozalishwa hivi sasa bado haijafikia kiasi cha kuweza kuuzwa nje ya nchi.   Mtandao huo pia umeripoti kuwa Serikali ya Tanzania ilikataa viwanja vyake vya n

AFISA UTUMISHI WA MANISPAA YA ILEMELA AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA RUSHWA YA NGONO

   Afisa  utumishi  wa  manispaa  ya  Ilemela  ndugu Songoma  leo  amefikishwa  mahakamani  akikabiliwa  na  kesi  ya  rushwa  ya  ngono  kwa  mwalimu  aliyekuwa  akiomba  kuhamishwa  toka  Ngudu  kuja  Mwanza. Akisomewa  shitaka  lake   mbele  ya   hakimu  mfawidhi  wa  mahakama  ya  Mwanza, ofisa  wa  TAKUKURU  Bi. Debora amedai  kuwa   Songoma  alitenda   kosa  hilo  may  tano  mwaka  jana  ambapo  maofisa  wa  TAKUKURU  walifanikiwa  kumtia  mbaroni  wakati  akijiandaa kupokea  rushwa  ya  ngono ndani  ya  gesti  moja  jijini  mwanza  katika  mtego  ambao  uliandaliwa  na  mwalimu  huyo. Hata  hivyo, Afisa  huyo  amekana  shitaka  hilo  na  kesi  yake  imeahirishwa  hadi  septemba  13  mwaka  huu

MAITI YAFUKULIWA NA KUTUPWA NJE YA MGAHAWA JIJINI MWANZA

Jeneza la mwili wa mtoto ambalo lilikutwa limetelekezwa mbele ya mlango wa mgahawa wa Ester. --- JENEZA lenye mwili wa mtoto mchanga, limezua taharuki kwa wananchi na wakazi wa Mtaa wa Ihago, Kata ya Mahina, Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza. Tukio hilo la kushangaza na la aina yake, lilitokea Agosti 29, mwaka huu, majira ya saa 12:00 asubuhi baada ya kugunduliwa na mfanyabiashara Ester Musa (28) likiwa limetelekezwa kwenye mlango wa mgahawa wake.   Jeneza likiwa limefungwa tayari kwa kwenda kuzika mara ya pili. -- Jeneza hilo linaaminika kufukuliwa na watu wasiofahamika kwenye moja ya makaburi eneo la Mahina jijini hapa. Akizungumza kuhusiana na tukio hilo, Ester anayemiliki na kuendesha mgahawa alisema, alifika katika eneo lake hilo la biashara, ghafla akapigwa na mshangao baada ya kuona jeneza likiwa mbele ya mlango wa mgahawa wake. Umati wa watu uliofika kushuhudia tukio hilo. “Nashindwa kujua nini maana ya tukio hili sababu hivi kari