KOCHA JKT OLJORO AWAKANDIA UBINAFSI WAO, ASEMA KWA SERA ZAO WATABAKI KUWA WASHIRIKI TU WA LIGI KUU!!
Tabia
ya baadhi ya watu kuendekeza hila, fitina na tamaa ndio chanzo cha
kumaliza soka la klabu za Tanzania kuanzia ligi za chini mpaka ligi kuu.
Hayo
yemesemwa na aliyekuwa kocha wa JKT Oljoro, Riziki Shawa ambaye kwa sasa
amebwaga manyanga ambapo amesema wakati ikifundisha klabu hiyo kuna
baadhi ya watu walikuwa na tamaa na kutaka kuendesha timu watakavyo wao.
“Kuna
watu wanajifanya ile timu wanaijua sana, kuna watu wana tamaa sana,
kutoka ukatibu mkuu mtu anataka ukocha mkuu, soka haliko hivyo, na
hawatafanikiwa kwa misingi hiyo”. Alisema Riziki.
Riziki
alisema kwasababu wao ni wanajeshi, basi wanataka kuendesha timu
wenyewe kwa wenyewe na wanaamini wanaweza kufanikiwa kwa haraka, jambo
ambalo ni sumu sana kwa klabu ya soka.
“Pia
kuna wakati wanaendekeza ukabila, kwasababu mkubwa ni kabila lake, basi
wanataka kubebana na kuendesha klabu watakavyo”. Alisisitiza Riziki.
Riziki
aliongeza kuwa kila binadamu anataka sifa, ila mpira unatakiwa kuucheza
kwanza na baadaye uje kuufundisha, lakini kwa Tanzania watu hawajacheza
mpira na wanang`ang`ania kufundisha timu kubwa na wanashindwa
kufanikiwa.
“Kuna
makocha ambao ni bora sana, kocha anatakiwa kuwa mfano, ukiangalia
uwezo alionao kocha Mbwana Makata aliyeaacha kazi JKT Oljoro ni bonge la
kocha, tulifanya kazi nzuri, lakini kutokana na tamaa zao na kumfanyia
majungu akaamua kuondoka”.
Riziki
alisema ametoa mchango mkubwa sana katika maendeleo ya klabu hiyo,
lakini leo hii wanaona hana jipya na wanashindwa kumthamini kutokana na
urasimu wao, na kwa misingi hiyo hawatafanikiwa.
“Kwa
sera zao, hila zao, fitina zao, majungu yao na kubebana kwao kutawafanya
kuwa washiriki tu wa ligi kuu, mafanikio yatakuwa ni ndoto kwao”.
Riziki alipigilia msumari wa moto.
Akizungumzia
mipango yake, Riziki amesema kwa sasa anapumzika, lakini kuna timu
zimemfuata kuzungumza naye na anaweza kufundisha hata ligi daraja la
kwanza.
Comments
Post a Comment