Skip to main content

Posts

Showing posts from December 6, 2015

TAZAMA BONGE LA VIDEO KUTOKA KWA Diamond Platnumz - Utanipenda

Taarifa kwa Umma Kuhusu Mlipuko wa Homa ya Nguruwe Jijini Mwanza

Baada ya kuripotiwa ugonjwa wa Kipindupindu kutokea katika maeneo mbalimbali kanda ya Ziwa headlines zimerudi tena.   Uchunguzi uliofanywa na Maabara ya chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine SUA umethibitisha kuwepo kwa ugonjwa wa homa ya nguruwe katika Wilaya ya Nyamagana, Mwanza.   Katika taarifa iliyotolewa na Katibu tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mwanza, Yohana Sagenge amethibitisha kuwepo kwa ugonjwa huo ambao unasababishwa na Virusu aina ya African Swine fever Virus ambapo madhara yake ni makubwa na husababisha kifo kwa 100%. kwa wanyama hao.   Taarifa hiyo ilisomeka hivi Nguruwe Homa   JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA  MITAA OFISI YA MKUU WA MKOA WA MWANZA TAARIFA KWA UMMA.  YAH: MLIPUKO WA UGONJWA WA HOMA YA NGURUWE Kumetokea mlipuko wa ugonjwa wa Homa ya Nguruwe (African Swine Fever) Wilaya ya Nyamagana, Kata za Mabatini, Mirongo kishiri na Buhongwa na Igoma. Mlipuko huu umedhibitishwa kwa uchung

TFF Yampongeza Nape Nnauye Kwa Kuteuliwa Kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtumia salamu za pongezi mbunge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye kufutia kuteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo katika serikali ya awamu ya tano. Katika salamu zake, Malinzi amempongeza Nape na kusema TFF ina imani nae katika nafasi hiyo, na kuahidi kushirikiana katika michezo na haswa katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya mpira wa miguu nchini. Aidha pia Malinzi amewapongeza Paschal Kihanga, Mwenyekiti wa chama cha soka moa Morogoro kwa kuchaguliwa kuwa Meya wa manispaa hiyo, na James Bwire mmiliki wa shule ya Alliance kwa kuchaguliwa meya wa manispaa ya Nyamgana. Malinzi amewatakia kila la kheri katika nafasi hizo walizozipata za kuwatumikia watanzania, na kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu nchini anawatakia kila la kheri na kuahidi kushirikiana nao.

Billioni 473 Zatolewa Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya juu.....Tahliso Yammwagia Sifa Rais Magufuli

Shilingi billion 473 zimetengwa kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu nchini kwa mwaka huu ikilinganishwa na Shilingi bilioni 341 zilizotolewa  mwaka jana ikiwa ni ongezeko la Tsh. bilioni 132 katika bajeti ya mwaka huu. Hayo yalisemwa  jana jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa shirikisho la wanafunzi wa vyuo vikuu Tanzania (Tahliso)  bwn. Nzilanyingi  John  alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuaandaa mdahalo kujadili hotuba ya Rais Dkt. John Magufuli aliyoisoma Dodoma wakati wa ufunguzi wa bunge la kumi na moja . Alisema kuwa kwa kipindi kifupi kumekuwa na  mabadiliko ya haraka yaliyotokea katika sekta ya elimu nchini kwa mwaka huu  kwani kuna ongezeko la zaidi ya wanafunzi 1800 waliopata mkopo ikilinganishwa na mwaka uliopita ambapo ni wanafuzi 34128 pekee ndio waliofanikiwa kupata mkopo. “Mpaka sasa jumla ya wanafunzi 51,675 wa mwaka wa kwanza wamepata mkopo na lengo ni kufikia 53,032, pia jumla ya wanafunzi 91 wa shahada ya uzami

Wizara Ya Mambo Ya Ndani Ya Nchi Yafuta Vyama Vya Kijamii 1,268

WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi imefuta vyama vya Kijamii 1,268 kutokana na kushindwa kutekeleza majukumu yao na sheria zilizowekwa katika uendeshaji wa vyama pamoja na mashirika yasiyo ya Kiserikali (NG’0s). Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Isaac Nantanga alisema kuwa kufutwa kwa vyama hivyo ni kutokana na kukiuka masharti ya uendeshaji wa taasisi ikiwemo kutolipa ada kwa mujibu wa sheria. Katika ufutwaji wa vyama hivyo chama kimojawapo kilichofutwa ni chama cha wapiga picha nchini ambacho kimeshindwa kukidhi vigezo vya uendeshaji na kushindwa hata kuendesha vikao vyake. Nantanga alisema kuwa vyama vingine 1,406 vimepewa kusudio la kufutwa na baada siku 21 kuanzia jana, kama havitatoa kusudio la kujitetea basi navyo vitafutwa. Alisema kufuatana na kanuni ya vyama inayoundwa na kifungu cha 38 cha sheria ya vyama vyote vya kijamii vinapaswa kulipa ada ya kila mwaka. Aidha, alisema kanuni ya 6 za v

Serikali Yaelekeza Uendeshaji wa Sekondari Zake za Bweni

SERIKALI inatarajiwa kutoa utaratibu wa namna wanafunzi wa shule za Serikali za mabweni, watakavyosoma huku ikionya wakuu wa shule watakaodai ada au michango ya aina yoyote, kwamba watachukuliwa hatua ikiwemo kufukuzwa kazi. Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Jumanne Sagini amesema hayo jana wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Kitaifa wa mwaka wa wadau wa Camfed unaofanyika mjini hapa. Katika hotuba yake iliyosomwa na Mkurugenzi Idara ya Usimamizi wa Elimu, Benard Makali, Sagini alisema kuanzia Januari 2016, elimu nchini katika shule za msingi na sekondari itatolewa bure. Alisema shule zenye hosteli kisheria, usajili wake ni shule za kutwa na zitapewa utaratibu wake katika uendeshaji na Serikali itakaa na kutoa maelekezo sahihi ili wazazi wasaidie kuchangia chakula. Amesema Serikali itakaa na kutoa maelekezo sahihi, ili wazazi wasaidie mipango mizuri ya halmashauri.     “Chakula si pesa kama wazazi watakubaliana kucha

Wafanyabiashara Wapuuza Agizo la Siku 7 Lililotolewa na Rais Magufuli........ Kamanda Kova Atangaza Zawadi Nono Atakayemdaka Mfanyabiashara Huyu

Makampuni 26 yamekaidi agizo la Rais John Magufuli lililowataka wafanyabiashara wote waliokwepa kodi kwenye Makontena 326 yaliobainika kupotea bandarini walipe kodi ndani siku saba. Hata hivyo ni Makampuni 6  tu ndio yaliyotii agizo la Magufuli baada ya kulipa kodi iliyokadiliwakuwa  pamoja na faini. Vilevile Makampuni 16 yamelipa kodi  nusu tu tofauti na ile iliyokadiliwa,ambapo  jana ndo ilikuwa siku ya mwisho toka siku aliyosema  Rais Magufuli kuwa ndani ya siku saba wawe wamelipa kodi hizo. Kodi iliyolipwa na makampuni haya 22 ni  10,075,979,462.08 Akizungumza na waandishi wa habari jana Mchana kwenye Makao ya jeshi la polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Meneja wa Huduma na elimu kwa mlipa kodi kutoka wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Diana Masalla alisema  mpaka jana saa kumi jioni ni makampuni sita tu ndio yaliyolipa kodi hiyo huku mengine 16 yakilipa nusu ya madai ya kodi na Makampuni 26 yakishindwa kulipa kodi iliyotakiwa pamoja nafaini ya kukwepa kodi.  

HIZI HAPAA ...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi

Ajira za makatibu wakuu ziko salama- Ikulu

Uamuzi wa Rais John Magufuli kuunganisha wizara kutoka 30 hadi kuwa 18 na idadi ndogo ya mawaziri, hautasababisha kupunguzwa kwa watumishi, hasa makatibu wakuu, Ikulu imeeleza. Juzi, Rais Magufuli alitangaza kuunganisha wizara na kuunda Baraza la Mawaziri lenye wizara 18 kutoka 30 za Serikali ya Awamu ya Nne, uamuzi ambao umeibua hofu kwa baadhi ya watumishi kuwa panga hilo linaweza kuwakumba makatibu wa wizara zilizopunguzwa. Jana, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alieleza kuwa Serikali itafanya mgawanyo mpya wa majukumu kwa watumishi wote na suala la kuwapunguza kazi halifikiriwi kwa sasa. Balozi Sefue alisema fedha zilizotengwa kwenye bajeti ya mwaka 2015/16, zitapelekwa kwenye kila wizara husika, hata kama itakuwa imeungwanishwa na nyingine na kuunda wizara moja. Katika mabadiliko na uundaji wa baraza hilo, Dk Magufuli ameunganisha baadhi ya wizara, huku akizihamisha baadhi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu na kuzipeleka Ofisi ya Rais na nyingine kuziondoa kwe

Wakuu wa Mikoa na Wilaya Kupukutishwa

Baada ya kutaja Baraza la Mawaziri lenye sura mpya nyingi juzi ikiwa moja ya hatua katika ukamilishaji wa safu za uongozi wa serikali ya awamu ya tano, Rais John Magufuli anataraji kuondoa Wakuu wengi wa Mikoa na Wilaya kutokana na kukosa sifa, taarifa za uhakika zinasema. Mbali na wawakilishi wa Rais hao katika ngazi ya Mkoa na Wilaya, panga kubwa litawakumba wakurugenzi wa Taasisi na Mashirika ya Umma nchini. Taarifa kutoka ndani ya serikali zinaeleza kuwa Rais Magufuli ameshaitisha mafaili ya kumbukumbu za wasifu wa viongozi hao ili kujiridhisha na sifa zao. Chanzo cha habari kutoka serikalini kimedokeza kuwa taasisi na mashirika ambayo yapo katika hatari ya kukumbwa na fagio la Rais Magufuli ni pamoja na Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru). Taarifa zilieleza kuwa Rais Magufuli atachukua hatua hiyo kwa lengo la kuteua watendaji wapya ambao wataendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano inayotekeleza kauli mbiu

kama ukupata kufahamu baraza jipya la mawazirii.......HILI HAPA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI WA WIZARA ZOTE 18 NA MAJINA YAO !!!!!!.

  Habari wakuu Magufuli:  Tutakuwa na mawaziri 19, kuna baadhi ya wizara zitakuwa na mawaziri na hazitakuwa na manaibu waziri. Lengo ni kuwa na baraza dogo kupunguza gharama. Zilitengwa bilioni 2, mawaziri watakapoteuliwa waende semina elezi, baraza nitakaloliteua halitakuwa na semina elekezi na fedha tutaelekeza sehemu nyingine kama ni madawati au kwenye elimu bure. WIZARA Ofisi ya Rais, Tamesemi utumishi na utawala bora, Simbachawene na Kairuki, Naibu waziri Jaffo Mazingira: Makamba, naibu Makamba Ajira, walemavu: Jenista Mhagama, Naibu nimemtua mbunge, Pos Abdallah ambae ni mhadhiri Dodoma Ulemavu: Mavunde Kilimo, mifugo na uvuvi: Mwigulu Lameck Nchemba, Nashe naibu Ujenzi, uchukuzi na mawasiliano: Waziri bado sijamtafuta, naendelea kumfikiria, Naibu waziri Ngonyani. Fedha na mipango: Waziri bado, naibu Kijachi Nishati na madini: Waziri ni Muhongo, Naibu Katiba na sheria: Waziri Mwakyembe Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki: Augustino Mahiga nmemteua mbunge na waziri,