Wafanyabiashara Wapuuza Agizo la Siku 7 Lililotolewa na Rais Magufuli........ Kamanda Kova Atangaza Zawadi Nono Atakayemdaka Mfanyabiashara Huyu
Makampuni 26 yamekaidi agizo la Rais John Magufuli lililowataka wafanyabiashara wote waliokwepa kodi kwenye Makontena 326 yaliobainika kupotea bandarini walipe kodi ndani siku saba.
Hata hivyo ni Makampuni 6 tu ndio yaliyotii agizo la Magufuli baada ya kulipa kodi iliyokadiliwakuwa pamoja na faini.
Vilevile Makampuni 16 yamelipa kodi nusu tu tofauti na ile iliyokadiliwa,ambapo jana ndo ilikuwa siku ya mwisho toka siku aliyosema Rais Magufuli kuwa ndani ya siku saba wawe wamelipa kodi hizo. Kodi iliyolipwa na makampuni haya 22 ni
10,075,979,462.08
10,075,979,462.08
Akizungumza na waandishi wa habari jana Mchana kwenye Makao ya jeshi la polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Meneja wa Huduma na elimu kwa mlipa kodi kutoka wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Diana Masalla alisema mpaka jana saa kumi jioni ni makampuni sita tu ndio yaliyolipa kodi hiyo huku mengine 16 yakilipa nusu ya madai ya kodi na Makampuni 26 yakishindwa kulipa kodi iliyotakiwa pamoja nafaini ya kukwepa kodi.
“Agizo la Rais Magufuli mwisho wake ni leo( jana) saa kumi jioni,lakini wafanyabiashara hao waliotorosha makontena yao wamekaidi agizo hilo. Sisi TRA hatuna kingine cha kufanya, tunaiacha sheria ichukue mkondo wake,” alisema Bi Massala.
Bi Masalla aliwasisitiza wananchi wote watoe taarifa kuhusu vitendo vya ukwepaji kodi kutumia namba 0784210209. Pia taarifa za mwenendo wa wafanyakazi wa TRA Wasio waadilifu zitolewe kupitia simu namba 0689 122515 na ujumbe mfupi 0689 122516..
Naye Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamisha Kova aliwaambia wanahabari kuwa Jeshi la Polisi linamtafuta Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya REGIONAL CARGO SERVICES LTD,ABDULKADIR S/O KASSIM ABDI, Miaka 38, Mkazi wa Temeke Mikoroshini ambaye anatuhumiwa kwa kutoa makontena 329 kwenye bandari kavu ya AZAM (AZAM ICD) bila kulipia kodi .
Kamishna Kova alidai kuwa anayetafutwa na jeshi hilo pia ni mmoja wa wakurugenzi wa kampuni za “JAS EXPRESS FREIGHT LTD” na “XL CLEARING AND FOWARDING Co. LTD” ambazo zote zilitumika kutoa makontena hayo.
Alisema Mwananchi atakayefanikisha kukamatwa kwa mtu huyo (pichani) atapewa zawadi nono ya milioni 20.
Alisema Jeshi la polisi pia linawashikilia watuhumiwa 40 ambao wanahojiwa kwa tuhuma za kula njama na kuikosesha serikali mapato.
Kamanda Kova alisema uchunguzi unafanywa kwa pamoja na maafisa wa Jeshi la Polisi na Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kwa lengo la kubaini jinsi ambavyo makontena 329 na mengine 2489 yalivyotolewa bandarini kinyume cha taratibu.
Kamanda Kova alisema uchunguzi unafanywa kwa pamoja na maafisa wa Jeshi la Polisi na Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kwa lengo la kubaini jinsi ambavyo makontena 329 na mengine 2489 yalivyotolewa bandarini kinyume cha taratibu.
Alisema kati ya watuhumiwa hao, watuhumiwa 26 ni watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na watumishi 03 wanatoka Bandari kavu (ICD) YA AZAM ambao wote kwa pamoja wanatuhumiwa kuhusika na upotevu wa makontena 329. Watuhumiwa 11 ambao ni watumishi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) wanatuhmiwa kwa kuhusika na upotevu wa makontena 2489.
Kamisha Kova alisema uchunguzi unaoendelea pia unahusisha kupitia kumbukumbu mbalimbali na kadhia za forodha ili kubaini mtindo uliotumika na kuwabaini wote waliohusika katika mchakato huo.
Makontena 329 yaligundulika kukosekana kwenye ICD ya AZAM kuanzia mwezi Julai hadi Novemba 2015, wakati makontena 2489 yaligundulika kutolewa Bandarini kuanzia Mwezi Machi mpaka Septemba, Mwaka 2014 kinyume cha taratibu kwa lengo la kukwepa kodi na ushuru
Makontena 329 yaligundulika kukosekana kwenye ICD ya AZAM kuanzia mwezi Julai hadi Novemba 2015, wakati makontena 2489 yaligundulika kutolewa Bandarini kuanzia Mwezi Machi mpaka Septemba, Mwaka 2014 kinyume cha taratibu kwa lengo la kukwepa kodi na ushuru
Comments
Post a Comment