Skip to main content

Posts

Showing posts from June 28, 2015

Wanaomwita Lowassa fisadi? mwisho wa kurudisha fomu CCM?

Kwenye headlines kubwa Magazetini kuna hizi stori ambazo nimekusogezea baada ya kuchambuliwa redioni June 02 2015. Makada wa CCM wameendelea kurudisha fomu za Urais na leo ndio siku ya mwisho, Lowassa   amesema amechoshwa na wanaomwita Fisadi.. kingine ni kuhusu ishu ya ushirikina Wilaya ya Mwibala, mtu mmoja ameuawa akituhumiwa kuwafanyia ushirikina  Walimu. Stori nyingine inahusu  utafiti uliofanywa TZ kuhusu Wagombea Urais  umepokelewa kwa hisia tofauti,  Bajeti 2015/16 yadaiwa kuwanyonya damu Watz … Tume ya Taifa ya Uchaguzi TZ imesema Uchaguzi Mkuu uko palepale. Serikali imetangaza kwa wanaotoa taarifa za uongo Kikosi cha Zimamoto kukiona! NECTA wamekuja na mfumo wa matokeo ya Mitihani kwa njia ya simu. Washitakiwa wa mauaji ya albino wamehukumiwa hukumu ya kifo Mbeya.. stori zote ninazo kwenye sauti niliyorekodi # PowerBreakfast   hapa.

JE? Unamfahamu Rais bora Afrika 2015? Ninayo hii stori iliyopewa headlines kubwa leo..

Rais wa Kenya  Uhuru Kenyatta   amechaguliwa na muungano wa wanafunzi wa Vyuo vikuu barani Afrika  AASU  kama rais bora barani Afrika mwaka 2014/2015. Kabla ya Kenyatta kushinda, Rais  Paul Kagame   wa Rwanda alikuwa akishikilia nafasi hiyo. Rais Kenyatta  akikakabidhiwa hati ya Ushindi na Wawakilishi wa Wanafunzi hao. Kenyatta  alichaguliwa na maelfu ya wanafunzi kutoka Vyuo mbalimbali Afrika ambao walishiriki kwenye zoezi la kupiga kura. Kenyatta  alichaguliwa kwa uwezo wake wa kujenga makubaliano kitaifa na kimataifa na juhudi zake za kubadilisha sera na kutoa ufumbuzi katika masuala yanayohusu nchi ya Kenya.

Eti wachezaji wa Taifa Stars walikuwa hawakuelewa Kingereza?, Cannavaro kanyoosha mkono

. Kumekuwa na headlines tofauti tofauti katika mitandao zikiwahukumu wachezaji wa timu ya ‘Taifa Stars’  kutojua lugha ya kingereza ndio chanzo iliyopelekea kutofanya vizuri uwanja na kutoelewana na aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’  Mart Nooi. . Sasa leo July 2, 2015  Nadir Haroub a.k.a  Cannavaro  amefunguka na kuelezea hujuma hizo… ‘ Sisi wachezaji tunaumia zaidi kuliko mashabiki kwasababu maisha yetu tunategemea mpira tunapopata matokeo mabaya familia zetu zinakaa na njaa, kwanza tunakosa fedha tunazoahidiwa, tunakosa pia kuthaminiwa na watu nje unajua unapofanya vibaya watu hawawezi kukusapoti sisi tunaumia zaidi. . Kwa suala la mwalimu kusema kuwa watu hawajui kingereza sio kweli, kwani suala la mpira ni vitendo mwalimu anakuambia fanya hivi hivi na mchezaji unaelewa nini cha kufanya, matokeo yanatokea kwenye mpira unaweza ukashindwa au ukafungwa, sisi tunaumia sana na tunataka matokea mazuri ili tupate kuheshimika kwenye vilabu vyet

DUUUU! TAZAMA KALI YA MWAKA Mwanafunzi kaona aingie na jeneza kwenye Graduation yake…

Niliwahi kukuletea stori ya bibi harusi kuamua kufanya surprise kwa mume wake pamoja na wageni waalikwa siku ya harusi, akajipanga na kuingia zake Ukumbini akiwa ndani ya jeneza.. lengo lake ilikuwa afanye tu kitu tofauti na kuvunja rekodi yake mwenyewe. Leo nakuletea hii nyingine ambayo imetokea Uingereza, mwanafunzi mmoja kaingia kwenye sherehe za mahafali ya kumaliza Shule akiwa ndani ya jeneza, wakati yeye  anakuja kihivyo wenzake walitumia magari na usafiri mwingine kawaida kabisa kwenda kwenye Sherehe hiyo. Simom May  alikuwa Mwanafunzi wa Chuo cha   Alder Grange Community and Technology School,   Ross endale  Uingereza … aliingia maeneo ambapo ilikuwa ikifanyika Graduation hiyo akiwa ndani ya jeneza. Simon  hakuwa pekeake, alisindikizwa na wapambe wake pamoja na mdogo wake ambaye inasemekana ndiye alimshauri kuja na mtindo huo tofauti. Kitendo hicho kilionekana kuwafurahisha na kuwashangaza wanafunzi wenzake pamoja na walimu waliohudhuria sherehe hiyo.

Madam Rita na BSS 2015, Joh makini na matapeli wa mitandao, Madee kaamua kuacha muziki?

Jana  Madam Rita   alipiga stori na kipindi cha  XXL  na kusema mashindani ya  BSS  yatakua yakifanyika kikanda na kila Mkoa watachukua watu watano kama awali lakini pia inategemea kama hakuna anayewafaa kwenye Mkoa husika wanaondoka na kwenda Mkoa mwingine. Pia amezungumzia kituko ambacho hatakisahau katika maisha yake kwenye mashindano ya BSS ni kijana mmoja ambaye alienda jukwaani akiwa ameweka vinyonga tumboni kisha akawatoa na kuwaweka mdomoni…amesema hawezi kusahau. Madam Rita Kingine ni kutoka kwa  Joh Makini  ambaye baada ya mashabiki wake kudai kutapeliwa hela walizotaka kununua Tshirt za weusi, mwenyewe amesema amesikitishwa na kitendo hicho lakini anashukuru ni mmoja ambaye aliweza kutuma pesa za oda ya Tshirt na kuahidi kumrudishia huku akiwataka watu kuwa makini na akaunti feki ambazo hutumiwa na matepeli kuwaibia. Joh Makini Madee  naye amesikika akisema anafikiria kupumzika kwenye game muda si mrefu, amekaa kwenye muziki zaidi ya miaka 15 na anaamini hak

HIZI NDIZO SABABU ZA MSANII MB Dog, KUKAA KIMYAA MUDA WOTEE

.  . Mkali wa ‘Latifa’, Si uliniambia’ Mbwana Mohamed aka MB Dog time hii amefunguka na kuelezea sababu zilizopelekea kuwa kimya kwa muda mrefu kwenye tasnia ya muziki wa Bongo Fleva  alisema…’ Kwanza nilikuwa nimetoa kwenye kampuni ambayo ilikuwa ikinisaidia halafu then nikawa mwenyewe so baada ya kuona mambo yamekuwa mazito nikatoa kidogo nikaenda kukaa sana Ujerumani kama miaka miwili nikaja nikarudi Uingereza hapo katikati zile safari baada ya kuona mambo yamekuwa mazito ndio sababu ya kukuwa kimya. . Sijawahi kupiga ngoma ikawa imeenda tofauti kila niliyowahi kuupiga ulikuwa unaenda na damu zao halafu ilikuwa zinafanana na wao kwa hiyo ngoma zangu zote zilikuwa na manufaa na zilikuwa na faida kwasbabu ndio zimenifanya mpaka leo nipo nakutana na watu tofauti wananiamia na heshima kubwa kupitia hizo ngoma . Mimi niko chini ya Qs Mhonda J Entertainment kampuni kubwa sana ambayo kwasasa ndio inasimamia kazi zangu kiufupi niwahabarishe mashabiki wangu kuna kazi amba

anuary Makamba kajibu haya kuhusu wizi wa muda wa hewani unaofanywa kwenye simu za watu

Kama uliwahi kuweka vocha kwenye simu yako alafu ukakuta ile hela uliyoweka haipo na wala hujaitumia, hii ishu imewagusa Wabunge… Alianza Mbunge kwa kuuliza swali kwamba nini kinafanyika kuzuia wizi wa aina hiyo. “ Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi kwamba wanapoteza pesa kujiunga na vifurushi ama wanaponunua vocha… Serikali itachukua hatua gani kudhibiti Makampuni ya simu ambayo yanafanya wizi kwa wananchi ” >>> Mbunge  Murtaza Mangungu . “ Kumekuwa na udhaifu mkubwa kwa upande wa TCRA kwenye kufuatilia malalamiko ya watu pale ambapo wanadhurumiwa, watu wanatoa malalamiko kwa Makampuni ya simu lakini hakuna  hatua zinazochukuliwa ” >>  January Makamba . Naibu Waziri Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, January Makamba . “ Serikali imetoa onyo kwa TCRA kwamba tunataka hatua zianze kuchukuliwa na namna mpya ikiwemo kuhakikisha kwamba kuna kituo ambacho kipo saa zote kwa ajili ya kupokea simu na malalamiko ya watu na ni rahisi kituo hicho kufikik

KAMA HAUKUFANIKIWA KUTAZAMA JINSI Mwimbaji Ben Pol alivyonusurika kifo baada ya boti kuzama baharini. tazama hapa

Ben Pol ni mwimbaji staa wa RNB kutoka kwenye Bongofleva Tanzania, alinusurika yeye na rafiki zake kwenye ajali ya Boti iliyozama wakiwa wanatokea kwenye kisiwa cha Mbudya, nje ya Dar es salaam kurudi Dar es salaam.

Tazama jinsi video ya Ali Kiba 'Chekecha Cheketua ' itakavyokuwa

Maneno mengine ya Ommy Dimpoz kuhusu waliomtukana Instagram…

Ommy Dimpoz  alipost tangazo la Video mpya ya  Ali Kiba   lakini baada ya kupost wapo waliopita kwenye post yake @Instagram na kuanza kuandika comments za matusi. Mwenyewe amesema hakupenda kuona watu wanaandika comments za matusi kila kitu ambacho anapost…  Ommy   amesema kwenye kurasa za mastaa kama yeye wanaotembelea ni watu wengi kwa hiyo sio kitu kizuri watu kuandika lugha za matusi. Mitandao huwa inakuwa na story nyingi sana kuhusu mastaa, wakati mwingine utasikia staa huyu na huyu hawapatani,   Ommy  amesema wakati mwingine watu huwa wanakuza hata beef kati ya mastaa lakini beef nyingine sio za kweli.

Haya ndio maneno ya H. Baba kuhusu video mpya ya Ali kiba ‘Chekecha’

. Muimbaji Hamis Baba aka  H Baba  leo ameamua kuandika kwenye ukurasa wake Instagram kuhusu video mpya ya Ali Kiba iitwayo Chekecha iliyochezwa kama ‘Exclusive’  June 29 kwenye kituo cha luninga maarufu  Trace Tv  ya Ufaransa. Ujumbe huo unasomeka hivi; ‘ #KIUKWELI WEE JAMAA@officialalikiba UMENIFURAHISHA SANA KWENYE HII #VIDEO KAMA NILIOTA VILE #UMEITENDEA HAKI WIMBO HUU WA #CHEKETUA PIA UMECHEZA VIZURI SANA NAUFUNDI WASAUTI SASA NIMENJOY SANA KUITAZAMA NARUDIA RUDIA TUU#SALUTE KIBA #NAONGEA KAMA#MWANAMUZIKI MWENZAKO #salute#KINGKIBA HUU WIMBO UMEUTENDEA HAKI SANA @VIDEO HATARIIII#NILICHOPENDA KWENYE HII VIDEO#LOCATION ZAKE TAMU SANA#UTAZANI SIO MAREKANI KAMA KINO AU MIGO #UVAAJI ULIOVAA UNAENDANA NA #CHEKETUA LILE BEAT LAKO NANGUO NIMEPENDA#UNAJUA NINI UNAFANYA #HONGERAZAKO #WAHUSIKA WALIOMO NDANI YA VIDEO #KIAFRIKA ZAIDI#HONGERAA SAAAANA #SINA TEAM YOYOTE HUMU NDANI ILA #KIBA ANAJUA TUACHE MASIHAraaaa MWANAMUZIKI kumkubhali mwenzio inaruhusiwa SIO KIFUNGO CHA MIAKA#30 JE

HII NDIYO List ya Washidi Wote Tuzo za BET2015

Usiku wa Jumapili ulikuwa ni usiku wa utoaji wa Tuzo za BET, ambapo East Africa Tulikuwa tunawakilishwa na Sauti Sol...Japo Hawajabahatika kupata Tuzo. Tuzo zilikuwa zina Buradani ya aina yake! Performance zilikuwa nzuri sana! kati ya waliotumbuiza ni pamoja na Waimbaji wa Series Maarufu ya EMPIRE, Chris Brown, Kendrick Lamar na wengine wengi. Hii ni list nzima ya wasindi walioshinda katika Tuzo za BET. Aliekuwa kinara wa tuzo hizi alikuwa Beyonce aliechukua tuzo tatu. Best International Act UK: FKA Twigs Fuse ODG Lethal Bizzle Little Simz Mnek Stormzy- Winner Best International Act Africa: AKA Stonebwoy- Winner Sarkodie Fally Ipupa Sauti Sol Wizkid The Soil Yemi Alade Best Female R&B/Pop Artist: Beyoncé- Winner Janelle Monáe Jhene Aiko Ciara Rihanna K. Michelle Best Male R&B/Pop Artist:   Chris Brown- Winner Trey Songz The Weekend August Alsina Usher John Legend Best Group: A$AP Mob Migos Ra