Skip to main content

Posts

Showing posts from January 5, 2014

TUNAOMBA RADHI KWA HIZI PICHA: HAWA NDIO MAJAMBAZI WATATU WALIOUAWA NA KUCHOMWA HUKO MOROGORO

  WANANCHI wenye hasira wa Kijiji cha Kisiwa Kata ya Kiloka Wilaya ya Morogoro Vijini jana usiku wamewauwa kisha kuwachoma moto watu watu  wanaosadikiwa kuwa majambazi.   Akizungumza na Mtandao huu shuhuda wa tukio hilo Bw Shabani Mango alisema majambazi hao walivunja nyumba ya mkazi mmoja wa kijijini hicho na kuiba shilingi  490,000.   "Jamaa walifka hapa majira ya saa 8 usiku wakiwa na pikipiki Feko yenye namba za usajiri T310 BTC wakipakizana mshikaki,walivunga geni na kuingia ndani ambapo walipora kiasi hicho cha fedha "alisema Mango na kuongeza" Fedha hizo Mwalimu Said Swale Tajiri alizikopa jana mchana kwenye saccos ya Moboto kwa lengo la kumlipia ada mdogo wake anayesoma jijini Dar es salaam leo ijumaa alipanga kwenda Dar kulipa ada nahisi jamaa walipata taarifa kwamba Ticha ana mzigo ndani"alisema Bw Mango.   Akihojiwa na mtndao huu afisa mmoja wa jeshi la polisi alithibitissha kutokea kwa tukio hilo na kuwataja majambazi

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo amaliza ziara yake katika Mkoa wa Pwani.

Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Bi.Mwanamvua Mrindoko akimweleza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel(mwenyeshati Jeusi) Mpango wa kuendelea kuwawezesha vijana katika halmashauri yake kwa Kutekeleza mipango mbalimbali iliyowekwa ikiwamo kutoa mafunzo kwa vijana na kuongeza bajeti hadi kufikia shilingi milioni 40 kutoka milioni 10 iliyokuwa inatolewa hapo awali kwa mwaka wa fedha 2014-2015,wakati wa Ziara ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo kuangalia shuguhuli mbalimbali za vijana zinazoratibiwa na Wilaya hiyo. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel(mwenyeshati Jeusi) akiongea na vijana wa kikundi cha bodaboda wakati wakati wa Ziara ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo kuangalia shuguhli mbalimbali za vijana leo katika wilaya ya Kisarawe. Naibu Katibu Mkuu Wiz

Huyu hapa MTOTO WA AJABU

Na Hamida Hassan na Imelda Mtema AMA kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya Farao, Andrea Marcus (13), mkazi wa Mbezi-Kibanda cha Mkaa, Dar anadaiwa kuwa wa ajabu kutokana na vitendo vyake. Mtoto huyu amedaiwa kuwa ni wa kichawi kutokana na maajabu yafuatayo: Mkazi wa Mbezi-Kibanda, Andrea Marcus. Ana uwezo wa kula ubwabwa sufuria moja la familia, anamudu kunywa maji ndoo moja, ana uwezo wa kuingiza tumboni mikate mikubwa saba kwa mlo mmoja,  amewahi kula mchele (si ubwabwa) ndoo nzima. Mbaya zaidi baada ya kula milo hiyo huwa haoneshi ameshiba. Maajabu mengine ambayo yanawashangaza watu wanaoishi naye ni jinsi anavyokula chakula kwa kumwaga chini kisha kukomba mpaka udongo. “Sina amani ya moyo, naomba Watanzania wanisaidie, mwanangu ananiuma sana, hata kujisaidia ni hapohapo, chakula anakula kupita kiasi, kama nilivyosema hashibi na bado hali kama mwanadamu wa kawaida,” alisema mama wa mtoto huyo. Akizungumzia madai ya uchawi, mama huyo, Angelina Marcus alisema

Hawa hapa wapiganaji 30 wa Al Shabaab waliouawa

Wanamgambo wa Al Shabaab Msemaji wa jeshi hilo Meja Emmanuel Chirchir ameelezea kuwa jeshi la Kenya lilishambulia kwa mabomu mojawapo ya kambi za kundi hilo katika eneo la Gedo , Alhamisi Jioni. Aliongeza kwamba miongoni mwa waliofariki ni makamanda kadhaa wa kundi hilo. Al Shabaab hata hivyo hawajatoa tamko lolote kuhusu shambulizi hilo. Kadhalika Al Shabaab walikiri kufanya shambulizi la kigaidi mjini Nairobi mwaka jana dhidi ya jengo la kifahari la Westgate na kuwaua watu 70. Kenya imekuwa ikipambana na wapiganaji wa kundi hilo tangu mwaka 2011 Oktoba wanajeshi wake walipojiunga rasmi na vikosi vya muungano wa Afrika ambavyo tayari vilikuwa nchini Somalia kwa kazi hiyo. Rais Uhuru Kenyatta ameahidi kuwa majeshi ya Kenya yataendelea va vita dhidi ya wanamgambao hao tangu waliposhambulia Kenya mwaka jana.

HIZI NDIZO SABABU ZILIZOMFANYA JOYCE KIRIA AIKACHIFU ELIMU YA PHD!

  Nikienda shule ntachizika!!!! Acha nibaki na hizi zinazonisaidia kukataa Usaliti ambao ni Ukatili mkubwa sana wa kijinsia... na wanaume ndiyo wanaoongoza kusaliti Ndoa zao tena Wasomi wa taifa hili (japo siyo wanaume wote.) Kama elimu hii ya std7 inanisaidia kuupiga vita Usalitikwa nguvu na akili zangu zote..huku wasomi wenye nondo zao wakipinga vikali na kutaka kunitoa roho kwa sababu tu ya kuvunja kwangu ukimya, Ni bora std7 yangu walahi.... Phd ya kukumbatia Maovu SIITAJ I. Phd ya kutetea Uzinzi/Umalaya/Wizi! SIITAKI Phd ya kutomsifia Mume wangu baba watoto wangu bila Eti kwa sababu anaweza kuja kugeuka! SIITAKI... 2014 siitaji umaarufu Mavi, wa kufa na tai shingoni. Najua ni ngumu sana msimamo wangu kuwaingia watu, lakini ntakomaa mpaka mwisho. Wanawake wengi sana tunaumia kwa sababu za Usaliti unaoitwa ni "Utamaduni wa Kiafrika Wanaume kusaliti Ndoa zao!!" Itatuitaji wanawake kubadili hii mitazamo kandamizi kwa kuchukua hatua ya kuach

MATOKEO YA SENSA YA IDADI YA TEMBO KATIKA MFUMO WA IKOLOJIA WA SELOUS-MIKUMI NA RUAHA-RUNGWA

Wizara ya Maliasili na Utalii inapenda kuujulisha umma matokeo ya sensa ya tembo iliyofanyika mwezi Oktoba na Novemba mwaka huu ili kuiwezesha Serikali kutambua hali ya rasilimali ya wanyamapori ndani na nje ya maeneo yaliyohifadhiwa. Wizara kwa kushirikiana na wataalamu wa ndani na nje ya nchi imefanya sensa katika Maeneo ya Mfumo ikolojia wa Selous – Mikumi na Ruaha – Rungwa pekee kwa kuwa ni maeneo yenye tembo wengi nchini.  Matokeo ya sensa hii yanaonyesha kwamba Mfumo wa ikolojia wa Selous-Mikumi kwa sasa una tembo wapatao 13,084 na Ruaha–Rungwa una tembo wapatao 20,090. Takwimu hizi zinaonesha kupungua kwa idadi ya tembo na hasa katika mfumo ikolojia wa Selous-Mikumi ikilinganishwa na Sensa za awali. Takwimu za muda mrefu zinaonesha kwamba mwaka 1976 katika mfumo ikolojia wa Selous–Mikumi kulikuwa na tembo 109,419. Idadi hii ilipungua kufikia 22,208 mwaka 1991 kutokana na wimbi la ujangili uliokuwepo katika kipindi cha mwaka 1984 -1989. Hata hivyo, idadi hiyo

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA SHULE YA SEKONDARI YA KIEMBE SAMAKI ZANZIBAR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza jambo na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kiembe Samaki, Amina Salum Khalfan, wakati alipokuwa akitembelea chumba cha Maabara baada ya kuzindua rasmi Shule hiyo wakati wa hafla fupi iliyofanyika shuleni hapo mjini Zanzibar leo Jan 10, 2014. Picha na OMR Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na mmoja wa wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Kiembe Samaki, baada ya uzinduzi rasmi wa shule hiyo uliofanyika leo Jan 10, 2014, mjini Zanzibar. Picha na OMR Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kiembe Samaki, Amina Salum Khalfan, wakati alipotembelea katika chumba cha Mawasiliano na mafunzo ya Kompyuta cha shule hiyo, baada ya uzinduzi rasmi wa shule hiyo uliofanyika leo Jan 10, 2014, mjini Zanzibar. Picha na OMR Makam

KAULI YA AWALI KUHUSU ONGEZEKO LA BEI ZA UMEME

Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), katika kikao chake cha tarehe 10 Desemba 2013 pamoja na mambo mengine, ilitoa maamuzi ya ongezeko la bei za umeme kwa viwango mbalimbali kwa makundi mbalimbali ya wateja hatua ambayo itaongeza mzigo wa gharama za maisha kwa wananchi na itaathiri uchumi wa nchi. Maamuzi hayo yamefikiwa kufuatia tarehe 11 Oktoba 2013, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuwasilisha maombi ya kurekebisha bei ya umeme kwa EWURA. TANESCO ilipendekeza kuongeza bei kwa asilimia 67.87 kuanzia tarehe 1 Oktoba 2013, asilimia 12.74 kuanzia tarehe 1 Januari 2014 na asilimia 9.17 kuanzia tarehe 1 Januari 2015. Vilevile TANESCO waliomba kuidhinishwa kwa kanuni ya kurekebisha bei ya umeme kulingana na mabadiliko ya bei za mafuta, mfumuko wa bei na mabadiliko ya thamani ya shilingi ya kitanzania. Maamuzi hayo ya Bodi ya EWURA ambacho ni chombo cha Serikali yamethibitisha kwamba Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter

BREAK NEWS MOTO MKUBWA WAUNGUZA JENGO LA RK BARABARA YA NYERERE DAR

Jengo la RK lililokaribu na eneo la Jet katika Barabara ya Nyerere karibu na sheli ya Victoria linaendelea kuwaka moto mkubwa chana huu ambao umefika katika eneo la ghala la kuhifadhia madawa. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wapo eneo la tukio ambako hali bado si shwari. Sehemu iliyoathirika zaidi  ni ghala la kutunzia dawa za binadamu la kampuni ya Philips.
Hatma ya Djotodia ilikuwa swala kuu katika ajenda ya mkutano wa viongozi wa kikanda kuhusu mzozo unaoendelea nchini humo. Mkutano huo ulifanyika nchini Chad huku maelfu wakiendelea kutoroka nchini humo kutokana na ghasia. Maelfu ya watu waliandamana leo katika barabara za mji mkuu Bangui kumtaka Rais Djotodia, ajiuzulu. Rais Djotodia amekosolewa vikali kwa kukosa kumaliza mapigano ya kidini kati ya wakristo na waliokuwa waasi waisilamu ambao walimsaidia kuingia mamlakani kwa njia ya mapinduzi mwaka jana. Baraza lote la mpito katika Jamuhuri ya Afrika ya kati limekwenda nchini Chad ambako viongozi wa Afrika wanakutana kujadili mzozo unaoendelea nchini humo. Mkutano huo wa viongozi wa kikanda, uliahirishwa, mapema asubuhi Ijumaa. Lakini wajumbe kwenye mkutano huo wanasema walitakiwa kuendelea na mkutano usiku kucha ili kubuni mkakati kuhus

Hizi ndizo sifa zilizomfanya Yaya Toure ndiye awe mwanasoka bora zaidi mwaka 2013 barani Afrika

  Toure alikabidhiwa tuzo la (caf) mwaka wa tatu mfululizo katika sherehe zilizofanyika mjini Lagos, Nigeria Alhamisi usiku. Aidha Toure pia alishinda tuzo la BBC la mwanasoka bora zaidi barani Afrika mwaka jana. Alikuwa anawania tuzo hilo dhidi ya mchezaji mwenzake wa Ivory Coast Didier Drogba, ambaye huchezea Galatasaray na John Mikel Obi mnigeria ambaye husakata soka nchini Uingereza. "nimefurahi sana kwa sababu hii ni ishara kuwa nacheza vyema sana ,'' alisema Toure baada ya kupokea tuzo yake. Lakini alisema kuwa majaji walikuwa na wakati mgumu kumchagua mchezaji bora kwa sababu washindani wenzake wote ni wazuri. ''Sikudhani kama nitashinda kwa sababu Drogba na Obi Mikel ni wasakataji wazuri wa kabumbu,'' aliongeza Toure.

Hii inakuhusu, soma mambo 12 toka kwa mwanadada mainda unayopaswa kufanya kijana wa kizazi kipya.

Mambo 12 toka kwa mwanadada mainda unayopaswa kufanya kijana wa kizazi kipya. 1. Jifunze kuweka akiba ya fedha. 2. Jitaidi utafute mchumba sahihi na mjitaidi mfunge Ndoa... 3. Acha kuishi nyumbani kwa wazazi anza kujitegemea na usiende kuishi na washikaji (mageto). 4 Lipa madeni yote ya zamani. 5 Jali sana Afya yako. 6. Kuwa na marafiki wenyechangamoto za maendeleo tena wanaotafuta maendeleo kwa njia halali za kumpendeza Mungu wetu. 7. Anza kununua asset kama ardhi,nyumba, gari,n.k. 8. Jifunze kuvaa kwa Heshma na sii tu suala la kupendeza. 9. Yazamani yote futa anza maisha mapya. 10. Achana na starehe zisizo na maana. 11. Zingatia sana Muda wako maisha ni malengo. 12. Hii ndio kubwa kuliko zote Tenga Muda wako wa kuongea na MUNGU usemezane nae useme shida zako ulipokosea Utubu usisahau kutoa Sadaka, kutoa fungu la kumi, kusaidia wasiyojiweza, na uwe ma moyo wa shukrani...........Mungu atupe nguvu mwaka huu 2014 ....

HICHI NDICHO KILCHOSABABISHA kifo cha Mgimwa

Iringa/Dar.  Wakati mwili wa Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa ukitarajiwa kuzikwa leo, Serikali imesema kilichosababisha  kifo chake ni ugonjwa wa figo. Dk Mgimwa alifariki Januari Mosi, mwaka huu katika Hospitali ya Kloof Medi Clinic, Pretoria nchini Afrika Kusini alikokuwa amelazwa. Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dk Servacius Likwelile uliutaja ugonjwa huo mbele ya waombolezaji waliofika kuuaga mwili wake kwenye Viwanja vya Karimjee. Likwelile alisema: “Marehemu Mgimwa alikwenda Hospitali ya Kloof Medi Clinic, Afrika Kusini Novemba 3, mwaka 2013 kwa ajili ya uchunguzi wa kawaida wa afya yake...baada ya uchunguzi, madaktari walimshauri alazwe kwa uangalizi zaidi na matibabu na kwamba aliendelea na matibabu ya figo hadi kifo chake.” Aaagwa Dar Rais Jakaya Kikwete jana aliongoza mamia ya waombolezaji waliofika kwenye viwanja vya Karimjee kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Dk Mgimwa, pamoja na viongozi wengine wakiwemo Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gh

ZITTO ATOBOA SIRI NZITO YA CHAMA CHA CHADEMA KWA HABARI ZAIDI SOMA HAPA

Jana alipokuwa akiongea na waandishi wa habari, Mheshimiwa Tundu Lissu alimtuhumu Zitto kuwa ana magari mawili ya Nimrod Mkono na pia kwamba Mkono amewaambia CHADEMA kuwa amempa Zitto hela nyingi sana. Pia Lissu aliendelea kusema "Zitto alishiriki moja kwa moja kumzuia mgombea wa CHADEMA katika Jimbo la Nimrod Mkono wakati Nimrod Mkono alikuwa ni namba sita katika orodha ya Mafisadi iliyotajwa pale Mwembeyanga." Baada ya hapo naye Zitto Kabwe aliibuka na kumjibu Tundu Lissu kupitia ukurasa wake wa facebook; ingawa baada ya muda alihakiki majibu yake lakini hiki ndicho alichoandika awali.

MAZISHI YA DK MGIMWA; JIMBO LAZIZIMA

Stori: Na Francis Godwin, Iringa KUFUATIA kifo cha Mbunge wa Jimbo la Kalenga, Dk. Wiliam Mgimwa aliyefariki katika Hospitali ya Kloof Med- Clinic, Pretoria, Afrika Kusini wiki iliyopita na anayetarajia kuzikwa leo Kalenga, jimbo zima limezizima kwa simanzi. Jeneza lenye mwili wa Dk. Mgimwa likiwa mbele ya waombolezaji jijini Dar. Wananchi wa jimbo hilo wameingiwa na simanzi kwa kuwa enzi za uhai wake  marehemu alikuwa karibu sana na wapiga kura wake na hata maisha yake aliyokuwa akiishi ni tofauti na baadhi ya viongozi ambao wanalalamikiwa kwa kuwatelekeza wananchi wao baada ya kupanda vyeo. “Natambua ni mapenzi ya Mungu ila kweli tulimpenda sana mbunge wetu alikuwa ni mtu wa kujishusha, asiyependa kujilimbikizia mali zaidi ya kuwatumikia  wananchi ....kweli kifo chake ni pigo kubwa,” alisema mmoja wa wapiga kura wake aliyejitambulisha kwa jina la Dismas Mbwela. Gazeti hili lilifika nyumbani kwa marehemu eneo la Magunga Jimboni Kalenga  ambapo liliiona nyumba yake ambayo ni

HIZI NDIZO SABABU ZILIZOSABABISHA MAHAKAMA KUMFILISI WEMA

Achilia mbali watu binafsi wanaochukua vyao baada ya mambo kuzidi kumwendea ndivyo sivyo, habari ya uhakika ni kwamba Mahakama ya Ilala, Dar imeridhia kukamatwa kwa lile gari lake la kifahari… Stori: Waandishi Wetu YAMETIMIA! Ni kweli hakuna marefu yasiyokuwa na ncha! Miss Tanzania 2006, Wema Isaac Sepetu aliyesifika kwa kumwaga fedha kila kukicha  ameanza  kufilisiwa, Ijumaa Wikienda lina habari ya kipekee kuhusu mrembo huyo. Wema Isaac Sepetu. MAHAKAMA YAANZA Achilia mbali watu binafsi wanaochukua vyao baada ya mambo kuzidi kumwendea ndivyo sivyo, habari ya uhakika ni kwamba Mahakama ya Ilala, Dar imeridhia kukamatwa kwa lile gari lake la kifahari aina ya Audi Q-7 lenye namba za usajili T 973 BUJ lililokuwa likiwakosesha akina dada usingizi na kukabidhiwa kwa mmiliki halali kwa kuwa Wema alikuwa nalo kimagumashi. Gari aina ya Audi Q-7 lenye namba za usajili T 973 BUJ alilokuwa akiendesha Wema. Kwa mujibu wa vyanzo vilivyoenda shule vya Ijumaa Wikienda, gari hilo lilikama