Skip to main content

Posts

Showing posts from June 8, 2014

MKUU WA WILAYA YA KIBONDO AONGOZA MAPOKEZI YA BONDIA IBRAHIMU CLASS .KING CLASS MAWE’ BAADA YA KURUDI NA UBINGWA WA WPBF AKITOKEA ZAMBIA

 Bondia Ibrahimu Class “King Class Mawe ” kushoto akiwa na promota wa kimataifa Jay Msangi ‘Jiwe Gumu’ baada ya kutua nchini wakitokea Zambia walipo nyakuwa ubingwa wa WPBF Africa kwa kumpiga Mwansa Kabinga  wa Zambia katika Arthur Davis  Mkuu wa wilaya ya Kibondo Venance Mwamoto ‘kushoto’ alivyongoza mashabiki na wapenzi wa mchezo wa masumbwi kumpokea Ibrahimu Class ‘King Class Mawe’  aliyeshika mkanda baada ya kurudi na mkanda wa WPBF kwa kumpiga mzambia Mwansa Kabinga katika uwanja wa Arthur Davis kwa k,o ya raundi ya tisa na  kufanikiwa kunyakuwa ubingwa uho wa pili  kushoto ni bondia Shomari Milundi, kulia ni Promota aliyefanikisha safari hiyo Yaj Msangi, wadau Bilali Ngonyani na Rogers Masamu Picha na www,superdboxingcoach.blogspot.com   Bondia Ibrahimu Class ‘King Class Mawe ‘ akiwasili nchini kutokea Zambia aliponyakua mkanda huo Bondia Ibrahimu Class ‘King Class Mawe ‘ akionesha mkanda wake wa ubingwa juu Bondia Ibrahimu Class ‘King Class

RUVU SHOOTING YAWAJIA JUU WACHEZAJI WANAOIPONDA, WASEMA DHAMIRA NI UBINGWA

Na Baraka Mpenja wa fullshangwe, Dar es salaam MAAFANDE  wa Ruvu Shooting wamedhamiria kufanya maajabu katika msimu wa 2014/2015 wa ligi kuu soka Tanzania bara unaotarajia kuanza kutimua vumbi mwezi agosti mwaka huu. Masau Bwire, afisa habari wa klabu hiyo ameuambia mtandao huu kuwa wanaendelea vizuri na mazoezi waliyoanza jana chini ya kocha mkenya, Tom Alex Olaba katika uwanja wao wa Mabatini, Mlandizi, mkoani Pwani. Masau amesema nia yao ni kujiimarisha mapema ili kuleta changamoto mpya na ili kufanikisha ndoto hiyo, ndio maana Shooting imekuwa timu ya kwanza kuingia kambini. “Lengo letu ni kuchukua ubingwa au nafasi ya pili. Tukishindwa sana, sana tunahitaji nafasi ya tatu. Hatuongei kwa kujifurahisha, tunajipanga vilivyo”. Amesema Masau.

EDEN HAZARD `ASILIMIA 100` KUBAKIA CHELSEA, AANZA MAZUNGUMZO YA MKATABA MPYA

 Kujifunga: Eden Hazar amesisiza kuwa na furaha kubakia Chelsea na kumaliza tetezi za uhamisho majira ya kiangazi. Eden Hazard amedai kuwa kwa `asilimia 100` atabakia Chelsea na amethibitisha kuanza mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya.  Kocha wa Paris Saint Germain, Laurent Blanc alisema hadharani kuwa klabu hiyo ya Ufaransa inatamani kumsajili mshambuliaji huyo. Lakini mtandao wa Sportmail alhamisi iliyopita ulitoa taarifa kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji yuko katika harakati za kusaini mkataba mpya wa miaka mitano katika klabu yake ya Chelsea na atakuwa analipwa paundi laki mbili kwa wiki.

NEYMAR AITETEMESHA BRAZIL NZIMA, LAKINI MAMBO YAWA SHWARI KABISA….

Hofu: Neymar  akionekana mwenye maamivu makali baada ya kupata majeruhi ya kifundo cha mguu wa kulia. BRAZIL nzima jana ilizizima baada ya nyota wake kupata majeruhi ya kifundo cha mguu katika mazoezi na hofu kubwa kundanda juu ya ushiriki wake katika fainali za kombe la dunia.  Nyota huyo wa Barcelona aliteguka kifundo cha mguu wakati Selecao wakifanya mazoezi nje ya Rio Janeiro na kumlazimu kupata matibabu ndani ya uwanja. Hata hivyo baada kukaa chini kwa dakika kadhaa, nyota huyo tegemeo kwa kombe la dunia aliweza kusimama mwenyewe na kutembea bila tatizo lolote.

TBL YAWAPATIA WAKULIMA ELIMU YA UZALISHAJI BORA WA ZAO LA SHAYIRI

 Joel Msechu mtaalamu wa zao la shayiri kutoka Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) akiwaonesha wakulima magonjwa wa shayiri na namna ya kuzuia magonjwa hayo katika katika mashamba yaliyopo Kijiji cha Emairete Monduli juu, mkoani Arusha. Wakulima hao huwezeshwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) katika uzalishaji wa zao hilo ambalo ni malighafi ya kutengenezea bia zinzozalishwa na kampuni hiyo.  Meneja wa Zao la Shayiri Dk. Bennie Basson akiwaonesha wakulima kijitabu cha muongozo wa kilimo cha shayiri katika Kijiji cha Emairete Monduli juu, mkoani Arusha juzi. Wakulima hao huwezeshwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) katika uzalishaji wa zao hilo ambalo ni malighafi ya kutengenezea bia zinzozalishwa na kampuni hiyo.  Meneja wa Shayiri wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) D.. Bennie Basson akizungumza na wakulima wa shayiri ktk kijiji cha Emairete Monduli juu, mkoani Arusha. Wakulima hao huwezeshwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) katika uzalishaji wa zao hilo ambalo ni mali

Rais Jakaya Kikwete azindua Chapisho la Tatu la taarifa za msingi za Sensa

Rais Jakaya Kikwete akitoa hotuba yake  kabla ya kuzindua Chapisho la Tatu la taarifa za msingi za Kidemografia,Kijamii na Kiuchumi linalotokana na Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 na Matumizi ya tovuti katika kupata  taarifa mbalimbali kuhusu Sensa ya Watu na Makazi kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwalimu J.K.Nyerere jijini Dares Saalam leo. Rais Jakaya Kikwete akitoa hotuba yake  kabla ya kuzindua Chapisho la Tatu la taarifa za msingi za Kidemografia,Kijamii na Kiuchumi linalotokana na Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 na Matumizi ya tovuti katika kupata  taarifa mbalimbali kuhusu Sensa ya Watu na Makazi kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwalimu J.K.Nyerere jijini Dares Saalam leo. Rais Jakaya Kikwete akitoa hotuba yake  kabla ya kuzindua Chapisho la Tatu la taarifa za msingi za Kidemografia,Kijamii na Kiuchumi linalotokana na Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 na Matumizi ya tovuti katika kupata  taarifa mbalimbali kuhusu Sensa ya Watu na Makazi kwenye ukumbi wa

DANA DANA ZAENDELEA! KAMATI YA RUFANI KUTOA KIAMA CHA MICHAEL WAMBURA KESHO

HATIMAYE  kamati ya rufani ya shirikisho la soka Tanzania, TFF imemaliza kujadili rufani ya mgombea wa urais katika uchaguzi wa klabu ya Simba sc unaotarajia kufanyika juni 29 mwaka huu, Michael Richard Wambura. Kamati ya Rufani chini ya mwenyekiti wake,wakili,  Julius Luhaziya imekaa kuanzia jana juni 9 mpaka jioni ya leo (juni 10) katika Hoteli ya Courtyard iliyopo Upanga , jijini Dar es salaam. Kikao hicho kilichojaa usiri mkubwa kimemalizika jioni ya leo na kufikia maamuzi juu ya rufani ya Wambura, lakini mwenyekiti wa kamati , Lugaziya ataongea na waandishi wa habari kesho mchana majira ya saa 6:00 katika ukumbi wa mikutano wa TFF.

HII NDIO SABABU ILIYOMFANYA TAJIRI RICHARD MOLLEL {PESA CHAFU)KUJIPIGA RISASI ARUSHA

Kijana matata Richard Mollel pesa chafu kajipiga risasi Arusha Yaani ndio nimetokea hapo kwake kwani ni ajabu kabisa.Alikuwa na girl friend wake kwenye gari kufika eneo la Mount Meru akagonga Hiace kwa nyuma gari  ikabonyea lakini yeye na mpenziwe wakatoka wazima bint anadai baada ya dakika km 2 akahisi kizunguzungu akaanguka chini kuja kushtuka anaona watu wengi na kijana naye kutoka hapo akatimka mpaka karibu na nyumbani kwake ndio kujipiga risasi na kufa.Sasa bint anaulizwa mlikuwa na ugomvi anasema wala yeye mwenyewe anashangaa kilichomkuta keshatoka mzima kwenye ajali kukimbia na kwenda kujiua.Ni kijana wa 86 yaani mdogo kabisa na ndio pesa imekubali na baba yake ni mgonjwa yuko hoi muda huo yenyewe alikuwa amepigiwa cmu na dada zake aende kumuogesha maana ni mtt pekee wa kiume na ndio alikuwa anaenda sasa hawajui ni kitu gani kilimkumba kuamua kujiua chanzo ni Kz Baba Precious Acasolid  tunazidi kupamabana kupata taarifa zaidi endelea kutufuatilia.......

Hizi hapa picha za Kili Music Tour Ilivyofunika Kahama

Na Kili Music Tour Kahama ilifunguliwa nae Shilole ambaye anawaonuesha mashabiki umahiri wake wa kulishambulia jukwaa.

HUU HAPA NDIO UKWELI KUHUSU KIFO CHA MWIGIZAJI MAARUFU NCHINI

Maehemu Mzee Small akiwa hospitali enzi za uhai wake. Stori: MWANDISHI WETU Msiba tena! Ukweli ni kwamba gwiji wa maigizo na vichekesho Bongo, Said Ngamba ‘Mzee Small’ ameandamwa na roho wa kifo kwa siku 790 hadi alipokutwa na umauti usiku wa kuamkia jana, Ijumaa Wikienda lilikuwa naye bega kwa bega. Mke wa marehemu Mzee Small, Bi. Fatuma Said akiwa na simanzi nzito. Mzee Small aliyekuwa na umri wa miaka 59, anakuwa mwigizaji wa nne kufariki dunia ndani ya siku 21 akitanguliwa na Adam Phillip Kuambiana, Sheila Leo Haule ‘Recho’ na George Otieno Okumu ‘Tyson’ ambaye bado hajazikwa huku kwenye michezo kukiwa na pigo la kuondokewa na Ally Hassan Mwanakatwe na Gebo Peter. ALITESEKA SIKU 790 Kabla ya kukutwa na mauti kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar, Mzee Small aliteseka kwa miaka miwili na miezi miwili, jumla ya siku 790, ambapo alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi au kupooza (stroke). Mzee Small akiwa nyumbani kwa

soma KURASA ZA MBELE NA NYUMA ZA MAGAZETI YA LEO